top of page

Unabii 100 "Acheni NIwapime Katika Mizani"


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 1 Oktoba, 2020


Maandiko Husika


Warumi 8:5-8

5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili;

bali wale waifuatao ROHO huyafikiri mambo ya ROHO.

6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti;

bali nia ya ROHO ni uzima na amani.

7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya MUNGU,

kwa maana haitii Sheria ya MUNGU, wala haiwezi kuitii.

8 Wale waufuatao mwili hawawezi kuMpendeza MUNGU.


Zaburi 26:2

Ee YEHOVAH, Unijaribu, Unipime,

Uyachunguze mawazo yangu na moyo wangu.


Ujumbe wa Kinabii


NInatamani urafiki, sio uadui. Uadui ni ya wavunja sheria, ya wasiotii, ya walazimishaji. Wavunja sheria na wasiotii wanapata miale ya jahanam. Lakini NIngependa kwamba mwe na uzima na mwe nao tele kabisa (Yohana 10:10). Mipango NInayo kwa ajili yenu watoto WANGU ni ya wema na sio ya uovu. MIMI ndiye MUNGU wa Tumaini. Msihangaike. Msitoe jasho wakati hamwezi ona jawabu, wakati yote inaonekana imepotezwa. Jua tu NDIMI NILIYE yuko na udhibiti. Jua tu macho yako yakikuongoza yatakusababisha upotoke. Ona katika ROHO. Abudu katika ROHO. Tembea naMI na NItatembea nawe. Wawili wanawezaje tembea pamoja ila kwanza wawe katika upatano (Amosi 3:3)?


Natembea nanyi kila siku. Je mnatembea naMI? Je mmejitiisha KWANGU katika njia zenu zote? Sio ninyi tena mnaoishi (Wagalatia 2:20)? NIko wapi katika maisha yenu? Wapi Taji LANGU? Je, linaheshimiwa na kutiiwa? Je, linastahikiwa? Au je, linatupwa chini kwenye sakafu, linakanyagwa? NInawatazama watoto WANGU. Jitiisheni KWANGU katika njia zenu zote na muone jinsi mnavyositawi (Mithali 3:5-6). Oneni jinsi tamaa zenu za mwili zinakimbia na kuwa kumvi katika upepo, bila umuhimu wowote.


Acheni NIwapime katika mizani, NIkamilishe kile kinachohitaji kukamilishwa. MIMI ni MUNGU. MIMI ni MKWELI. NIhitajini MIMI zaidi sasa kuliko wakati mwingine. Acheni kila pumzi yenu iwe JINA LANGU, kila tafakuri ya moyo wenu iwe JINA LANGU. MIMI ni MFALME (Zaburi 47:8). MIMI ni MWENYE ENZI KUU. MIMI ni MKWELI. NIsikizeni watoto WANGU, na msijue woga wowote. MIMI ni YEHOVAH – MPAJI wa mahitaji yenu YOTE. Selah.


Kuweni waangalifu. Kuweni wenye tafakuri. Jihadharini watoto WANGU wazuri sana, kwa maana adui wenu aenda akitafuta yule anaweza mmeza (1 Petro 5:8). Lakini hakuna cha kuogopa alimradi mnaweka macho yenu, mioyo yenu, akili zenu, kila kitu chenu kimekaajuu YANGU. MIMI ndiye MUNGU MKUU “NDIMI NILIYE”. Hakuna kinachoweza NIyumbisha. Hakuna ripoti inayoweza timua manyoya [fadhaisha] YANGU. MIMI ni MFALME (Zaburi 9:7-12). MIMI ni BWANA juu ya yote. NItazameni na mtii. Fanyeni NInavyofanya na hamtawahi potoka kamwe. Selah.


Mwisho wa Neno.

2 views

Recent Posts

See All
bottom of page