top of page

Unabii 58 "Kuweni Wasio na Lawama Watoto WANGU: Shikeni Amri ZANGU na Muishi!”


Umepewa Nabii Shema’YAH kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 25 Juni, 2019

Ujumbe wa Kinabii

Wajinga! Hawa watu ni wajinga kivipi kuja dhidi YANGU? Baada ya yote NImefanya kulisha, kuongoza, kuelekeza na kuonyesha na Fimbo YANGU ya Mchungaji (Zaburi 23). Lakini katika kweli, NImehifadhi wale wote ambao wameNIpenda na kuangamiza wale wote wengine (Zaburi 145:20). Kwa maana ni dhahiri kwamba hawaNIpendi. Kuona uovu na kusimamia udhalimu katika uso wa ukweli WANGU! Kwa maanaimeandikwa katika Maandiko. Msingi wa KITI CHANGU cha Enzi kimeanzishwa na uadilifu na haki (Zaburi 89:14).


Na angalia udhalimu wa hawa watu wote kuua watoto WANGU! Xenia (mshirika wa Amightywind), umeanguka barabarani. Na nafsi yako imekuponyoka! Na nafsi ngapi zimepotezwa kwa sababu ya upumbavu?


Lakini yote yameandikwa katika Sheria YANGU. Kwa kukataliwa kwa Torah YANGU, laana kubwa imekuja juu ya wote (Walawi 26:14-46; 1 Sam 15:23). Kwa maana wakati hausimamii haki, unapofushwa na dhambi. Unapinduliwa kwa ndani. Na sio wengi wameponyoka (kutoka huduma ya Amightywind), na majina yao hamjui. Kwa wale ambao mnajua washauawa kwa ndani; wamepoteza maisha yao na nafsi zao. Na hili linaNIhuzunisha sana.


Shikeni Amri ZANGU na muishi (Mithali 7:2)! Hii ndiyo amri toka mwanzo, watoto WANGU wa kweli wote watakuwa wameponyoka hili. Kwa maana Neno LANGU halidanganyi. Unapotii, linarudi juu yako. Linatekeleza yale yote NIlilituma kufanya; bila kufeli. Na hilo ni sawa [pia] kwa wale wasiotii. Neno LANGU halidanganyi (Hesabu 23:19; 1 Sam. 15:29; Tit. 1:2; Waebrania 6:18)!


Kile mnacho hapa, ni mwanadamu anajaribu kujifanya MUNGU. Na umati wa waovu wakiifukuzia. Lakini kuna MUNGU mmoja, na SIpatikani katika [huduma ya] Amightywind na NItaiteketeza hadi chini! Na hukumu ZANGU nyofu na Mkono WANGU adilifu wa Kulia, NItaileta chini. Kulipiza kwenye nyuso, kuchukua kisasi juu ya wote ambao hawajaNIpenda! NItawaangamiza wote (Kumb. 7:9-10)! Na majeruhi wamekuwa wengi. Lakini walichagua kupuuza mwito WANGU. Kwa maana, Nawaambia hakuna mmoja ndani [ya huduma ya Amightywind] hakuonywa! Badala ya kuichukua na kuNIletea, walichagua kuamini uongo hizo.


Lakini huu ni mwanzo tu wa kazi ZANGU za haki za mwisho wa wakati- kufanya mfano mbele ya wote – kwa wale wanaodanganya. Ya uongo uliomo ndani (katika kisa hiki huduma ya Amightywind, lakini siri zote zilizosemwa katika siri zitafichuliwa; Luka 12:2). Hakuna uongo wowote katika huduma hii [hakuna uongo katika Huduma ya Torah Keeper (Mshika Torah)]. Na, karibu na mbali Naita watoto WANGU – wa kweli, wale wanaopenda ukweli – waje karibu. Waje KWANGU. Nawasanya nyote toka uso wa dunia! Kuepa mitego ya maadui katika kila taifa kote duniani.


Hukumu ZANGU zitasimama! Msiguse Kondoo WANGU na Wanakondoo WANGU! Kwa maana MIMI, MCHUNGAJI Mwema, Nachukua Fimbo YANGU na kuwapiga wote [watokomee] mbali (maadui/mbwa mwitu)! Mbwa mwitu wote, mbwa mwitu waliovalia nguo za kondoo. Na kazi YANGU itasimama, kwa sababu SIwezi feli. Wale walio kweli hawataanguka. Kwa maana ni katika mkono WANGU wote wanasimama na SItapoteza mmoja wa Kondoo WANGU na Wanakondoo WANGU. Haijalishi pale ulipo kwenye uso wa dunia. Haijalishi adui unayekabiliana naye. Haki YANGU bado inasimama. NItawalinda na kuwaokoa nyinyi Watu WANGU. Haijalishi njama na mipango ya adui wa nafsi yako (Ezek. 34:11-12; Zaburi 23:1-6).


Watoto WANGU, kuja KWANGU ni haraka na lazima mjitayarishe kwa sababu huu ulimwengu umekutana na mwisho wake. Na SItaruhusu tena vile vitu ambavyo vimefanyika katika ulimwengu kuendelea mbele. NInakomesha uovu NInapoinua kiwango. Na wanafanya vita. Na msiendelee mbali zaidi (waovu na uovu wao). Maana wamekuja kukutana na mauti yao! Jueni tu kwamba wale wote wanaowafukuzia, wamekutana na mauti yao. Maana ni mpango WANGU na NInawatumia, NInawatwaa kama shoka YANGU ya vita duniani kuwaua maadui WANGU (Yeremia 51:19-23), wale wanaosimama dhidi YANGU! NInatumia wanakondoo WANGU wadogo wasiojiweza. Wasio na hatia WANGU, wasio na lawama WANGU! Kwa maana hamna meno makali, na ni mbinu YANGU (YAH Azungumzia kuhusu Wanakondoo na Kondoo WAKE) kuwavuta ndani karibu. Kabla wajue, SIMBA wa Kabila la Yuda Ako tayari kuwameza/teketeza!


Kuweni wasio na lawama watoto WANGU! Na mNItazame NIkifanya kazi katika hii dunia, NInapotoa upanga WANGU dhidi ya maadui WANGU wote! Maadui wenu wote, mmoja baada ya mmoja wanaanguka. Ikianza na [huduma ya] Amightywind! Kutoka kwenye ukingo, wote walienda... wote wanaanguka (Luka 6:39; Mathayo 15:14). Wakifuata malkia wao, malkia wa kukana (MUNGU Amwita Elisabeth Elijah “malkia wa kukana"). [Amightywind] yasema ndani yake, “mimi ni mwadilifu!” Wanapangusa mdomo wao na kusema, “Sijafanya kosa lolote!” (Mithali 30:20). Kipofu akiongoza vipofu! Na si ajabu walianguka katika shimo kuu! Kwa maana laana ambayo imekuja juu ya Amightywind ni laana kuu! Na haitageuka nyuma! Maana NIliinua mkono WANGU katika hii siku, na NInatangaza “Nitawaangamiza wote!” Yeyote yule ambaye ameamini hizi uongo yuko katika hatari kubwa ya moto wa Jahanam! Ya kupoteza nafsi yako!


Na SItashindana na mwanadamu! Upumbavu! Huu ni upumbavu. Mbona nyinyi nyote mfanye hili? Mbona nyinyi nyote mfanye hili? Mnafanya nini? Wakati NIliwaambia mkimbie? Na mnapata nafsi zenu katika hali isiyoweza kurekebishika!


MIMI ni NDIMI NILIYE MKUU! Na mNIsikize, ee Dunia. Jahanam na She'ol imefungua mdomo wao kupokea kila mmoja wenu, wote wasioabudu hii Sheria adilifu (Isaya 5:14; Enok 60:6). Hii njia ya ukweli. Hiki kitu kizuri ambacho NImewapa: Sheria ZANGU za Torah! Na MWANANGU YESHUA!


Jueni sasa tu kwamba wengi wataanguka kwa sababu neema inaondolewa duniani. Ikiwa hawatakuja haraka, watakutana na vurugu kubwa! Kwa maana MFALME Anakuja! NItaua maadui WANGU! Hii ni Dunia YANGU! Hiki ni kibago CHANGU cha kuweka miguu! Na si chenu! Lakini NImesema, “wanyenyekevu watarithi dunia" (Math. 5:5). Haki YANGU bado inasimama. Na hakuna chochote cha kupotosha au kubadilisha hilo. Sio sasa, sio kamwe! Asilani! Asilani SItabadilika! Asilani SItabadilika! (Yakobo 1:17; Malachi 3:6)!


Ni wewe, ee Dunia, utaNIinamia! Kwa maana imeandikwa, “kila goti litainama Mbinguni na kwenye dunia, hata wale chini ndani mwa dunia,” hivyo viumbe vitambaavyo (Wafilipi 2:10-11; Isaya 45:23). Ni MIMI NItakayesimama na kuangamiza maadui WANGU. Na wale wanaobaki wataenda kwa utekwa. Kwa maana imetosha! Na macho YANGU ni Matakatifu sana kuangalia huo weusi, giza la dhambi; uovu. NImemalizana nanyi, Ee Dunia!


Kunao tu wakati wa rehema ikiwa mtaichukua. Kwa maana NInanyosha mikono YANGU, mikono YANGU. Na lazima mfukuzie rehema. Lazima mfanye amani NAMI (Isaya 27:4-5)! Maana hamna tena neema. Hakuna wakati wa neema! Kwa maana mmeNIweka jeraha kubwa. Na ilimalizika pale Msalabani wakati huyo mwanajeshi aliNIdunga kwenye upande, na bado mmeazimia kurudia pigo hilo (Yohana 13:24). Na NIlitaka tu mjue jinsi NInavyojali. Jinsi NIliwapenda! Na kupeana maisha YANGU kwa ajili yenu. Bado mnatema mate katika uso WANGU na kuuma mkono uliowalisha!


Kwa maana uadilifu WANGU umo duniani mwote. Na NImewapa wote kwa wingi. Na Siwezi vumilia kuona MWANANGU Akikanyagwa kanyagwa tena na tena. YEYE ni Mpendwa WANGU! Na NIlimtoa kwa ajili yenu! Kwa hivyo NInaachilia moto WANGU baada yenu nyote. Na NInafukuza maadui WANGU. NInawafukuza hadi kwa vimo, hata vya bahari. NInashika maadui WANGU wote. NInawakumba kwa kishindo na kuwarusha chini. Hilo pia ni kwenu ufalme wa Maji! Kwa maana hakuna ufalme ila Ufalme WANGU. Ufalme WANGU ambao upo, ambao utakuwa (Dan. 2:44-45). Na Nawathubutu, Nawathubutu kusimama dhidi YANGU! Kwa maana MIMI ni MFALME Mkuu, MWANAUME wa Vita! Na kwa hakika NInaongoza Majeshi YANGU, MajeshiYANGU, kupigana na ni ushindi tu Tutaona. Na ulishindwa pale Msalabani. Na NInaimarisha ushindi WANGU juu yenu.


Kwa hivyo NIsikizeni sasa, ikiwa una nafasi yoyote, na NIlisema, “Kwenye magoti yako utaanguka na kutubu.” Tubu KWANGU! Tubu KWANGU! Kimbia hiki kizazi potovu. Kwa maana kunao wengi ambao hata si wanadamu na wanapotosha Dunia na uumbaji wa ajabu na kubadilisha Sheria ZANGU; na upotovu wao, vitu ambavyo yeyote hapaswi kujua, wacha hata kuvizungumzia! Na Nataka mjue NItachoma hii dunia na moto usiozimika (Malachi 4:1)! Kwa maana NImemalizana nanyi nyote. Kwa maana hamtaNIdhihaki na kuNItusha kabisa! Kwa maana ni MIMI ambaye NItakuwa na kicheko cha mwisho. She'ol inapowadai nyinyi nyote, ambao hamjafunikwa na Damu ya MWANANGU YESHUA.

Mwisho wa Neno

8 views0 comments
bottom of page