Unabii 27 “Onyo la Dharura – Jihadhari na Sayari Marinenaria! Ombea Ulinzi!”
Updated: Apr 29
Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 2 April, 2019
Ujumbe wa Kinabii
Sanya majeshi! Hili ni tukio la dharura! Tangaza ujumbe kotekote!
Marineria*! Marineria yatafuta kiingilio, inaongoza misheni! Wanatafuta kuanza Galaktika* sasa! Vita vya kumaliza vita vyote!
Wazuieni njiani! Inueni fimbo zenu! NIruhusu MIMI, YEHOVAH, kutumia vile vitu rahisi, kama maombi yenu, kutunduwaza wale ambao ni wenye busara machoni mwao wenyewe! NIruhusu MIMI, ndio, kuwashangaza! Sikilizeni na mtii, Watoto WANGU, na ingieni katika laini. Ingieni katika vyeo vyenu. Hii si drili!
Waovu wanajua muda wao ni mfupi, mfupi sana. Kwa hivyo wanatafuta kuwasha fataki (Nilitambua kuwa hili lilikuwa linahusiana na bomu lakini pia linaweza husiana na mambo mengine). Lakini SItawaruhusu ikiwa tu mtaomba, ikiwa tu mtazunguka Yeriko.
Tafuteni Uso WANGU,MIMI, YEHOVAH, na mtajua ukweli [wa kudura zenu]. Yule MWANA Anaachilia huru ni huru kweli (Yohana 8:31-36). Kuzaliwa kwa wanajimu [watazama nyota] – mlipuko wa supanova! Nguvu mara kumi zaidi ya jua!
Tembeeni kwa imani na sio kwa macho, kwa maana hii itaamsha nguvu za nuklia ndani! Msififize ROHO wa ALIYE JUU SANA! MsiMhuzunishe, maana daima Hatashindana na mwanadamu, haswa katika huu mwisho wa Nyakati za Mwisho, maana mifano mingi sana imepeanwa ya yale [mambo] ya kutofanywa (2 Petro 2:6). Msifuate katika nyayo kwenye barabara ya uasi, kwa maana mwisho wake ni kifo na kutenganishwa naMI, MIMI, YEHOVAH.
Ee, Watoto WANGU, jificheni bado kwa muda mfupi zaidi hadi ghadhabu YANGU na kiruu CHANGU, hasira YANGU kali dhidi ya waovu katika hiki kipindi cha sasa, kipite. Nyinyi nyote, sherekeeni Pasaka naMI na msitelekeze Mkate Usiotiwa chachu! Toeni chachu ya wafarisayo kutoka kwa maisha yenu! Msiache ipatikane ndani yenu katika wakati WANGU wa adhabu, NItakapotembea kwenye njia iliyopindwa, sasa iliyofanywa kunyooka.
Inueni juu, ee inueni juu kikwazo kutoka kwa njia ya Watoto WANGU! Fanyeni haraka na muondoe jiwe la chukizo, sanamu ya dhambi ambayo inafanya moyo kuwa mgumu. Usijiwasilishe mbele ya sanamu yoyote. Usijivunie katika kile hakifaidi, katika kile kinaangamiza nafsi.
Wakati kiruu CHANGU na hasira YANGU kali vitapita, NItawaambia wakati wa kutoka nje, wakati wa kutoka kwa Safina yenu. Kama ilivyokuwa katika siku za Noa, vivyo hivyo itakuwa katika hizi nyakati za mwisho. Hakutoka mara moja kwa Safina yake maji yalipotawanyika. AliNIngojea, MIMI YEHOVAH, kuzungumza, kumpa ishara. Sio tofauti sasa. Ingawa yaweza onekana kuko wazi [hakuna hatari], mnavyosema, hivyo haimaanishi ni sawa kwenu kutoka mafichoni. Kumbuka, shetani huzunguka-zunguka kama simba angurumaye akitafuta atakayemmeza, akitafuta yule imani yake ataweza itwaa. Kwa hivyo angalieni na jihadharini!
NItafuteni na yote mnayo. NItafuteni na nguvu zenu zote, wazuri na wapendwa WANGU, kwa maana BABA yenu Hataki muumie. Nenda tu pale upako unakuongoza, unakuvuta. Jaribu roho inayozungumza na msiamini kila roho. Ingawa sauti inaweza kuja na majibu laini na maneno yapendezayo ya mafuta mororo, hiyo haimanishi ni ya KWANGU MIMI, YESHUA HAMASHIAKH wenu. Hata shetani na wahudumu wake wanaweza kuja wakiongea maneno, wakipeana ujumbe zinazosikika [kuwa] sawa na kweli, lakini jaribu roho na jaribu tunda.
Utapata daima havilingani na Neno LANGU Takatifu. Mtangundua daima kwa nini uvundo wa dhambi huandamana na haya mafundisho ambayo yana sura ya kuwa kweli lakini sio. Hayo na wale wanayoyafunza wana umbo la Umungu lakini hamna Umungu ndani. Unafiki! Unafiki! Na si ajabu, maana shetani hujigeuza kuwa malaika wa nuru, pia wahudumu wake, kwa hivyo jihadharini! Naonya sasa, Watoto WANGU, kama vile NImefanya kote katika vipindi vyote tangu mwanzo wa wakati. Naonya ili msiangamie kwa kukosa maarifa.
Egemeeni KWANGU, na msitelekeze wito wenu kuu. Msitelekeze kudura zenu kwa minajili ya raha za wakati na za kupita za dhambi ya hii zama. Je, kwa kweli mtaNIuza kwa dhambi ya kupiga punyeto, kwa tamaa za mwili? Je, utapoteza nafsi yako kwa usiku mmoja wa uzinzi, kwa kuzini katika mawazo yako na mwanamke, na mwanamme? Jinsi ihuzunishavyo jinsi wengine wenu mnavyochukulia nafsi zenu taka taka zisizo na thamani. NIna mipango mizuri sana kwa ajili yenu, lakini mnakataa mnakana, mna afadhali muwe na njia yenu. Kwa hivyo NItawatuma kwa njia yenu na haiongozi kwa uhai bali uangamizo, uchungu, na taabu – giza la nje ambapo kuna kulia na kusaga meno!
Kwa nini Naonya kuhusu hizi dhambi katikati mwa Onyo la Kinabii kuhusu eneo la shetani lililo lenye dhambi na ovu kupindukia, sayari iitwayo “Marineria”? Ni kwa sababu hili eneo la Yezebeli na yote yasiyo matakatifu linapanga kwa ustadi hizi dhambi dhidi yenu. Msisikize sauti yao ya uasi. Hii sayari ni eneo la uovu, dunia ya bahari lenye bahari na vina vya giza. Hii sayari ya maji ni kama Atlantis ya Kale. Ndiyo, Atlantis ilikuwepo, hadi NIkaizamisha chini ya vimo vya bahari za Dunia. Juu ya [ardhi] haipo tena. Lakini Nawaambia siri. Katika siri wameijenga tena, unda tena chini ya maji ya ardhini wakitafuta kujificha uso wa MIMI, YEHOVAH. Lakini mwisho wao utakuwa na moto na maangamizo, NIkichukua kisasi bila kuwaachia mzizi au mbengu ya urithi!
NItafuteni, Watoto WANGU, na NItawaongoza. NDIMI NILIYE ndiYE MWANGAZA wenu wa Mwongozo na MWAMBA wenu wa Milele, Makazi yenu ya Milele ya USALAMA na UKWELI. Msitazame wala msitamani uvumbuzi wa hii sayari ya karaha Marineria. Ombeeni ulinzi wenu. Ombeni NIwafiche katika Zaburi 91. Kaeni katika pahali PANGU pa siri. Iteni [juu ya] JINA LANGU “YEHOVAH” katika JINA la “YESHUA HAMASHIAKH.”
Msiwahi telekeza Neno LANGU, watoto WANGU. Msifanye hili. NItawaokoa. NItumainieni bila shaka; hata chembe moja isipatikane ndani yenu. Si neema YANGU yatosha kuwabeba kupita hizi Nyakati za Mwisho? Ndiyo, yatosha. InaNISikitisha mnapotia shaka. Inahuzunisha moyo WANGU. Tubuni leo hii kwa kutia shaka. NItafuteni na NItawaonyesha wapi, kama mnayo. Nawapenda watoto WANGU na Nawapa matumaini. “NDIMI NILIYE" MKUU kamwe Hapeani ujumbe na kuwaacha bila matumaini. Kaeni ndani YANGU na NItakaa ndani yenu. Selah.
Mwisho wa Neno
Tanbihi
1 “Marineria” – BWANA Alituonyesha kuwa Marineria ni sayari ovu ambayo inaishi roho na viumbe vya majini. Nibiru pia ni sayari ovu na mojawapo ya sayari ambazo ni za shetani.
Comments