top of page

Unabii 46 “YEHOVAH Asema, “Wapi Nuru Yenu, Ee Israeli?”

Updated: Mar 24

Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa Juni 22-24, 2019


Maandiko Husika

Isaya 55:6-7 “Mtafuteni YEHOVAH wakati bado Anapatikana, mwombeni msaada wakati YUPO bado karibu. Muovu na aache njia zake mbaya, mtu mbaya aachane na mawazo yake mabaya; amrudie YEHOVAH Apate kumhurumia, amwendee MUNGU wetu maana atasamehe kabisa.”

Hosea 6:1-3 “Njooni, tuMrudie YEHOVAH; maana YEYE Amerarua, na YEYE Atatuponya; YEYE Amepiga, na YEYE Atatufunga majeraha yetu. Baada ya siku mbili Atatufufua; siku ya tatu Atatuinua, nasi tutaishi mbele ZAKE. Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua YEHOVAH; kutokea KWAKE ni yakini kama asubuhi; naYE Atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi. “


Ujumbe wa Kinabii

Nazungumza katika fumbo, Nazungumza katika ajabu. SIneni kufurahisha sikio, lakini kuwasilisha Ukweli, kwa maana MIMI ndiYE UKWELI, MUNGU wa Milele, MWENYEZI MUNGU! Na hakuna (aliye)kama MIMI!


Ee dunia, kuweni tayari! Kwa maana karibuni NItamwaga Ghadhabu, Kiruu CHANGU, na Hasira YANGU katika njia hamfikirii. Ndiyo, vimondo vitakuja, dunia itafanywa giza wakati jua na mwezi itaomboleza kwa ajili ya jinai ya hunde na kuogofya ya binadamu dhidi ya MUNGU (Mathayo 13:24-26). MIMI, hata MIMI, MWENYEZI MUNGU MKUU, MIMI ELOHIM wenu na bado mnaNItupa kama kipande cha takataka kinachotupwa nje ya dirisha la gari.


Ee dunia, karibuni mtaona Sheria ZANGU, Torah YANGU, Ukweli WANGU havifai kuachwa. Kwa maana ndani yenu tayari yafanyika fumbo la uovu. Tayari mshachukua chambo. Kile kinafanyika ndani yenu ni laana ya kuogofya, kwa maana njia inayoonekana sawa kwa mwanadamu yaelekeza tu hadi mauti, ikiwa chukizo machoni PANGU (Mithali 14:12).


Msishikike katika chaka la dhambi na uabudu sanamu la hii dunia. Ee Watoto WANGU, tokeni miongoni mwake na msichukuliwe katika mtego. Msipinduliwe na majarabio ya zama hii, huu wakati wenye giza na wa sasa. MIMI ni YEHOVAH MUNGU MWENYEZI, NIkiahidi kutowahi kamwe kuwaacha au kuwatelekeza (Waebrania 13:5). Kwa hivyo, watoto WANGU, msiwe na wasiwasi kwa kile mnaona kikija toka kwenye anga au dunia chini. Jueni tu majina yenu yamenakshiwa kwenye viganja vya mikono YANGU (Isaya 49:16).


Ee Israeli, mbona mmefuata katika nyayo za hii dunia? Je, hamjui kwamba kujiunganisha na hii dunia inahuzunisha machoni MWANGU?! Wapi Torah, Maagizo YANGU ya Milele? Mnakusanyika kila Shabbat, lakini mnapeleka dunia moja kwa moja hadi katika masinagogi. Ee Israeli, hili linaNIsikitisha! Mlistahili kuwa nuru kwa mataifa, kwa watu wa Mataifa (Isaya 49:6). Lakini mnajifurisha dhidi yao, mkijifikiri bora kuwaliko. Lakini katika kweli Nawaambia, nyinyi sio [bora], kwa maana wote wamehitimishwa chini ya dhambi. Hakuna aliyeadilifu (Zaburi 14:1). La, hakuna mmoja bila MWANANGU YESHUA HAMASHIACH.


Mlistahili kuwa wabebaji-nuru WANGU, lakini mwawezaje kubeba nuru bila NURU YANGU IONGOZAO Ikiwaongoza? Mwawezaje kuwa nuru ikiwa mmejawa na giza? Hamwezi tumikia mabwana wawili, kwa maana aidha mtapenda mmoja au mchukie mwengine au mchukie mmoja na mmpende mwengine.


Mnabeba Torah YANGU katika sinagogi zenu, lakini inashuhudia dhidi yenu, ee Israeli. Huu wimbo wa Moshe unashuhudia dhidi yenu (Kumbukumbu 31:19-22). Ole iwe kwenu, ee Israeli! Ole iwe kwenu, kwa maana Moshe atarudi tena lakini bila huruma, [na] hukumu YANGU tu (Yohana 5:45)! Waasi! Nyinyi nyote! NItasafisha kutoka kwenye nchi, kwa maana lazima iwe Takatifu. Nchi inaNIlilia isafishwe. Mawe, ndege, wanyama, wote wanaNIlilia. Je MIMI si MUNGU wa huruma? Kwa hivyo NItajibu uumbaji WANGU na kuchukua kisasi.


Lo, inaNIsikitisha, mwanaNGU. InaNIsikitisha. Jinsi NInavyoangalia Israeli, Yuda, kwa mji mara moja uliitwa Takatifu. Ee Yerusalemu, umeenda wapi? Nawaita kutoka Mbingu ya Milele. Kupitia fumbo la wakati, Nawapungia mkono mje KWANGU nyinyi nyote ambao mmechoka na mmelemewa na mizigo ya dhambi za zama hii (Mathayo 11:28-30). Ule mzigo mnabeba ni jiwe, uzito wa maovu yenu ya ujana, kwa maana bado hamjatakaswa kutokana na hatia ya uchanga. Ya uzee wenu, kwa maana mmekua wa zamani – kuwa ngumu na kuimarika katika njia zenu. Na Nasema “njia zenu" kwa sababu hizo sio Njia ZANGU. Tamaduni za wanadamu zinawakaba roho, zinawakwamisha.


Wanawawekea vinga vya macho. NItafuteni wakati bado Naweza patikana (Isaya 55:6-7). Geukeni nyuma kabla kuchelewe kabisa, ee Israeli. Geukeni nyuma! Mpatikane naMI, MIMI YESHUA. Msitafute burudani za hiki kipindi. Hiki kipindi kinapita na wale Watakatifu tu, wale waadilifu tu – wale ambao wamefanywa hivyo na imani – watasimama, watavumilia hadi mwisho. Mpatikane naMI, BWANA wenu, kabla kuchelewe kabisa.


Chagueni hii siku ni MUNGU yupi mtatumikia. Chagueni ni Torah ipi, ni agizo lipi mtafuata. Je mtafuata neno la uovu ambalo huelekea tu kwa mauti? Au je mtachukua Torah YANGU? Je mtaruhusu JIWE LANGU KUU LA MSINGI kwa kweli Lilazwe kama msingi wa maisha yenu (Luka 20:17-18)?


Ee Israeli, mmefanya nini? Mbali naMI mmeenda. Mbali sana mmepotoka na kugeuka kando naMI, MIMI, YEHOVAH. Kwa hivyo, NItawavunja, ee Israeli! Lazima NIwavunje kwa wema wenu, ee Israeli! MIMI, YESHUA, lazima NIvunjevunje ardhi yenu iliyolimwa na kuwachwa bila kupanda mbegu (Hosea 10:12). Lazima NIpure kwenye uga wa kupuria. Lazima NIkanyagekanyage mizabibu katika Shinikizo la ukali wa MUNGU MWENYEZI (Ufunuo 19:15). Lazima! Lazima! Lazima! Lazima NIfanye kile MIMI, YESHUA, BWANA na MWOKOZI, MCHUNGAJI wenu, lazima Afanye.


Chukueni hatua, ee Israeli! Kuweni wenye kujishughulisha mapema! Waondoeni mafarisayo waovu, marabii waovu ambao wanakufuru Maandiko YANGU kutoka kwenye sinagogi, kutoka kwenye nchi. Haya majitu ya uovu hayafai kuogopwa! Wananukuu Neno LANGU, Torah YANGU na kuNIacha nje. Wanasema ni kwa mwingine ambaye Maandiko ya Kimesaniki yanahusika na sio KWANGU MIMI. Lakini mtajifunza lini, ee Israeli, kwamba MIMI NDIMI NILIYE na hakuna mwengine ila MIMI?


MIMI, YEHOVAH, MUNGU wenu, ELOHIM wenu, Nashuhudia dhidi yenu na kusema: NImetuma MASIA wenu kwenu na JINA LAKE ni “YESHUA HAMASHIACH.” Msiamini kile Wagiriki wanasema kuMhusu. YEYE si masia wa kipagani Akisimamia juu yasikukuu za kipagani, zilizowekwa na wanadamu na tamaduni kutoka shimo la Jahanam.


MASIA wenu ni Mwebrania, MFLAME wa Wayahudi, kazaliwa toka kwa Mjakazi Bikira Mwebrania. Alitembea (MASIA) mchanga wa Israeli, Akitangaza mbali na upana Ujumbe wa Wokovu, Injili ya Habari Njema. Alinukuu Torah, kwa maana kwani YEYE siYE TORAH ILIYO HAI? Mnafikiri madhumuni ya Torah ni nini? Ndiyo, kuwaonyesha kile NInachotarajia toka kwenu lakini pia ni mwongozo wa jinsi ya kufahamu MASIA wa KWELI. Mnatafuta katika Maandiko ili mpate Wokovu, mkifikiri kwamba ndani yake mnao uhai wa milele (Yohana 5:39-40). Lakini MIMI, YESHUA, Nawaambia Ukweli, ee Israeli. Yanashuhudia kuNIhusu MIMI, lakini hamko radhi kuja KWANGU kwa wakati huu. Wakati tu mtatembea njia ya uangamizaji, wakati mtapoteza vitu vyote ndipo mtakapokuja KWANGU. Wakati huo tu ndio mtakapolia, “Barukh haba B’SHEM YESHUA HAMASHIACH!” [ברוך הבא בשם ישוע המשיח] (Wale Mashahidi Wawili watakuja katika JINA LAKE- watapeana ushahidi kwa Ushuhuda wa YESHUA)


Ni wakati huo tu mtaNIpokea katika ROHO na katika UKWELI. MIMI NDIMI Njia, Ukweli na Uhai (Yohana 14:6). Mnasema mnaYE BABA, lakini mwawezaje ikiwa mnakana MWANA wa NDIMI NILIYE MKUU? MIMI na BABA tu MMOJA, ee Israeli (Yohana 10:30)! Kukana mmoja ni kukana YULE mwengine. Tubu, ee Israeli, kwa maana huu ni upumbavu! Kukana MJUMBE na Ujumbe Auletao ni kukana YULE AliMtuma na Ufalme Anaouwakilisha (Mathayo 10:40).


Hii ndiyo maana yatakuja tukia kwamba mtaona Abrahamu, Isaka, na Yakobo na manabii wote katika Ufalme wa ELOHIM na nyinyi wenyewe mmetupwa nje, sukumwa nje (Luka 13:28). Ee, lakini NInao waliobaki aminifu na kweli! NInaye Bi-Arusi ambaye hatajinajisi na tamaduni za wanadamu na mafunzo ya mapepo. Wanaamini MIMI ni NANI na NDIMI NILIYE Anapendezwa nao kabisa!


Ee, Bi-Arusi wa YESHUA katika Israeli, njooni! Njooni KWANGU nyinyi nyote ambao mmelemewa na mizigo na wagonjwa, wagonjwa [waliolazwa] kitandani na dhambi na hatia ya hii zama! NIruhusu MIMI, YESHUA, kuwasafisha makosa na dhambi zenu. NIruhusu NIwasamehe. Chukueni Mkono WANGU wa Rehema na Mkono WANGU wa Neema. NIlidungwa kwa ajili yenu. NItazame MIMI na msiogope. Kwa nini muogope kivuli chenu wenyewe?


Ee Israeli, MIMI, YEHOVAH, Nakumbusha Nyumba YANGU nidhamu. Lainikeni! Ingieni kwenye safu! Tupeni miungu yenu na muondoe mbali nanyi, nyinyi nyote, kiburi cha uzima na jicho ovu. SItembei katika dhambi na Nahitajisha kambi safi. Msiruhusu moto wa ALIYE JUU KABISA kuzuka miongoni mwenu na kuteketeza hadi viungani (Hesabu 11:1). Naita makabila yote kujieleza kutoka mkuu hadi wa chini kabisa. NIjibu MIMI na msimame katika gawo lenu. Msijaribu BWANA MUNGU wenu. Msifanye kile kisichofaa machoni pa ALIYE JUU KABISA. Kuweni wenye kustahiki. Kuweni wanyenyekevu. Msishawishike na shetani na njia zake za ugomvi, ee Israeli.


Ujumbe WANGU bado ni mmoja. Tubuni, ee Israeli, kwa maana Ufalme wa Mbinguni u karibu (Mathayo 4:17)! Tubuni na mbatizwe! Njooni chini kwenye Mto wa Maji Yaliyo Hai na mjazwe na uhai (Isaya 55:1)! NInayo mipango mingi sana mizuri kwenu, ee Israeli. NIruhusu NIwahuishe, NIwarejeshe kwenye njia za zamani (Hosea 6:1-3).


Mwisho wa Neno

9 views

Recent Posts

See All
bottom of page