top of page

Unabii 56 Sikia O Israeli, Wakati wa Taabu za Yakobo u Mlangoni Pako!


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 21 Juni, 2019


Ujumbe wa Kinabii

Kuponda NItaponda. Kwa maana nyundo itaanguka, imeanguka juu ya hiki kipindi cha dunia. Kwa maana ikiwa hautanguka juu ya MASIA na uvunjike na uwe mnyenyekevu, basi kuwa tayari kupondwa wakati Jiwe Linaloishi linaanguka chini! [Wakati] linakuja chini kuimarisha kuwa jiwe kuu la pembeni, Ufalme wa milele kwa maana hiyo sanamu itaanguka! Kichwa kitakatwa.


Ufalme wa hiki kipindi utakuwa UFALME wa MUNGU wetu! MIMI YEHOVAH Nasema hivyo. Na lolote lile NInaloamuru, hilo litakuwa. Sio katika wakati wako, o mwanadamu! Lakini katika wakati WANGU! Asema MIMI YEHOVAH MUNGU wa milele. Kwa hivyo lainikeni binadamu. Bonde la maamuzi. Wengi wamo ndani wanaishi katika uwazi na wakati. Je unapoteza wakati WANGU?!


Chagueni siku hii ni MUNGU yupi mtakayetumikia! Kwa maana milele inawakodolea macho usoni. Kila mmoja wenu ana mahali katika umilele WANGU. Je, ni katika Jahanam au ni pamoja NAMI, kando YANGU? Chagueni kwa hekima! Chagueni haraka. Leo ndiyo siku ya wokovu. Nani aliwahakikishia kesho?


Oh Israeli nani aliwaahidia kesho!? Jitayarisheni kutikiswa. Kwa maana NItawatikisa na mtikiso NIkikanyaga-kanyaga na miguu YANGU kwa vishindo na kufanya nyufa katika misingi ya kile mnachofikiri ni kweli! Lakini mmejenga kwenye mchanga wa wakati. Mchanga wa wakati wenu. Tamaduni za wanadamu. Kwa maana mnapuuza mambo mazito zaidi ya haki, huruma na ukweli na neema, mkichambua mambo madogo madogo ya sadaka za jira na nafaka.


Lakini wapi huruma yenu!? Kwa maana mligeuza jicho pofu kwa wale maskini ambao wanaishi barabarani mwenu na SIzungumzii tu wale ambao wanavaa matambara kimwili! Nazungumzia kuhusu kondoo na wanakondoo WANGU wenye njaa! Enyi marabii waovu mnaostahili twezo, Nawakujia! NItawauzulu! NItawavua nguo, NItawanyang'anya hiyo kashida!


Kwa maana mna mfumo wa utawa, lakini wapi maombi ya kweli, usemi wa kutoka ndani?! Marudio, maombi bure, machukizo! Kuchanti! Kuchanti lakini hakutoki moyoni! Maneno ya kurudia tu! Kurudia tu Maandiko YANGU! HaiNIpendezi, haiNIvutii kwa maana NInaangalia moyo.


Maana mnanena maneno ya kuinua lakini moyo wenu uko mbali NAMI, oh Israeli. Sio wote, kwa maana NIna waliobakia, NInaye Bi-Arusi, Bi-Arusi mwenye usingizi. Lakini Natumia ‘Torah Keeper' (Mshika Torah) YANGU kumtikisa aamke katika roho. Anaamka. Na sasa Nangoja tu tovuti iwekwe na NItatumia hii tovuti. Ni upanga wenye ncha mbili kuua, kukata maadui WANGU katika kila njia. Kwa hivyo simameni nyuma watoto WANGU na mtazame BABA wenu Akifanya kazi.


Ndiyo, lazima mtende matendo, lakini NItazameni, kwa maana MIMI ni mfano wenu, ELOHIM wa milele. Tendeni matendo YANGU lakini sio matendo yenu. Maana mtakuwa mnapoteza wakati, lakini mnapofanya kila kitu katika wakati WANGU, hili linaNIpendeza.


Bi-Arusi anajitayarisha na mafuta tayari! Utambi umepunguzwa, unawaka kwa ung’avu, hata kama vile kichaka kinachochomeka katika jangwa. NIruhusuni NIzungumze kuwapitia nyinyi watoto WANGU. NIruhusuni NIwawashe moto na moto WANGU. Hamtateketezwa. Hamtaangamizwa bali mtakuwa kama mfano KWANGU.


Kwa maana kile kichaka kinachochomeka ambacho Musa aliona kilikuwa ni ishara, watoto WANGU. Ya MIMI YESHUA kulazimika kukaa siku 40 katika jangwa NIkiwaka kwa ung’avu lakini bila kuteketezwa. Kwa hivyo Nazungumza nanyi Israeli, kwa sababu Nawapenda. Jitayarisheni, kuweni tayari, kwa sababu wakati wa Taabu ya Yakobo uko karibu sana kwenye shingo zenu. Mpingakristo atainuka na kuwaroga kwa wale wote ambao hawajajitayarisha. Wakati ulioje wa simanzi, wa taabu, wa kulia, huzuni, wa maombolezo. Someni Kitabu cha Maombolezo, oh Israeli. Jitayarishe. Jitayarishe. Ita tu juu ya JINA la YESHUA katika hiyo saa ya giza kabisa. Na Atakuwa hapo kukuokoa, kukusaidia, kukuopoa. Tumainia katika Zaburi 91. Kuwa kama yule mfalme Daudi na ufurahie katika uwepo WANGU. Hapo kuna ushindi.


Wengi wenu sana mnazungumzia kuhusu mababu, lakini ni wangapi mnaofuata mifano yao? Kwa maana inaburudisha kuzungumza kuwahusu, lakini tena ni wangapi mnaofuata katika nyayo zao? Wanafuata katika nyayo za MASIA. Vivyo hivyo mtafanya, Israeli. Tubu! Ufalme wa Mbinguni u karibu!


Nyundo itaanguka. NItavunja vidonge katika vipande. NItatakasa watu WANGU. NItahukumu na nyundo ya hakimu. Naam, NItavaa nguo za Mfalme mkuu. Mtaona, mtaNIpa Utukufu mkitazama juu ya YULE ambaYE mmedunga.


Katika kuomboleza mtaomboleza, mkiNIona katika Utukufu WANGU wote, NIkiweka miguu YANGU kwenye Mlima wa Mizeituni. NIkiupasua mbalimbali kuelekea kulia, kuelekea kushoto.


Kwa hivyo kuweni tayari, ee Israeli. Kwa kuja KWANGU, Ajaye kama mwizi usiku. NIiteni tu, O Israeli, katika saa yako ya giza kabisa. NItakuokoa kutoka kwa mpingakristo. Lakini utajifunza mafundisho magumu na ya thamani njiani, ili mwishowe sasa utainamisha goti, utainama mbele YANGU. Njia ngumu na ya kuogofya itabidi usafiri hadi huo wakati na kujua utajua kwamba ni MIMI na Naja kuwakomboa.


Inamisheni tu na muegemeze sikio lenu kwa kila neno ambalo Nasema, watoto WANGU, hamtawahi enda kombo. Bakini tu wanyenyekevu, bakini takaso. Ruhusu neema YANGU, rehema YANGU kutiririka kuwapitia. Kwa kufanya hili litaonyesha kwamba mnaNIpenda.


Kwa maana neema na rehema nyingi NIlimwaga wakati NIlikuwa kwenye hii Dunia, wakatiNIliwaruhusu kuNItusi, kuNIdhihaki. Kwa Mafarisayo kuinuka na kuNIpiga na kuNIuma. Nyoka, vipiribao! Kwa ajili yako NIliteseka, kwa ajili yako NIlikufa, kwa ajili yako NIlifufuka. Kwa ajiliyenu Narudi. Endeleeni tu kusoma maagizo YANGU ya Torah. Kwa maana mtakuwaje Washika Torah ikiwa hamjui kile kimeandikwa katika Kitabu Kizuri?


Bakini katika furaha, bakini takaso, bakini kali katika raghba ya MUNGU ALIYE HAI YEHOVAH, sio raghba ya muda lakini raghba ya milele! Raghba NInayowavisha. Sasa nendeni mbele watoto WANGU.


Kuna samaki wengi wa kusanya. Tupeni wavu wenu katika maji ya kimo. Na msihangaike, kwa maana NItawahimili hata katika saa yenu ya giza kabisa. Kwa maana MIMI ni nuru yenu iongozayo! Kamwe SIpunguki mwanga, kamwe SIchoki, SIlali au kusinzia. Msiende tu kwa ufahamu wenu, maana ufahamu wenu ni nyayo zenu wenyewe na NIlionya kuhusu njia zinazoonekana kuwa sawa kwa mwanadamu na pale mwisho ni kifo chake. Malipo ya dhambi ni kifo. Lakini Nawapanda katika ardhi nzuri. Pale ambapo kuna nafasi pana ya kustawi, kukua.

NIruhusu kuongoza hatua zenu kwa maana hatua ZANGU ni hakika na imara, zikiongoza kwa ushindi.


Maisha yenu si yenu wenyewe. Kumbukeni hilo, hilo ni muhimu. Ufunguo wa Daudi. Nyinyi nyote ni kanisa la Filadelfia. Endeleeni tu kukua thabiti kama huo mti wa msonobari. Wale 5 wenye hekima, wakinyua maji YANGU Yaliyo Hai kwa kimo, hawasikilizi mgeni yeyote, si sauti ya yule aliyeajiriwa.


Kwa hivyo, sikia , O Israel, siku hii, na kuweni kwa amani watoto WANGU, kuweni kwa amani, pumzikeni ndani YANGU kimawazo, kimwili, kihisia, kiroho, kifedha na kila njia mwaweza fikiria; pumzikeni ndani YANGU. Kuweni dhabihu zilizo hai kwa sifa, heshima na utukufu WANGU.


Mwisho wa Neno

7 views

Recent Posts

See All
bottom of page