top of page

Unabii 17 “Tumaini na Mhimili Jaribio la BWANA!"

Updated: 4 days ago

Umepewa Nabii Hannah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 24 Februari, 2019


Muhtasari

Hukumu itakayokuja kama Siku 3 za Giza itakuja tena na katika ufunuo 6:12 “Kisha nikatazama na wakati MWANAKONDOO Alipovunja Mhuri wa sita, kukawa na tetemeko kubwa la ardhi; jua likawa jeusi kama gunia la manyoya; mwezi wote ukawa mwekundu kama damu.” Hili ni tukio lenye maafa linalokuja, lilia BWANA YESHUA leo kwa ajili ya Wokovu, kesho inaweza kuwa ushachelewa zaidi!


Ujumbe wa Kinabii

Ee Duniani, wengi sana watakufa, wakati wa Siku 3 za Giza. NInaporuhusu giza kuja chini kwenye hii Dunia kwa ajili ya mioyo ya uovu ya wanadamu. “Hukumu!” –Atangaza Nabii WANGU Ezekieli ndani ya Korti YANGU ya Hukumu! (Muhtasari: BWANA Alinionyesha kwamba Nabii Ezekieli ndiye mkuu wa Korti ya Mbinguni ya Hukumu. Roho zao bado zinafanya kazi Mbinguni ingawa miili yao ilikufa.)


NInatangaza! Hukumu na baraka siku hii kutoka Mbinguni kuelekea kwa Dunia! Malaika wa Hukumu karibuni ataleta chini mwanzo wa mapigo 10! Yataua wale wote wasio na Damu ya YESHUA, MWANAKONDOO kwenye mhimili wa mlango wao! Na juu ya adui wako – hukumu kuu itakuangukia mara 7 kali zaidi! MIMI pekee YANGU ndiYE MWENYEZI, sio wewe adui unayecheza mungu. Tubu siku hii, toa kwa upesi chachu katika kambi yako!


Moyo WANGU uliwastawisha siku zote. Mnasafiri ndani YANGU kama mtoto mchanga katika BABA daima mkitafuta upendo wa BABA. Na NIliwapa Hazina YANGU, YESHUA. Anastawisha akili, mwili na nafsi yenu. YEYE ni Mshika Sheria wenu, Akiwashikilia kwenye njia nyoofu. NIliwafunza Mbinguni jinsi ya kufanya kazi YANGU, je mwakumbuka?


Nyota YANGU, angaza kwa ajili YANGU, unaposifu, omba na kupiga vita. NIligandamanisha ndani yako Kito CHANGU kikuu kabisa na chenye uweza. Unaweza kustahimili maelfu ya nyuzi za Selsiasi, na nyuzi hasi za hali ya hewa ya baridi. Lakini hauhangaiki na uliNItumainia na yote unayofanya.


Watoto, msiwahi kuwa na wasiwasi juu ya chochote ambacho NIliwaletea. Lazima mweze kustahimili maelfu ya nyuzi za Selsiasi na maji ya baridi yenye kimo kikubwa kabisa.


Jinsi Navyowathamini, mnapoNItazamia MIMI Mbinguni. Vile nyinyi nyote hamtawahi NIwacha MIMI. Moto WANGU ni nyuzi milioni elfu 10, nani anaweza stahimili joto hilo? Ee lakini yule ambaye amepitia moto na kuwa dhahabu iliyosafi kabisa ya yote.
Mwisho wa Neno

13 views

Recent Posts

See All

תגובות


bottom of page