top of page

Unabii 18 “Msichanganye Nyama na Maziwa na Bidhaa zake"

Updated: Oct 21, 2020

Unabii 18“Msichanganye Nyama na Maziwa na Bidhaa zake – Hii ni Sheria ZANGU za Kosher! Asema YAHUVEH wa MAJESHI!

Umepewa Nabii D’vorah kwa sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 14 Februari, 2019


Muhtasari


Kukupa wazo ya mbona Unabii huu ulitokea, kuna tamaduni ya Kiyahudi kwamba “kutokuchanganya nyama na maziwa na bidhaa zake”, na ilitokana na Kutoka 23:19. Torah inatuamuru: “Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake” (Kutoka 23:19). Torah inapiga marufuku kukula nyama na maziwa kwa pamoja, na hata yapiga marufuku kitendo cha kuvipika pamoja (pia kutoa faida fulani kutokana na mchanganyiko kama huo). Kama kinga, Wahenga walikataza kukula nyama na maziwa na bidhaa zake mlo mmoja, au kuvitayarisha na vyombo vile vile. Kwa hivyo, jikoni ambamo ni kosher lazima liwe na seti mbili tofauti za sufuria, vikaango, sahani na vyombo vya fedha – moja ya nyama/ kuku, mabata n.k. na hiyo nyingine ya vyakula vya maziwa.


Ujumbe wa Kinabii


(Nilikuwa nimekaa kwenye paja la ABBA YAHUVEH Mbinguni na Alikuwa na huzuni. Aliniambia kwamba sina wazo kuhusu uchungu ambao Anateseka. NiliMuliza, “Naweza fanya nini Kukufariji?” Alinionyesha Watoto WAKE wakitumikiana katika maono Mbinguni nilipokuwa nikiketi kwenye paja LAKE, na Akasema, “Mnaweza tumikiana kama Watoto WANGU.”

Halafu nikauliza Paulo – kwa sababu Mtume Paulo aliingia katika hicho chumba – “Paulo, unataka kutufunza nini?” Akasema…)


Ufafanuzi wa Tanakh (Bibilia). Ee, nasikitika! Nasikitika na jinsi wanavyogeuza maneno yangu na kudai nilisema tusishike Sheria za Torah na Sheria za Kosher!


‘Usichanganye nyama na maziwa na bidhaa zake’ ni Sheria ZANGU za Kosher, Asema BWANA YAHUVEH wa Majeshi, MWAMBA wa zama zote, MUNGU wa Shalom. Ni kisingizio kusema kwamba mimi sikufanya vitu hivi wakati nilikuwa mwangalifu wa wote. Usidharau mianzo midogo, mpendwa.

Mimi ni Paulo, na mimi ni yule mwanaume aliyesamehewa. Usiwahi tazama nyuma kwa yaliyopita. Kwenda mbele Binti. Unataka ujue jinsi mimi, Shaul, nilifanya? Sikuwahi kumbuka maisha yangu ya nyuma wala sikuyafunga katika yale mapya.

Unahitaji Maji YANGU Yaliyo Hai, Asema YAHUVEH, kufanya ubongo mpya. Wakati uchovu unakuja juu yako na unahisi mchovu, NIpe kelele ya sifa, hata ikiwa ni akilini – na NItainua shela ya giza ya usingizi inayofunika ubongo. Shika kila wazo tiifu chini ya mamlaka YANGU na NIpe mamlaka ya kufanya hivyo.


Ee, jinsi NInavyokupenda! Jinsi NImekosa wakati wako wa pekee na MIMI YAHUVEH, na MIMI YAHUSHUA! Pata kuTUjua zaidi Binti! Ee, jinsi NInavyokupenda! Wewe ni wa thamani machoni MWANGU na macho yako ni macho YANGU na NItakuhimili na kukufunika na kukuficha chini ya Mabawa YANGU ya Utukufu. Nakupenda tunu WANGU.


Mwisho wa Neno

9 views0 comments
bottom of page