top of page

Unabii 14“NIruhusu NIkufunze Kupitia Enoki!”

Umepewa Nabii D’vorah kwa sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 8 Februari, 2019 (Ibada ya Shabbat)

Ujumbe wa Kinabii


Tulia Binti WANGU mpendwa, MIMI ni YAHUVEH, MIMI ni BABA yako. Ee, Nakupeleka kwenye mwinuko mpya wa imani yako! Je, utaNIruhusu NIkuvunje kidogo? Kukutenganisha kidogo? Nataka uchukue muda zaidi pekee na MIMI, kama Enoki.

Enoki anakufunza. Anatayarisha BABA yako EZRA. Enoki ni mwalimu wako wa kibinafsi kwa sababu wito wako unafanana [na wake]. Naam, NIna BiArusi mmoja, lakini umoja wa jicho na ulinganisho na MIMI utakuwa sawa. Chukua muda zaidi katika Uwepo WANGU. Nakuamuru hili. Nakufunza kuweka mwili wako chini. (Naona Enoki akisema, “Acha Nikufunze.”) Je utaNIruhusu NIkutakase zaidi? Lazima upitie katika majaribu na lazima ustahimili. Kumbuka Yosefu – ustahimilivu ni dawa yenye uwezo.


(Naona maono ya YAHUSHUA nami Tukicheza dansi katika nyota pamoja. NDIYO! Nitakuruhusu unifunze Enoki, fanya vile ABBA YAHUVEH, YAHUSHUA, IMMAYAH WAnakuamurisha na nitafuata! Onekana kwangu! Nifunze!)


NItatuma Manabii njiani, kama tu vile NIlifanya na Moshe, kukusaidia. Unaona, hii inanNIletea faraja! MIMI NDIMI NILIYE Binti WANGU mpendwa D’vorah!


Uta na lazima ujifunze kule, kuweka chini mwili, kunakaa vipi kwa kweli. Kila wazo, nia, tendo, litakuwa katika roho. Ingia tu katika Uwepo WANGU asubuhi na NItakupeleka kwenye mwinuko mpya. shetani anaogopa hili kwa sababu sikuzote ameona utengano WANGU ndani yako. Uwezo WANGU umewekwa katika sauti yako. Hiyo ndiyo maana lile Neno limezungumzwa ndilo liko tele sana mara nyingi. Ee, tangaza utukufu WANGU na sauti yako! Ee, shetani anachukia sauti yako! Kwa maana unaitumia tu kwa ajili YANGU! Sasa NIpendeze mno MIMI, YAHUVEH, na sifa! Wewe ni WANGU! MIMI ni Mpendwa wako! NInanyesha juu yako na NInatuliza hofu zako na NInatuliza dhoruba. Kumbuka Zaburi 91. Kipenzi, upendo WANGU kwako hautawahi pita. NIKO hapa. MIMI ni YAHUSHUA wako na wewe umetangazwa WANGU!


MwanaNGU, nena Maneno YANGU! NImekuita MwanaNGU! Kazi nzuri sana! MIMI, YAHUVEH, Nasema, ‘Umefanya vyema kusoma Neno LANGU!’ Endelea MwanaNGU! Watie moyo na Andiko LANGU kila siku. Nina zawadi nyingi za ajabu zimehifadhiwa kwa ajili ya kila mmoja wenu, kama lakini tu mtaNIngojea. NIngojeeni saa 1 kwa siku asubuhi na mtabarikiwa.


Enoki ni Nabii WANGU kutoka nyakati za mafumbo! Maana D’vorah, NItakufunulia siri zote za mawingu na NItakufunulia pale upepo ZANGU zimehifadhiwa (1 Wafalme 8:38, Marko 11:23, Kutoka 14:21, Mathayo 14:29, Marko 4:39-40), 1 Wafalme 17:1). Usiwe mzembe, soma Neno LANGU na soma Enoki! Hii itaamsha upako WANGU. Hili linaenda kwako pia Shimshon! Ee, Hannah, kazi bora sana Binti YANGU! Wewe endelea kuandika Maneno YANGU na kupenda Nafsi-mwenzi wako na Kaka na Dada zako, na NItakubariki.


BABA EZRA – fuata mfano WAKE Watoto. Jificheni chini ya mabawa YAKE. Penda kama vile BABA EZRA Aliwafunza. MIMI huchoka na kuJIrudia. Ee, njooni KWANGU! Acheni NIwafunze jinsi ya kupenda bila ya ubinafsi. Kazi nzuri MwanaNGU Shimshon! Kazi umefanya vizuri leo. Inamisha sikio lako, MwanaNGU. NItakuonyesha cha kusema. NItaweka Maneno YANGU katika mdomo wako! Niite katika ukataji tamaa wako na NItakuonyesha mambo makubwa na ya ajabu! NIonee shauku na NItakufunulia uso WANGU – takubadilisha milele. Wewe ni wa thamani MwanaNGU. Endelea kujitahidi kuishi Takatifu – katika Usafi na Utakatifu.


Msiwahi jinajisi – na NIzangumza na wanaume na wanawake wote – na unajisi wa nafsi. Ee jinsi NInavyowapenda! Nyinyi ni WANGU! Nyinyi nyote! Na NInawatia muhuri siku hii, sasa semeni ‘Naipokea’ na mbarikiwe! Hallelu YAH! (Nasikia Mbinguni ikisema hilo)


Pendo, Ufalme wenu,


YAHUSHUA


Mwisho wa Neno

0 views
bottom of page