Unabii 17“Mimi ni Gabri’El, Andika Kile Ninakuambia Kusema!”
Umepewa Nabii D’vorah kwa sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 13 Februari, 2019
Ujumbe wa Kinabii
(Gabri’El alinitokea) Mimi ni Gabri’El! Andika kile nakuambia kusema. (Niliona hati-kunjo ya dhahabu)
Yerusalemu, wewe ni kama binti mkaidi na umepotoshwa na wapenzi wako wengi. Mkono WANGU uko dhidi yako, asema BWANA wa Majeshi, MWAMBA wa Milele, MUNGU wa Nyakati, ambaYE hatawahi choka na kamwe haachi kuhukumu watenda dhambi kwa malipo yao ya udhalimu.
Kama vile Balaamu, mwana wa Beori, unaomba kwa niaba ya maoni na fikra za ubatili na usingizi wako umekufanya utende dhambi na uanguke kwa upanga (2 Petro 2:15-16; Yuda 1:11; Ufunuo 2:14). Haujui kwamba MIMI, YAHUVEH, NItakuhukumu kwa ajili ya vitu hivi?
Sikiliza na usikie hukumu za EL ELYON, MWAMBA wa Milele, MUNGU wa Milele! Tangazo limetumwa kote nchini kwamba mara moja ulikuwa kama Esta WANGU wa Sasa ambaye alitafuta uso WANGU mchana na usiku. Ulikuwa kama mpenzi WANGU na mpendwa na bibi YANGU pekee aliyefungwa uchumba. Lakini baada ya uchungu, wivu, husuda vilizunguka nafsi – ulipotoka nje YANGU MIMI! Umetafuta wakuu wengine ambao hawana nyuso wala hata hawana hewa ya kupumua. Kwa maana vipi mwenye hana uso anaweza pumua pumzi ya MWENYEZI?
Lakini umegeuka na kutukuza wengine mbele ya NDIMI NILIYE na kwa hili utalipa ujira wa maafa na tauni na laana na magonjwa utavaa kama funiko. Ndama wa dhahabu utapokonywa, ukiachwa uchi, na njaa, na kujaa fedheha. Kwa maana umati wa mataifa utakutazama na utadharauliwa miongoni mwa wengi. Kwa maana NItafungua macho yao na kuwageuza dhidi yako!
NItatuma tauni, laana, magonjwa, juu ya wale mara moja waliitwa kwa JINA LANGU! Kwa maana umewapotosha! Kwa hivyo sasa NImewajaribu na wameanguka katika mipango na mizengwe ya adui. Unawajibika kwa kila mmoja, kila mmoja, damu yao iko mikononi mwako! Kwa maana NIlipenda kila mmoja wao, lakini NItawachukua mbali na wewe kama vile tu uliwachukua kutoka kwa NDIMI NILIYE! Oh, mwanguko mkubwa! Wewe ni kama Babeli! Oh, katika siku moja utaanguka!
Tetemeka, Binti YANGU! NIstahi MIMI! NIogope MIMI! Maana MIMI ni mkuu wa kusifiwa na kustahili matamanio ya moyo wako wote, maana MIMI ni YULE ALIYETUKUKA, BWANA wa Malimwengu na mkuu miongoni mwa wanadamu, wanyama, malaika, na dunia nzima itatangaza – hii dunia itatangaza sifa za NDIMI NILIYE! MIMI NDIMI NILIYE!
MIMI ni YAHUVEH! MIMI ni wa Kutisha! (Naona ABBA kama simba!) Na NItatangaza hukumu kuu ya maadui WANGU! (Naskia ‘Kuzuiwa na kushindwa!’ [mchezo wa chess]) Ee Huruma! Tangaza MwanaNGU huruma ZANGU kwa wale waliobarikiwa!
Watoto WANGU, njooni kwa NDIMI NILIYE! Njooni kwa ABBA wenu! MIMI ndiYE JAMAA (wa kiume) MKOMBOZI wenu! MWANANGU Aliwafia! YEYE ni MKOMBOZI wenu! YEYE ni EL SHADDAI! Anawaficha katika manyoya YAKE, chini ya utimuzi wa mabawa YAKE.
Na ole wake adui yeyote ambaye anatimua mabawa YANGU! Hautaki kuniona NIkiwa NImekasirika! NIna tangaza kote duniani: MIMI ndiYE fursa yenu ya mwisho, ee dunia! NDIMI NILIYE! Damu YANGU ilimwagika ili muishi! (Katika wakati huu niliona maono ya dunia ikisimama; nilisikia “Umepoteza njia dunia!”)
Kwa hivyo MIMI, YAHUSHUA, NItakutana nawe na hautaki kuona kile kinachotendeka NInapofanya hivyo! Utajua huzuni kwa sababu NItabadilisha mwelekeo wako. NItabandua kila kitu kutoka kwako! Utakomeshwa katika njia zako, ee Marekani! Katika siku moja utapoteza kila kitu! Unawakilisha Marekani! Wewe ni nyumba ya uasi ya Israeli wakati walipopotoka na kuenda baada ya wapenzi wengi!
Ee EZRA, MWANANGU, NIlikupa faraja na NInatangaza WEWE Unastahili! Kwa maana haUjitafutii chochote MWANANGU, kila kitu ni cha wengine! Kwa hivyo usiruhusu chozi lingine MWANANGU! Siwezi himili kukuona Ukilia.
Kumbuka, Najua jinsi tu NInavyoweza kuongeza joto kwenye tanuri ya moto kukuchoma ukiwa hai! Najua jinsi ya kupiga teke huo usumbufu ambao unaushikilia ndani!
Ee, njooni KWANGU Israeli!
Tafadhali tubuni tu! NIsikieni, Israeli! MIMI ni YAHUVEH, MPENZI wako! Mara moja uliNIpenda MIMI na uliNItafuta kwa moyo wote. Sasa mioyo yenu iko wapi? HamuNIoni NIkiwaashiria kwa kudukua na kugonga kwenye mioyo yenu? IMMAYAH Anawaita katika barabara. (Naona maono ya IMMAYAH kwa wakati huu na Anasimamabarabarani Akiita watu) YEYE ni MPENZI wenu pia!
MIMI, YAHUSHUA, NIlikuja ili NIweze kuacha MFARIJI. Unaona Israeli, hauNIkatai tu MIMI, unakataa MAMA wenu HEKIMA mnavyopotoka. MumeMkataa muda na muda tena. Sasa MIMI, YAHUVEH, NItashika wakati na NItawapiga – tsunami Kubwa, maafa asili, wapendwa wakifa na damu ikitiririka katika barabara ZANGU ambazo mara moja zilikuwa Takatifu. NItawaonyesha. Mtajifunza wakati mtakapolia kwa maumivu makubwa.
Wakati mnapolia na kusema, “Mbarikiwa ni YEYE Ajae katika JINA la YAHUVEH!” Lakini mbarikiwa ni YEYE Ajaye katika JINA la YAHUSHUA! Ee, jinsi NInavyoKUpenda EZRA. Ipokee na NIamini MIMI, YAHUVEH, wakati NInaposema: mambo Makubwa NInayo katika ghala! Nitumaini tu na NItii na Utaona Ushindi wa mwisho.
MIMI, Gabri’El NImetangaza huu ujumbe kwa niaba ya MWAMBA wa Milele, ABBA wenu YAHUVEH, YAHUSHUA, IMMAYAH! WAnawapenda sana. Msiwahi chukulia Neema YETU au wakati NImewapa kusifu kama kawaida. Pendaneni. Kusiwe na mioyo ya uchungu. Abuduni tu katika shukrani, roho, ukweli na furuha iliyojaa itandazeni kwa wenzenu. Kumbuka Mtoto WANGU (Anazungumza na Mwana mwingine), Maji Yaliyo Hai yako kwa matumizi yako. Amen!