Umepewa Nabii D’vorah kwa sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 9 Februari, 2019 (Ibada ya Shabbat)
Maandiko Husika
Zaburi 91:14-16 “YAHUVEH Asema, “Kwa kuwa anaNIpenda, NItamwokoa; NItamlinda, kwa kuwa analikiri JINA LANGU. AtaNIita, naMI NItamjibu; NItakuwa pamoja naye katika taabu, NItamwokoa na kumheshimu. Kwa siku nyingi NItamshibisha na kumwonyesha Wokovu WANGU.”
Yoshua 23:8 “Bali mtashikamana kwa uthabiti na YAHUVEH, ELOHIM wenu, kama vile ambavyo mmefanya mpaka sasa.”
Ujumbe wa Kinabii
(Nilipokuwa nimekaa mezani, nikiongea na kaka [zangu], nilianza kusikia YAHUSHUA Akinena Neno kwa kwa Shimshon)
Ee, MwanaNGU Mpendwa, Shujaa WANGU, Samsoni WANGU wa Sasa, tiwa moyo! Niko hapa! MIMI ni YAHUSHUA. NIfikie MIMI. NIshikilie MIMI. Jione MwanaNGU ukiNIfikia. (Naona Maono ya kaka mmoja akiimba “nionyeshe njia ZAKO” lakini badala ya kuimba “njia” aliimba “nionyeshe uso WAKO.”)(Zaburi 27:8)
Nakufanya uwe na nguvu zaidi. Nakuimarisha. Nachukua Fimbo YANGU ya Mfalme na Naweka juu yako. Pokea Fimbo YANGU ya Mfalme. Hiki ni kifaa cha wakati. Hii haiji na gharama rahisi ya kutembea-bustani.
Tulia na jua SISI ni ELOHIM! Inua mikono yako MwanaNGU! TUtumainie! Pokea nguvu zako kutoka KWETU (Nehemia 8:10)! Wahaka, TUtaiondoa kama utaNIruhusu kukubadilisha. Ikiwa utaNIruhusu kukunyekeza kwa kiwango ili usitamani kuenda kwa sababu inaumiza mwili na inafanya wengine wajikwae lakini ee MwanaNGU, hauwezi ona jinsi ni muhimu mapenzi YANGU yatendeke, licha ya kile wanaume na wanawake wanafikiri?
Hata dada yako alipitia makaa ya moto na iliNIbidi NImvunje na bado Nitamvunja ikiwa hataNIruhusu NImkunje bila roho ya kulalamika, kunung’unika. Usifanye chochote na roho ya kulalamika, kunung’unika. Inua malango yako KWANGU MIMI MwanaNGU! NItakusaidia. Maana haisemi katika Neno LANGU, “Msaada wangu watoka kwa BWANA YAHUVEH?” (Zaburi 121:2)
MwanaNGU, Shujaa WANGU wa sasa, inuka! Nazungumza na roho yako na NInaimarisha nafsi yako na roho yako na mwili lazima utii. NInakufundisha jinsi ya kusulubisha mwili pia – jinsi ya kuweka chini kiburi, tamaa, uabudu sanamu, njaa, usingizi, ubatili wote, na yote yanayotenganisha mwanadamu NAMI. Je, utaNIruhusu MwanaNGU? Najua moyo na nia zako, lakini MwanaNGU, unapouliza “Mbona?” ama unatafuta kuelewa na unajua hivi vitu, unaamsha tu roho ya kulalamika, ya uchungu.
Badala yake, NIshikilie MIMI. NIone uso kwa uso na NIwaze MIMI mbele yako na Fimbo YANGU ya Ufalme NIkikuimarisha kama vile NImefanya siku hii. Ee Mtoto WANGU mpendwa, utaua simba za kiroho na utaona ushindi katika sehemu zote za maisha yako na maisha ya Kaka na Dada zako!
NInakujaribu MwanaNGU. NInakufundisha. NInaona umbali gani utakunjika bila kulalamika. Je, si ni mapenzi YANGU yatimie? Weka chini matamanio yako yote kila asubuhi kama vile tu umefanya na NIshikilie MIMI – matakwa YANGU, matamanio YANGU na salimisha matakwa yako na NItakuonyesha ushindi mkubwa.
NInazungumza hili Neno, ili utiwe moyo ili uangalie nyuma na ujue kwamba MIMI pekee YANGU ni Mpenzi wa nafsi yako na NInajali kuhusu kila kitu unafanya. NInakutakasa katika tanuri ya moto. NInakujaribu MwanaNGU mwaminifu. Endelea kujitahidi kutii na NIshikilie MIMI, UPENDO wako wa KWANZA, MSAIDIZI wako, MKOMBOZI wako, NGOME yako, MUNGU wa Wokovu wako, ELOHIM wa Ulimwengu!
Sasa, NIsifu MIMI na TUimbie wimbo, kwa maana TUnapenda unapotuimbia na moyo wa shukrani!