top of page

Unabii 45 “Jina la ‘Yesu/Jesus' SItaitikia Tena! YESHUA Ndilo JINA LANGU!”


Umepewa Nabii D'vorah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa Aprili 23, 2019


MUHTASARI: Onyo la MUNGU kwamba tena Hataitikia jina la “Yesu/Jesus" inahusu wakati ujao, ambao Mpingakristo atakuwa anatawala Duniani na jina la “Yesu/Jesus" litatumika na Mpingakristo. Kwa wakati huu YESHUA bado Anaokoa watu na jina la “Yesu Kristo".


Ujumbe wa Kinabii

(Nilijiona nikipaa kuelekea chini duniani tena, na nilitazama na nikaona vita na kulikuwa na kifaru kikubwa na kunaonekana kuna mtu muovu kabisa aliyevalia nguo zote nyeusi kwenye hususan hiki kifaru cha jeshi akipiga nalo watu wengine... nasikia “Vita na njaa kuu")


Marekani, enzi yako ya ukubwa imeisha! MIMI, YEHOVAH, NImesema mara moja tena kwamba NItachoma hiyo bendera ya taifa mnaloshika kwa dhati kwa mioyo yenu. (Wakati uo huo niliona moano ya bendera ya Marekani ikichomwa.) Na hivyo, kwa sababu mmeraruararua Sheria ZANGU na mmevunja mawe za Amri ZANGU 10, hata nyuma kutoka wakati wa Hakimu Jaji Roy Moore. MIMI, YEHOVAH Natikisa kichwa CHANGU katika kinyaa, kwa maana mnaNIchukiza sana, na NItageuza jicho pofu na sikio kiziwi wakati watoto wenu wenyewe wanachinjwa mikononi mwa jeshi la Urusi.


Marekani, mna rundiko la dhahabu lililohifadhiwa watu wa tabaka aali waovu na hamjui kwamba ushuru mnaolipa umechangia kwa ajenda yao, kwa njama na mipango yao miovu! Oh Marekani, MIMI, YEHOVAH, Natikisa kichwa CHANGU katika karaha kwa maana nyinyi ni waovu sana na hamjui tena kwamba msitari wa maadili umetiwa ukungu kabisa. Hamngejua dhambi hata vile hamjui kulia kwenu na kushoto kwenu, kwa sababu ya giza ya mioyo ya mwanadamu.


NImechukizwa nanyi, oh Marekani! Na kwa hakika NItawasaga! MIMI, YEHOVAH, NItachukua ngumi YANGU na kuwaponda! SIjafurahishwa! SIfurahishwi na teknolojia yenu iliyoendelea! Mizungu itakuja angani na kwa kihalisi itawakula mkiwa hai! Itaaibisha teknolojia yenu! Lakini mizungu tayari iko hapa na imekuwa ikiishi miongoni mwenu kwa siri na hamjui, maana wengi wa Wakristo wanalala na vivyo hivyo pia Bi-Arusi na Wageni katika njia nyingi!


Amkeni Watu WANGU!!!


Inukeni na mpokee mwito wa toba! Maana mnahitaji kujua kuwa MIMI, YEHOVAH, ni JAJI wa Haki Aishiye, ambaYE Atahukumu hasa nafsi zenu! Je, hamjui, kwa kusinzia kwenu, NItawahukumu kwa hili? NItawahukumu kwa kukosa kuomba na (kwa) uvuguvugu ambao NImeona katika makanisa, ijapokuwa mnaonywa kila wakati!


Kama vile Alama ya Mnyama inapokaribia na watesaji wa anga wanasonga karibu, mnajua kwamba mnahitaji Safina ya Usalama! Msijigambe na kusema, “Oh, tunakupenda Yesu!” kama hamNItii!


Tumieni JINA LANGU la Kiebrania! Kwa maana jina la ‘Yesu’ SItaitikia tena! ‘YESHUA’ ndilo JINA LANGU! Kuna wokovu katika JINA la Kiebrania la ‘YESHUA’ na hili ndilo JINA juu ya majina yote! NImekuwa na huruma, kwa maana wengi wenu hamkujua wala kuelewa, lakini kuweni na hakika na hili, ikiwa unasoma hili Neno unawajibika kwa kile unachojua!


Asante kwa kuNIsifu na KuNItafuta kwa ajili ya Neno hili. Fanya hili mara nyingi (hizi) siku chache zijazo na NItaitikia haraka. Nakupenda binti YANGU muhibu, mischana mdogo wa EZRA. Nyinyi nyote ni wenye thamani isiyohesabika KWANGU na siwezi wabadilisha, mmoja kwa mwengine. Nyote mnang’aa na nyote mnameremeta. Nyinyi nyote ni kama chemsha bongo moja kubwa na wakati vipande vilivyoisha vinakuja pamoja mtaona jinsi rembo picha NInayoona kwa kweli ilivyo. (Katika wakati uo huo, niliona wengi wetu tukiweka kipande cha mwisho cha chemsha bongo kwenye chemsha bongo iliyokamilika ya uso wa YESHUA.)


NInawependa!


Asema YESHUA.

Mwisho wa Neno

18 views0 comments
bottom of page