top of page

Unabii 62 ‘“MIMI na NENO LANGU ni Aminifu na Kweli,” Asema MWENYEZI MUNGU!’


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 20 Julai, 2019
Maandiko Husika


Zaburi 33:4

“Maana Neno la YEHOVAH ni haki, na matendo YAKE yote yanafanywa katika ukweli.”


Mithali 30:5

“Kila neno la MUNGU ni kamilifu; YEYE ni ngao kwa wale wanaoMtumainia.”


1 Yohana 2:22-23

“Je, mwongo ni nani ila mtu yule asemaye kwamba YESHUA si MASIA? Mtu wa namna hiyo ndiye mpinga Kristo, yaani, yeye humkana BABA na MWANA. Hakuna yeyote amkanaYE MWANA aliye na BABA. Yeyote anayeMkubali MWANA anaYE na BABA pia.


Ujumbe wa KinabiiNIandameni MIMI, ee Waadilifu. NIwekeni kwanza katika maisha na upendo wenu. Shikeni Amri ZANGU na mtafanya vyema. Msikataze watoto wadogo kuja KWANGU Asema MIMI, YESHUA MASHIAKH na BWANA wenu Aliye na upendo (Mathayo 19:14). Fungua roho yako na uNIpe yako yote. NIpe kila kitu chako na usishikilie chochote nyuma.


NIlikupa Torah YANGU, Neno LANGU la Ahadi. Ruhusu mikono YANGU kukufinyanga na kukuumba. Usijenge maisha yako juu ya matuta ya mchanga wa wakati na uovu. Jijenge kwenye MWAMBA wa Milele, juu ya “NDIMI NILIYE” Mkuu (Mathayo 7:24-25). Hautatikiswa au kufadhaishwa. Usikate tamaa na maisha yenyewe. NImewapa uhai na uhai tele zaidi (Yohana 10:10). Sasa tembeeni ndani yake.


Msione Amri ZANGU kama mzigo na pingu. Msione Neno LANGU kama kawaida au bure. SIzungumzi tu bure au kusikia tu sauti YANGU. Ubatili hauna sehemu yoyote ndani YANGU na haukuwahi. MIMI, YESHUA, ni kamili katika Njia ZANGU zote (Zaburi 18:30). Unaweza NIamini. Unaweza amini BWANA MUNGU MWENYEZI. Unaweza amini Neno LANGU, kwa maana MIMI ndiYE Neno-lililofanywa-mwili, Wingi huo ulitoka kwenye Moyo wa BABA YANGU.


Kwa hivyo NItazamieni MIMI, ELOHIM wenu ambaYE mipango YAKE kwa ajili yenu ni kwa uzuri na sio kwa uovu (Yeremia 29:11). NDIMI NILIYE Anawavuta KWANGU. Fanyeni kile NInawaambia mfanye. Fanyeni kile Nawaambia mfanye. Kwa maana kila Neno LANGU ni “ndiyo” na “amina” (2 Wakorintho 1:20). SIwezi feli, nanyi pia hamtafeli mradi muendelee kushikilia imara kwenye upindo wa nguo YANGU. Shika imani! Shika furaha! Tembea katika shalom (amani) siku zote za maisha yako.


MIMI, YEHOVAH MUNGU, ni Mhaki na Mkweli. Shalom ni YANGU. Shalom iko na MIMI. Tafuta amani YANGU ambayo inafungua dunia nzima mpya ya uwezekano. Yaliyozeeka yanapita, yanaoza na kushutumiwa. Tembea katika Nuru, Nuru YANGU, na mtakuwa wazima. Inua Torati na msitembee kulingana na hukumu ya adhabu. Neno LANGU ni Uzima (Yohana 5:24). Neno LANGU ni mwelekeo. Kwa hivyo kaeni katika Mapenzi YANGU. Ni nini Mapenzi YANGU kwa maisha yako? Tafuta Uso WANGU (Zaburi 27:8, Hosea 5:15). Tafakari juu ya Neno LANGU na ule Mana YANGU ambayo ni ya kila siku kwa ajili yako, yote (mbili) katika msimu na nje ya msimu, nyakati zote inafaa, nyakati zote ni mpya [fresh].


Hakuna aliye kama MIMI, MFALME wa Milele, MWAMBA wa Milele. JINA LANGU ni YEHOVAH na NImetuma MWANANGU kuwa MWANGA wenu wa Kuongoza, MCHUNGAJI wa Milele, wa Uaminifu. Anawaongoza kando ya maji matulivu na kuwaongoza katika Njia Nyoofu (Zaburi 23). Hamwezienda kombo katika kuMufuata YEYE, Watoto WANGU. Ijapokuwa elfu moja wataanguka kando yako na elfu kumi kwa mkono wa kulia, endelea na ujue hii ni njia YANGU kwa ajili yako, nyayo za uadilifu kwa ajili yako, Mtoto WANGU (Zaburi 91:7).


Misiba ikiangukia wale wote kando yako haimaanishi uko katika uasi. Kila mtu huvuna kile anachopanda. Shukuru tu kwamba haiji karibu na makazi yako. Shukuru kuwa katika Zaburi 91 unasimama, katika Zaburi 23 unakaa. Shukuru kuwa Malaika WANGU wako hapo kukuinua ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe, isije ukajikwaa kwenye kosa la shetani.


Kuwa wenye shukrani ndani YANGU, WanaNGU. Kuweni wenye shukrani na msitie shaka. Shaka ni roho ya mauti. Kwa hivyo tahadharini na mfuate Njia ZANGU. Fuata Torah YANGU ambayo haina miaka. YESHUA Alishika [Alitii] Torah. YESHUA ndiYE TORAH Iliyo Hai, kwa maana je, YEYE si Njia, Ukweli na Uzima (Yohana 14:6)?


Ee Israeli, ee Israeli MIMI, YEHOVAH, SItawacha kukuita hadi urudi mikononi MWANGU. Damu ya MWANANGU ilimwagika kwa ajili yenu pale Kalivari. Damu YAKE inaNIlilia kutoka mchangani, kutoka mchanga wa Kiyahudi! Kwa hivyo mbona mfikiri NIngewaambia kupeana hiyo ardhi? NIngefanyaje hivyo? Ardhi ambapo MWANANGU Alimwaga Damu YAKE, pale Aliteseka maumivu makali yasiosemeka, SIwezi kamwe kuwaambia mtelekeze, msalimishe. Lindeni kilicho dhati KWANGU. Lindeni Torah YANGU. Lindeni Njia ZANGU na mshike Amri ZANGU, kwa maana kwa [sababu ya] hili watajua nyinyi ni WANGU. Kwa maana kushika Amri ZANGU na moyo takaso ni kuNIpenda.


NIpendeni. NIpende MIMI wote, ee Israeli. Ukataaji wa MWANANGU lazima ukome, sasa! Kwa kweli mnapoMkataa, mnaNIkataa MIMI (1 Yohana 2:22-23). Hamwezi kuwa na Mbinguni bila YEYE. Bila Damu ya YESHUA HAMASHIAKH iliyomwagika kwa ajili ya upatanisho wa nafsi zenu, mmeangamia pasipo shaka yoyote. Haijalishi ikiwa wewe ni Myahudi mzaliwa-damu. Ikiwa hauna YESHUA, kwa kweli hauna MIMI. Kwa hivyo tubuni, ee Israeli! Tubuni, ee Yuda! Tubuni, ee Efraimu! Au mtaonja Ghadhabu YANGU. NImekuwa Mvumilivu muda mrefu wa kutosha. Rehema YANGU NImeendeleza. Neema YANGU NImemwaga. Lakini SItaendelea kudhihakiwa, hata na wale ambao NImechagua (Israeli)! Wote lazima wavune kile wamepanda.Itaendelezwa

7 views

Recent Posts

See All
bottom of page