Umepewa Nabii D’vorah kwa sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 9 Februari, 2019 (Ibada ya Shabbat)
Ujumbe wa Kinabii
(NIliendelea kusikia kuhusu Kutawaza ambao ungefanyika jana. Niliuliza YAHUSHUA kuuhusu na nikasikia Neno lifuatalo)
NItatawaza sauti zenu kuNIimbia sifa na viongo vya thamani (Zaburi 8:2, Mathayo 21:16). Si sauti za kawaida. Makuhani, nyinyi ni kama Makuhani WANGU (1 Peter 2:9). Ee, NIsifuni. NIsifuni Watoto WANGU! NInashika ufunguo wa kipawa cha muziki. Mwana, una kipawa hiki na unapaswa kutumia sauti yako kuNItukuza MIMI. MIMI ni YAHUVEH BABA yenu na Napenda kila mmoja wenu sana. Siri iko katika ufunguo WANGU.
Utatengeza video kuhusu hili na umetiwa mafuta kuimba. NItakutumia Binti kufikia mamilioni za nafsi kupitia muziki. Zile nyimbo NImekupa ukiNIsikiza jinsi ya kuzifanya, utashangaa na kile kinafanyika mara zinapoachiliwa kwenye YouTube.
Niko nawe na NItakuonyesha jinsi ya kufanya hili. Jifunze muziki WANGU. Uliza Malaika wa Utukufu na Sifa kuja na kukuonyesha jinsi ya kucheza. NItakutia mafuta wewe na dada yako kimiujiza na NInawataka mfanye nyimbo pamoja pia NInavyoongoza. Huu ni wito wenu.
Ee, shetani anaogopa hili!
Sasa NIsifuni kutoka chini ya nafsi na NIlilieni na sauti yenye shauku mnaposifu. Nazungumza na Watoto WANGU wote: mnapoNIsifu, NInapendezwa sana. Kumbukeni tu Watoto WANGU mliotiwa mafuta, kila mmoja wenu anatembea katika Roho YANGU MIMI. Kila mmoja wenu ana upako wa kipekee na NImewaita kuwa kama Makuhani mbele ZANGU. (1 Petro 2:9)
Hili si jambo la kawaida! Ee, hili si jambo la kawaida! Kwa hivyo NIsifuni. Furahieni! NItawafunulia Zaidi Watoto WANGU wachanga! Nisubirini. Kwa maana Roho ya Ushauri ni wewe Binti YANGU (ADONAI YAHUVEH Anazungumza na binti YAKE). Na iliobaki NItafunulia dada yako. NInafunulia siri ZANGU Manabii WANGU na mafumbo yaliyomo. Nakupenda Binti YANGU.