top of page

Unabii 52 ““Ee Israeli, Benjamin Netanyahu Si Rafiki Wa ELOHIM!”


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 15 Juni, 2019


Maandiko Husika


Waefeso 4:1-6: “Basi, mimi niliye mfungwa wa BWANA, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa. Kwa unyenyekevu wote na upole, mkiwa wavumilivu, mkichukuliana kwa upendo. Jitahidini kudumisha umoja wa Roho katika kifungo cha amani. Kuna mwili mmoja na ROHO mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja. Tena kuna BWANA mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, MUNGU mmoja ambaye ni BABA wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote.”


Ezekieli 20:38: “NItawaondoa miongoni mwenu wale wanaohalifu na wale wanaoasi dhidi YANGU. Ingawa NItawatoa katika nchi wanazoishi, hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtakapojua kuwa MIMI NDIMI YEHOVAH.”


Ujumbe wa Kinabii


Oh watoto WANGU, jinsi inavyoNIhuzunisha, jinsi inavyoNIumiza kuona moyo na hali ya Israeli Mpendwa WANGU! Kwa maana NIliangalia kuona ikiwa kuna tumaini nchini, lakini yote macho YANGU yanaona ni ubatili na mwuozo! Ubatili na mwuozo, asema Mhubiri!


Mababu zenu wanatazama katika hofu, kwa maana wanajua kile kitakachowapata. Bila kukoma wanawaombea, wakitafuta uso WANGU, wakitafuta uso wa MUNGU wao kwa suluhisho, kwa wakati wa mabadiliko.


Oh lakini watoto WANGU, vitisho vya vitisho vitawaangukia (Israeli) wakati hawatarajii kabisa. Kwa maana wataamini katika mkono wa mwili mgeni na wataachwa wametapakaa miongoni mwa milima yenu, oh Israeli! Msiamini katika serikali za hii dunia, oh Israeli. Msiamini katika serikali yenu, kwa maana si tayari NIshawaonya watawauza kama vile tu waliNIuza kwa fedha thelathini (Mathayo 26:14-16)?


Msitafute serikali za hii dunia kwa msaada wa kupona wakati wa hitaji. Tengeneza shida – toa suluhisho. [Tabaka aali katika hii dunia wako nyuma ya maafa mengi, vurugu (nyingi) katika mataifa. Wanasabaisha hii halafu wanatoa suluhisho, kama vile sheria za uovu, kwa madhumuni ya kuondolea watu uhuru. Hii ni tamaa ya mamlaka.] Kila kitu kimepangwa, watoto WANGU. Yote sivyo yanavyoonekana. Yote sivyo yanavyoonekana.


Mkono wa Moshe umeinuliwa mara moja tena. Fimbo ya hasira na adhabu YANGU umewekwa wazi. Uadilifu utajulikana mara moja tena kote kwa nchi, kote kwa Watu WANGU, kote kwa Makabila ZANGU. NInakusanya Watu WANGU, Naunganisha Makabila. Karibuni yatakuwa moja – vijiti viwili [kuwa] moja – Yuda na Efraimu chini ya paa moja, katika nyumba moja (Ezekieli 37:15-23). Kwa maana hakutakuwa tena na utengano katikati mwa Watu WANGU! Hakutakuwa tena na mfarakano na kutokuelewana! Hakutakuwa tena na Samaria na Yerusalemu!


Lakini kutakuwa na kundi moja, MCHUNGAJI mmoja – MIMI, YESHUA – imani moja, tumaini moja, ubatizaji mmoja – EKHAD (Waefeso 4:1-6). Someni Maandiko yenu, ee Israeli, na muone utengano huu ni laana. Kamwe Sikuwahitamani kuwepo na haya mashindano makali, hivi vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Watu WANGU. Ndiyo, waasi lazima wasafishwe toka kwa nchi lakini moyo WANGU unavunjika kwa yale NImeona.


NItafanya mambo yote mapya, kwa maana SIkusema kwamba wakati MIMI, hata MIMI, YESHUA, NItainuliwa juu kwamba watu wote watavutwa KWANGU (Yohana 12:32)? Kwa hivyo NIsikilizeni, ee Israeli, kwa maana Nafanya vitu vyote vipya. Yule NInayeweka huru yu huru kweli (Yohana 8:36). Furahieni ndani YANGU, ee Israeli – TORAH yenu ILIYO HAI!


NItaondoa waasi wote katika nchi (Ezekieli 20:38). Huyu Netanyahu si rafiki YANGU, Asema BWANA MUNGU wa Majeshi, ambaYE JINA LAKE pekee ni YEHOVAH MWEZA YOTE! Vita ndivyo anavyotaka? Basi vita ndivyo atakavyopata, NInaporarua maisha yake, NIkifumua mishono, mfumo wa familia yake. Atakuwa pekee yake na hawinde kwa maovu yake dhidi YANGU. NItamrarua toka kiungo hadi kiungo kwa uovu wake wa uavyaji mimba. Damu iko kabisa hadi kwenye hatamu ya farasi; damu inatiririka katika barabara za maisha yake na damu ya wasio hatia ikirowesha ardhi, ikirowesha mikono yake.


Kwa hili utalipa Netanyahu! Kwa woga, ufisadi, uroho, tamaa yako ya mamlaka, dhihaki ya Neno LANGU, na mengine mengi zaidi – utalipa na nafsi yako yenyewe! Ni wangapi umeua katika jina la faida na kupiga hatua kisiasa, kwa fedha zako tu [za ubatili]? NItafichua dhambi zako ili wote waone, maana unapotosha Kondoo na Wanakondoo WANGU wa kweli. Katika kiburi chako, unajiinua dhidi YANGU – MIMI, YEHOVAH.


Kwa hili utalipia! Muda na muda tena NIlinyosha mkono WANGU kwako, ee Netanyahu, ee Yuda (Iskariote). Kwa hivyo msililie tena walioanguka, watoto WANGU. NIpeni mizigo yenu – MIMI, YEHOVAH, BABA wenu MWENYE upendo (Zaburi 55:22).


Kwa hivyo pumzikeni ndani YANGU, watoto WANGU, na msisahau faida ZANGU zote ambazo kila moja ni “ndiyo” na “amen” (Zaburi 68:19). MsiNIsahau, watoto WANGU. Selah.


Mwisho wa Neno

0 views

Recent Posts

See All
bottom of page