top of page

Unabii 47 “Ee Israeli, Msitumainie Ufaransa Au Ndani Yenu Wenyewe, Lakini Katika “NDIMI NILIYE” Mkuu

Updated: Mar 24


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 9 Julai, 2019


Maandiko Husika


Isaya 57:16-18: “SItaendelea kulaumu milele, wala SItakasirika siku zote, kwa kuwa roho ya mwanadamu ingezimia mbele zangu: yaani pumzi ya mwanadamu NIliyemuumba. NIlighadhibika na tamaa yake ya dhambi; NIlimwadhibu, NIkauficha uso WANGU kwa hasira, na bado aliendelea katika njia zake za tamaa. NImeziona njia zake, lakini NItamponya, NItamwongoza na kumrudishia upya faraja.”


Kumbukumbu 30:19-20: “Leo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi, na ili upate kumpenda YEHOVAH MUNGU wako, uisikilize sauti YAKE na kuambatana NAYE. Kwa kuwa YEHOVAH ndiYE uzima wako, na Atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi Aliyoapa kuwapa baba zako Abrahamu, Isaka na Yakobo.”


Ujumbe wa Kinabii

Ee nchi ya Warubeni, ee Ufaransa, ni nyinyi ambao mmetibua maji yenu wenyewe, mkichochea uchafu na kinamasi cha uchafu wenu wenyewe. NIliangalia kutazama maji safi na [maji] yaliyopo ya Mto WANGU wa Uhai, badala yake NIkaona kutotengamaa na najisi imeenea kote nchini (Mwanzo 49:3-4).


Mbona mjichafue wenyewe, ee Israeli? NIliwaambia “msiguse kitu najisi,” kwa maana hili halikubaliki kabisa machoni MWANGU, katika macho ya TORAH YANGU ILIYO HAI (Isaya 52:11, 2 Wakorintho 6:16-18). NIlikuja kuwaweka huru lakini mlijiunganisha nira na najisi ya mataifa. Ni nini Ufaransa iko nayo hadi mnaNItupa MIMI, NDIMI NILIYE MKUU, kwa ajili ya vipande vya fedha na dhahabu pekee? NIliwaambia msirudi Misri lakini mlisisitiza, kwa hivyo NIliwaacha mzuru, ishi katika banda la nguruwe la kinyaa na aibu. NInawahukumu kwa hili na NItawahukumu.


Gharama kubwa mtalipa! SIkuwahi waambia mtumainie katika Warubeni kwa usalama wowote kabisa. Ni nani ambaye hamjalala naye? Chini ya mti upi mkuu juu ya mlima wa dhambi na uabudu sanamu hamjajinajisi (Yeremia 3:6)? NItapindua milima yenu mikuu na jukwaa za machukizo (Ezekieli 6:3). Mnatoa dhabihu pale mkifikiri mnaNIpendeza lakini hili liko kabisa dhidi ya Torah YANGU; chukizo kubwa dhidi ya Neno LANGU. NIliwaonya zamani msichanganye kikombe cha mashetani na Kikombe cha BWANA MWENYEZI. Hili linawaingia?


Ee Israel, Nawaadhibu! NInawavunja! Maneno YANGU yote ni ndiyo na amina bila kujali ufafanuzi wenu binafsi. Njia ZANGU ziko juu zaidiya njia zenu (Isaya 55:9). MmeNIsahau katika usitawi wenu, lakini SIjawasahau Asema BWANA Mwenyezi NDIMI NILIYE Mkuu. NDIMI NILIYE Awaita mrudi KWANGU, Anatuma WANGU Wawili Walioaminiwa – Moshe na Eliyahu WANGU (Ufunuo 11).


Watakuja na moto katika pumzi yao kuwaadhibu, kuwahukumu na Maneno ya Uhai. Mtahisi Moto wa Neno LANGU ambao ulikuwa umefungiwa, umebanwa katika mifupa ya Yeremia kwa ajili yenu, ee Israeli. Msifanye mioyo yenu migumu dhidi YANGU, MIMI YEHOVAH, kama katika siku ya ushari (Zaburi 95:8-11). Huu ni mwisho wa zama. Muda ni mfupi kwenu, ee Israeli, mfupi tena sana. Karibuni mpinga-masia atakuja, atatokea na maneno ya upendo mdomoni mwake, lakini hati-kunjo anayokuja amebeba haikuandikwa wala kuwekwa muhuri na MIMI, na Zerubabeli.


Hizi ni Nyakati za Mwisho na NItafanya matangazo dhidi ya mataifa, kwa maana MWANANGU, MASIA wa kweli, Yuaja! Hatashindwa, [hata]pitwa. YEYE ni MFALME wa Utukufu Mkubwa na “YESHUA" ndiyo JINA LAKE! Kwa hivyo tubuni siku hii kwa ajili ya upumbavu na upuuzi wenu mkubwa, ee Israeli. Mnafukuza waadilifu, mkiwapa kikombe cha uchafu wanywe.


Hamfai kujaribu Watakatifu, au kuweka kikwazo mbele yao. Kile ambacho NImewaambia msifanye, kitu kiki hiki mnatafuta. Njia zenu ni za kurudi nyuma lakini NItarekebisha njia zenu na kusafisha waasi kutoka kwa nchi yenu, migao ya kabila zenu (Isaya 57:16-18). Wale wasio watakatifu hawatakaa NAMI. Wale wenye kutubu pekee, wale wanaoomba msamaha kutoka KWANGU katika JINA la YESHUA MASHIAKH wenu kwa maana dhambi zenu zitakaa naMI katika nuru, katika Ukweli, katika Utakatifu, ee Israeli!


Kwa hivyo inameni mbele ZANGU siku hii. Msikimbie mguso WANGU. Hukumu YANGU inasulubisha mwili, ikiwa mtaruhusu. Ikiwa mtaamini na kupokea ripoti YANGU, itakuwa vyema nanyi. Kuepuka Neno LANGU ni kutafuta kifo. NImeweka mbele zenu uhai na mauti, baraka na laana (Kumbukumbu 30:19-20). Chagueni uhai! Chagueni YESHUA MWANZILISHI wa Uhai ili muishi – wewe na nyumba yako. Amina na Selah.



Mwisho wa Neno

3 views

Recent Posts

See All
bottom of page