top of page

Unabii 42 “Ufalme Mmoja Utasimama!”

Updated: Mar 24


Umepewa Nabii Shema’YAH kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 17 Juni, 2019


Ujumbe wa Kinabii


NIamini mwanaNGU, unaNIsikia NIkinena. Kuna uasi katika barabara za Yerusalemu. NImechoshwa na haya. Mara ya kwanza ilikuwa ni Yerusalemu ya kiroho na hukumu imekuja. Sasa na Yerusalemu ya kimwili, hukumu imekuja. Acheni kuzungumza uhalifu! Netanyahu! Jinsi umevunja moyo WANGU. Watoto WANGU wanakulilia, kwa kile sasa Naenda kufanya. Hamwezi ishi maisha ya uvunjaji sheria bila matokeo.


Watu WANGU, mmeenda wapi? Mmeenda wapi? Kimo kipi cha chini lazima muende kabla mNIrudie? Kunaenda kuwa na damu katika barabara kwa yote ambayo mmeNIfanyia. Kwa maana NIlitembea [katika] hizo barabara na Damu YANGU iliwafunika kwa muda mrefu sana. Lakini tena hamwezi endelea kukanyagia [chini] Damu YANGU. Ghadhabu YANGU inakuja! Ghadhabu YANGU inakuja! Ghadhabu YANGU inakuja! Wizara ya Haki (kwa dhihaka). Huu ni mwigo bezo. Mwigo bezo kweli. Kwa maana hakuna haki katika nchi [kukiwa] na uavyaji mimba. Mnaua watoto wenu wachanga!


Mnahisi moto WANGU, kwa hivyo uwachilieni. Mnaua watoto WANGU wachanga! Na hili halitasimama. Mnatolea Moloki dhabihu na mnajua vyema zaidi. Mnajua vyema zaidi. Lakini mnapokea uhalifu wa hii dunia. Kwa muda gani mtatamani kuwa kama mataifa wakati NImewapa Sheria nzuri. Wakati NIliwapa Sheria Takatifu kuonyesha hekima yenu kwa mataifa; kuwa mwangaza kwa wale walio gizani. Mmejazwa na giza. Barabara zenu zimejazwa na giza. Ni vipi yeyote kwenu anaweza ona pale mguu wake ufuatao utaenda?


Nazungumza nanyi Israeli! Nazungumza nanyi Israeli! Na hili halitakaa [halitadumu]. Huu msimu utakuwa wa taabu sana kwenu kwa yote mmeNIfanyia. Wakati NImewabeba juu katika mbawa ZANGU. NImewapenda, na jinsi mmeNItelekeza... Na hamjafanya mambo yaliyo sawa ingawa NImewaambia katika Sheria ZANGU, Sheria za Torah YANGU ambazo zinaonyesha njia za ukweli. Lakini sasa mmepofushwa. Dhambi yenu ni mvundo kwa Mbingu yote na kwa dunia! Mnafikiri hawawezi kuwanusa? Watoto WANGU kote duniani wanashika pua lao.


NInawaweka katika jela vile maadui wenu watawazingira. Watawaingilia. Ondoa uhuru wenu ambao NImewapa. Maana hii ni hukumu YANGU juu ya nyinyi nyote ambao mmeNItelekeza. Mkristo na Myahudi. Kwa maana mpingakristo anakuja na kambi za mateso. Na nyinyi nyote ambao mmeNItelekeza mtaiangukia. Hili litawatendekea. MtakapoNIlilia, SItawajibu. SItapatikana popote kama vile tu NIliwapata (YAH Asema watu hawakuwa wanaMtafuta wakati Anasema hawapatikani popote). Kwa maana NIliwaita barabarani na ni wangapi mlijibu, mliitikia huo mwito? MIMI ni MUNGU MTAKATIFU AnaYEdai Utakatifu. Haswa katika Ardhi YANGU!


Hiyo ni Ardhi YANGU! NIlifanya agano na Abrahamu kuwapa. Hiyo ni Ardhi YANGU. Kwa hivyo sasa Nawaletea maovu vile mmeNIletea maovu na kuyatoa dhabihu KWANGU: watoto WANGU wachanga waliuawa. Msiba ulioje! Msiba, msiba umefanyika! Msiba umefanyika miongoni mwa watu WANGU, ambao ni nuru na wanajua njia ya ukweli, bado walidhihaki Sheria ZANGU! Na kwa ajili gani? Hamkuweza isimamia (Sheria)!


Nyinyi ni wakaidi! Waasi! Hiyo ndiyo maana mjeledi unawakujia. Katika upendo WANGU, m[ta]kuwa na fursa moja katika wakati huo kuanguka kwa magoti yenu na kutubu dhambi yenu. Lakini, ni nini mtafanya? Bali kutesa Manabii WANGU, Mitume WANGU; bali kuua Wayahudi WANGU wawili: Mashahidi WANGU Wawili. Lakini NItaruhusu hili ili kuwaonyesha, hata katika hilo [ni] rehema kwenu. Mkiwatazama na kuwaona wakiinuka tena baada ya siku tatu mbele ya macho yenu. Itaonyeshwa kwenye televisheni dunia nzima. Na katika hiyo siku, ni heri mlie.


Kwa maana msipo[lia], hakuna lolote lililowabakia. Mtetemeko wa ardhi unawangoja! Msiba wa dunia nzima! NIkiwatupia mawe ZANGU! Na kumwaga ghadhabu YANGU. Umalizaji wa hiyo yote na NIrahisishwe mizigo YANGU ambayo NImetwishwa nanyi. Siku nenda, siku rudi. Bila mwisho, dhambi zenu zimerundika hadi Mbinguni. Hiyo ndiyo maana NInawaadhibu. Haitakuwa bila uchungu. Haitakuwa bila uchungu. Itakuwa uchungu sana kwenu katika siku hiyo. Itakuwa uchungu sana kwenu Watu WANGU, kwa ajili ya uchungu ambao mmesababisha. Vile mara kwa mara mnapuuza Sheria ZANGU. Lakini Ufalme WANGU utakuja! Ufalme WANGU utakuja.


Mara tu NImemalizana nanyi, kutakuwa na Maisha bila Mwisho. Maana wakati miguu YANGU itagonga Mlima wa Mizeituni, [i]tatokeza maisha. Kwa maana MWANA MFALME wa Maisha, MFALME wa Maisha Amekuja chini kwenu. Muda mfupi tu baada ya NImejituliza kutokana na maadui WANGU (Isaya 1:24)! Na NItawaonyesha jinsi NInavyopigana na mngetamani... Oh mtaomboleza! Mtakuwa mmetamani mlikuwa mmeamini, mlikuwa mmebaki waaminifu, wakati MFALME WANGU Anakuja kwa hìi dunia. Na ANIamrishie hukumu. NItawahimiza hii mara moja ya mwisho kugeuka kutoka kwa dhambi yenu. Kutubu! Tubuni! Kutubu!


Naphtali Bennett alikuwa kwa kweli mtu mzuri. Alijaribu kadri ya uwezo wake na kile ilimbidi afanyie kazi. Aliondolewa kwa ofisi na mipango ya mlango wa nyuma. Jambo aina hii hufanyika kila wakati Israeli, katika hii dunia. Haishangazi, kwa maana wale watakao simamia ukweli, daima itawabidi wagongane dhidi ya uongo. Na kwa kweli ni vita. Vita vikali.


Kwa hivyo chagueni pande zenu. Maana Ufalme mmoja utasimama. Na unainuliwa juu na Mkono WANGU wa Kulia. Na NItautuma kuwaponda! Kazi zote za mikono yenu. Na kutakuwa na kufanywa upya katika nchi na dunia NInapochukua tena kile shetani ameiba. Na hiyo itakuwa kazi rahisi NItakapodunga mawingu na kuenda kupigana vita [dhidi] ya maadui WANGU na NItawamaliza mara moja. NIkipigana dhidi yao na upanga wa mdomo WANGU na kuwaangamiza na ung'avu wa kukuja KWANGU.


Katika wakati huo, mtalilia mawe yawaangukie, yawafiche. Lakini hakuna funiko kwenu. Kwa maana mlilipuuza zamani. Na kuna tu makazi moja kwenu na hayo ni Jahanam chini. Woga na kutetemeka kutawararua maana mtaona ndani ya macho YANGU moto uwakao. Nchi YANGU itasafishwa uovu wote. Kamwe kutowahi tena najisiwa na wasiotahiriwa moyo! Sikio! [Mwili!] (Ezekieli 44:7-9).


Na moyo WANGU utarudi hapo – [ku]ongoza na kutawala kutoka Yerusalemu kwa miaka Elfu moja. Na wakati huo utakuwa Jubilii! Na watumwa wote, wataachiliwa huru! Watumwa wa akili, watumwa kimwili. Na mataifa yote yatakuja KWANGU!


MIMI, YESHUA, Nazungumza toka kwa mwanaNGU. Hayo yote yatakuja na yatakuwa, na Naja upesi kusahihisha makosa ya hii dunia (Anamaanisha kwamba kila kitu [YESHUA] Amenena kitatimia). Na itakuwa, kwa sababu SIwezi stahimili uongo wa mwanadamu. Ule usaliti. Ule uavyaji mimba. Kule kutesa Watoto WANGU. WataNIita NIrudi (Watoto wa YAH wanaMwita chini). WataNIita nyumbani (Yerusalemu). WanapoNIlilia, “YESHUA, Utakuja lini?” Mahubu WANGU, NIko njiani hata sasa! Na pia, mnahusika kwa sehemu katika hilo [ya kule kuja kwa YESHUA]. Kwa maana mnapaswa kuwa katika gauni jeupe limetametalo.


Kwa hivyo NItazameni NIkisafisha nyumba na litakuwa jambo la kuogofya. Kwa ajili ya vile vitu lazima NIruhusu vikuje juu ya Watu Wangu, Nchi YANGU. Kwa maana wanatuma laana kwenu, maadui wenu wanaowazingira. Na kiasi cha dhambi zenu... Kwa ajili yake [hicho kiasi cha dhambi] lazima NIwaruhusu waje. Katika utumwa mtaenda, kwa maana hili mnajua. Kwa maana hii ndiyo laana ya Sheria. NInaweka nira YANGU juu yenu sasa. Nira ya Utakatifu. Na wale ambao hawatajisawazisha, watachomwa, watateketezwa.


Na usiku huu, NInavua Taji LANGU na NInaenda kwa vita. NInakata mti uliokauka na kuung'oa kwa mizizi. Na yale matunda mazuri yatagonga ardhi. Na wao NItsanya, na wengine wote watachomwa (Yale matunda mazuri yalioanguka toka mti uliokauka yatasanywa). Maana NImewangojea vya kutosha mrudi. Na mnajua Utakatifu WANGU. Hivi vitu mnavyoruhusu, haviwezi simama. Siwezi ruhusu hili kuendeleakuwepo. Kwa hivyo, usiku utaingia na kuwateketeza ninyi nyote.


Njooni upesi kwenye kimbilio lenu la pekee chini ya mbawa ZANGU! Njooni upesi! Kuna njia moja tu. Ni YEHOVAH pekee Aokoae! Iteni juu ya JINA la MWANANGU, YESHUA. Fanyeni haraka!


Maana usiku huu, NInaanza kuhesabu kurudi nyuma [muda uliosalia], kulikuwa na kuhesabu kurudi nyuma kwingine. Kulikuwa na kuhesabu kurudi nyuma kwingine ambako kuko karibu zaidi na wakati wa Taabu ya Yakobo. Na utakuja upesi juu yenu. Giza NInalotabiria litakuja haraka juu yenu; kama mwizi usikuni. NIlikuambia Israeli kwamba usiku utaanguka. NIlikuambia kabla ya wote. Kwa maana imeandikwa katika Maandiko yako – katika Yoeli. Mara ngapi umesoma Yoeli? Kwa maana unajua “Siku ya BWANA” imekuja. Jambo la kuogofya; kupiga mayowe. Itakuwa kama mwanamke katika uchungu wa kuzaa, kuzaa MWANA wa Mtu [Adamu] kwenye barabara zenu, kwenye ardhi yenu.


Kwa maana mnajua – maana NIlikuja kwenu MIMI MWENYEWE na NIkawaambia Natuma waandishi na wale ambao ni wasomi katika Torah! Na mnawapiga na kuwarusha mawe. Na jinsi Navyotamani, kama mama, kuwakusanya chini ya mbawa ZANGU. Na hamtaNIona tena hadi mseme, “Mbarikiwa ni YEYE AnaYEkuja katika JINA la YEHOVAH!”


Kwa hivyo Watoto WANGU, NIsikieni sasa. Wale ambao kwa kweli mnaMjua NDIMI NILIYE MKUU. Jificheni kwa muda kidogo, ghadhabu YANGU ikipita. Na ni heri mshike Pasaka, kwa maana wakati huu NInaamrisha Utakatifu kuliko wakati mwingine asilani. Kwa maana hata nyinyi pia mnahitaji kujirekebisha! Na muelewe utiifu ni kubwa kuliko dhabihu. Maana ni ule wakati, ambao hata Noa, Danieli na Ayubu wangesimama mbele YANGU, SItasikia maombi yao kwa hawa watu. Na kila mmoja kwa chake, mtu atahifadhi maisha yake mwenyewe kwa jinsi wanavyoNItii MIMI (Ezek. 14:12-21).


Kwa maana hakuna makosa zaidi tena. Hakuna tena visingizio! Na yale maarifa NImemwaga juu yenu – wapi raghba? Wapi mapenzi makali? Katika Mwili WANGU! Wale wanaodai kuwa WANGU! Kiwango cha juu zaidi, kiwango cha juu zaidi kimekuja juu yenu. Maana wakati huu, NInapima nyumba YANGU! NInaangusha Fimbo, huku NIkiangusha timazi. Ni kwa unyoofu gani unapimika (Amosi 7:7-9)? Kwa ukuu gani unaogopa MUNGU? NItawaambia hili, inaenda kuwa jambo la kuogofya ikiwa huNIsikii kwa dhahiri! Ikiwa hutembei Nami, ukiNItii kwa uaminifu – kwa imani na sio kwa kuona ( 2 Wakorintho 5:7). Linaenda kuwa jambo la kutisha, litagonga moyo wako unapogundua, ‘Oh, Yesu, sikuwahi kwa kweli kujua! Oh, Yeshua, sikuwahi kwa kweli kujua!’ Lakini mkate wako utakula kwa kipimo. Kwa maana hii ndiyo hukumu ambayo imekuja juu yako.


Oh watu WANGU, mnajua kinachotendeka sasa? Lazima NIfiche macho YANGU kwenu. Lazima NIfiche macho YANGU kutoka kwenu NIkilia na kutaabika [kwa] kile lazima NIfanye, kile lazima NIruhusu, yale yatatoka kwenye mashimo [ya Jahanam] – kuja juu kwenye ardhi (Yeremia 13:17, Isaya 1:15). Kwa maana NInatuma nzige miongoni mwenu. Na watakula bohari zenu. Na mtatafuta huo mkate, huo mkate, huo MKATE wa Uhai. Lakini ni wangapi, na MIMI, watapatikana? (ni wangapi watapata YESHUA? Kutakuwa na na ukame wa Neno LAKE.)


Mwisho wa Neno

9 views

Recent Posts

See All

Comments


Commenting has been turned off.
bottom of page