top of page

Unabii 40 “Shule Zitasimamishwa, Asema YEHOVAH!”

Updated: Mar 24


Umepewa Nabii Shema’YAH kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 1 Juni, 2019Ujumbe wa Kinabii


(Hili Neno lilikuja baada ya dada mmojakushiriki maono alipokea kutoka kwa YEHOVAH kuhusu shule zikisimamishwa kwa sababu ya machukizo ambayo yanafunzwa watoto.)


Naja karibuni mwanaNGU, usiwahisahau hili. Penda na ubusu ndugu zako. Busu lililotengwa kwa kila mmoja. Hii inasidia upendo kutiririka. Kumbuka, NIko ndani ya kila mmoja. Nawashukuru kwa kukusanyika NAMI, nyinyi nyote. MIMI sikuzote hufurahia makusanyiko haya. Haswa mnapoNIalika ndani. Na NIko nanyi sasa.


Ndiyo, shule zitafungwa. Na ni vile vile NImeonyesha binti WANGU.


Kwa maana hukumu imekuja, inakuja kwa hii nchi na nyingine nyingi. Kwa maana wametelekeza Sheria YANGU na hawafunzi watoto ukweli. (Kumb. 28:20) Lakini sio nyinyi. Kwa maana mnapaswa kuwa na Huduma ya Watoto. Ili watoto WANGU waweze kuja KWANGU; waweze kuNIbariki. Ili NIweze kuwabariki. Kwa maana hawa watoto wote ni watoto WANGU. Kwa maana wazazi wamewatelekeza kwa kuruhusu hili kufanyika (Zaburi 27:10) – kile kinachofunzwa shuleni. Na abadani SIwaachi waliotelekezwa. Kwa maana MIMI NDIYE Tumaini, juu ya yote.


Polisi shuleni hawafanyi kazi zao kulinda watoto. Wazazi wanaofanya kazi katika mfumo wa shule wanageuza jicho pofu kwa yale machukizo na hata kwa hiari wao wenyewe wanafunza huu uhalifu kwa watoto. Kila mtu yu mshiriki. Na hakuna anayesimama na kusema, “Hili ni makosa!” Hata wakati wengine wanajua tofauti ya lililo sawa na lisilo sawa. Na uo huo ndio mtazamo wa kizazi hiki. Wanaona kitu kibaya na wanajua ni kibaya na wanasema, “Oh ndivyo maisha...”, wana mtazamo, “Oh ndivyo maisha...” Hivyo basi wote watateleza hadi Jahanam (Walawi 19:17)!


Ni nini kinastahilisha katika haya maisha kuenda pahali pa laana ya milele? Pa adhabu ya milele? (Mithali 23:17-18) Wakati ulijua tofauti ya lililo sawa na lisilo sawa. Na yote ilihitaji ni muda mfupi sana, muda mfupi sana wa kusimama. Muda mfupi sana wa kufedheheshwa. Muda mfupi sana wa maneno machache mabaya. Muda mfupi sana wa kukodolewa macho machache matupu kusema, “Hili ni makosa!” Na hivyo basi, wanakubaliana nalo. Kwa hivyo basi, wanawezapata adhabu yake pia. Wanaweza kubaliana na adhabu yake pia! Na kwa wale ambao mnasikia sauti YANGU na mnakubaliana nayo, jueni tu kwamba SIwajui (Luka 6:22-26, Yohana 10:27-28, 1 Yohana 3:10). Kwa maana mnapaswa kuwa walinzi wa watoto. Na mnaNIsikia NIkiwalilia! NIkiwathibitisha (Yohana 16:7-11). UnaNIsikia NIkikulilia katika dhamiri yako. “Hili ni makosa!” Na hauna amani yoyote. Na hauna raha. Na hiyo ni kwa sababu unajua hili ni makosa!


Na NInao mjeledi mweusi, mshipi WANGU mweusi! Na kwa wale, na mnasema mnaNIjua, NInaenda kuwapiga mjeledi (Yohana 2:13-1)! NInaenda kuwachapa! Ili mjue tofauti ya lililo sawa na lisilo sawa. Na kwamba katika haya maisha, kwamba hakuna chochote kinachostahilisha kuenda Jahanam kwa ajili yake.


Na shule kwa hakika zitaanguka, haswa vyuo vikuu. Na mtachoma midomo yao. Kwa maana NInawatuma huko kwanza. Naja upesi kwa shule kuonyesha rehema YANGU, kuonyesha ghadhabu YANGU. Hukumu ZANGU dhidi ya mafundisho ya mapepo ambayo [ni makosa] yanayofanywa katika hivi vyuo visivyo vitakatifu. Ikiwa hamtatoka katika hizi shule, mtaangukia utawala wa mpinga-kristo ambao umekuja ukitafuta kuwafunza na kila uchafu na najisi kutoka Jahanam; kujaza akili yako na takataka kutoka Jahanam kuchukia jirani wako; kuua, kuiba na kuangamiza.


Kwa maana kuna ukomunisti katika shule. Ndiyo, kuna ukomunisti katika shule, na itaongoza kwa uangamizaji wako Marekani, maana wanapotosha vijana. Vijana wa Hitler, wanajaribu kuanzisha na kujenga tena. Na katika usikivu WANGU, wanaNIdhihaki (katika shule wanadhihaki MUNGU). Na Naja karibuni, kwa hivyo NIsikieni: kimbieni kutoka kwa hivi vyuo! Kimbieni kutoka kwa hizi taasisi, kwa maana zinatafuta kuwafungia ndani, kuwateketeza.


Mwisho wa Neno

2 views

Recent Posts

See All

Comments


Commenting has been turned off.
bottom of page