top of page

Unabii 16 “Dunia, Sikuwapa Mushtara Muende Huko!”

Updated: Apr 14

Umepewa Nabii Hannah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 24 Februari, 2019



Ujumbe wa Kinabii


(BWANA YESHUA shiriki siri ZAKO nasi…)


Ee Nabii WANGU, tamanio la Moyo WANGU. NItafunua kile kiko moyoni MWANGU siku hii. NInatamani kuosha, NInatamani kutakasa, Natamani kukomboa wanadamu wote, wanavyotamani. Lakini jinsi wachache [tu] wanaotaka kukombolewa siri zao zilizofichika! Wanaruhusu wale malaika walioanguka kuingia, na hawaNIruhusu MIMI. Ni nini chenye giza zaidi KWANGU MIMI kujua, Watoto wapendwa? Kwa hivyo kiri woga wenu mmoja kwa mwenzake. MsiNIkosee, msikosee ROHO MTAKATIFU WANGU.


NIgeuzieni MIMI macho, YESHUA HAMASHIAKH wenu. Dunia inatazama kupaa kwa mwengine, lakini hiyo si ya ROHO WANGU, lakini ya mpinga-kristo (‘unyakuzi’ wa Mwali wa Buluu). Wanatazama teknolojia za dunia na kuona kile Elon Musk anazindua. Kuelekea Mushtara? Ni nini hiyo? Hakuna chochote cha kuvumbua kwenu [kwenye Mushtara] ila utupu na virusi. SIruhusu mwanadamu kuenda kwenye Mushtara! Sio mpaka wenu NImewawekea. Sio.


Na hakutakuja kuwa bora, dunia! NImekasirika! Kwa maana mnatazama hiyo sayari nyingine, lakini ni nini ilifanyika na sayari Nimewapa sasa? Eeh? Dunia inapuuzwa, ukiwa. Je, ni hilo NImewaita kufanya? Kuziangamiza? Ee, lakini wengi sana wataangamizwa badala yake na sayari YANGU, sio kwa sababu sayari yenyewe ina roho ya kutenda kama vile mizungu inaamini, lakini kwa sababu NItakuwa Naita Nyota ZANGU kuchukua hukumu juu ya yote ambayo yamefanywa kwenye Sayari YANGU Dunia!


Kwa hivyo tubuni leo kwa kuamini tofauti kivyovyote! Kwa kuamini hakuna MUNGU, hili ni chukizo KWANGU! Shikeni mawazo yenu, shikeni mawazo yenu kwa nguvu KWANGU MIMI. NInatubu kwa kuwatengeneza ee wanadamu, lakini kwa sababu Najua 144,000 na 144,000 WANGU wangezaliwa, halafu NInatuliza hasira YANGU. NIliregesha hukumu YANGU nyakati nyingi sana, nyakati nyingi sana katika historia zamani. Avraham aliNIsaidia kuregesha hasira YANGU, Haruni alituliza hasira YANGU baada ya toba yake kwa ajili ya Israeli katika ile nchi ya jangwa.


Eh Israeli YANGU, NIrudie na ufanye kile Israeli ya zamani ilifanya! NIgeuzie MIMI moyo na macho yenu. Tazama na uone – Utakatifu wote na nchi Takatifu ambayo mara moja ilikuwa yako, sasa ni ukiwa na ni ya mwingine. Je, utatubu na uNIgeukie siku hii? Je, utafanya hivyo?


NInajua jawabu tayari. Na hiyo ndiyo maana lazima NIchukue Biarusi WANGU kwanza kabla ya mateso yoyote yanayokuja chini kwenye hii Dunia. Lazima NIpeleke Biarusi WANGU pahali salama kwanza.



Mwisho wa Neno


Muhtasari:

*Mushtara – ni sayari ya nne katika mfumo wa jua, iko baada ya Dunia

 

18 views

Recent Posts

See All
bottom of page