top of page

Unabii 53 “Israeli, Fungueni Macho Yenu Kwa Torah na MsiMkatae YESHUA!”

Updated: Mar 24


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa Oktoba 26, 2019

Umepokewa 26 Oktoba, 2019 – asubuhi mapema

Maandiko Husika


Mathayo 24:4-5

YESHUA Akawajibu na kuwaambia, “Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye. Kwa maana wengi watakuja kwa JINA LANGU, wakidai, ‘Mimi ndiye MASHIAKH,’ nao watawadanganya wengi


Isaya 1:16-18

16 jiosheni na mkajitakase. Yaondoeni matendo yenu maovu mbele ZANGU! Acheni kutenda maovu, Jifunzeni kutenda mema! Tafuteni haki, watieni moyo walioonewa.

Teteeni shauri la yatima, wateteeni wajane. “Njooni basi tuhojiane,” Asema YEHOVAH. “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji; ingawa ni nyekundu sana kama damu, zitakuwa nyeupe kama sufu.


Ujumbe wa Kinabii


Moshe atakuja tena lakini na moto machoni mwake na [zile] amri mikononi mwake (Yohana 5:45-47). Israeli yote itaona UTUKUFU WANGU, Asema MIMI, YEHOVAH. Wataona UTUKUFU WANGU na UTUKUFU wa MWANANGU wa Pekee wa MILELE – YULE WA MILELE AsiYE na doa, AsiYE na dosari.


Ee Israeli, Alikuja mara ya kwanza na mkaMkataa (Yohana 1:11). Je, mtaMkataa tena? Anawalilia. Moyo WAKE unawalilia, ee Israeli. “YESHUA HAMASHIAKH” ndiyo JINA LAKE (Mathayo 1:21, Luka 1:30-33). MuIteni katika saa yenu ya giza. MuIteni wakati elfu wataanguka kwa upande wenu na elfu kumi kwa mkono wenu wa kulia ili yasije karibu nanyi (Zaburi 91:7). Mapigo, ee mapigo yatashuka na yatakuja chini NInapomwaga bakuli ZANGU za laana mara moja tena. Yale yaliyokuwa ndiyo yatakayokuwa. Yale yatakayokuwa ndiyo yale yaliyokuwa, kwa maana hakuna chochote kipya chini ya jua.


NIsikilizeni, ee Israeli, na mjue furaha kamili. Jueni furaha kamili kupitia MWANANGU YESHUA ambaYE ndiYE MWANA wa UADILIFU ambaYE Amesubiriwa sana. Mngojeeni, ee Israeli, na msimtazamie mwengine (Mathayo 24:4-5). Msimtazamie mwengine na hamtadanganyika. Na macho ya mwili mmesoma Torah na mkadanganyika.


Kwani hamuoni MWAMBA wa MILELE Akisimama katikati yenu; YEYE Akiwa JIWE-KUU-LA-PEMBENI? Jengeni juu YAKE ambaYE ni mkuu kuokoa; YULE wa MILELE na MFALME wa UTUKUFU. NInawalilia, ee Israeli, MIMI, YESHUA, MKOMBOZI wenu AliYEjaribiwa na [ni] Mkweli. MIMI ndiYE ELOHIM wa MILELE. Kabla Abrahamu awe, kabla Moshe wa Zama, NDIMI NILIYE (Yohana 8:58-59).


Msiokote mawe ili mNIpige mawe. Msiamini hizi wongo za shetani. NImemshinda na kazi zake (1 Yohana 3:8). Kupitia MIMI mtajua ushindi pia. Jiosheni katika DAMU YANGU. Tubuni dhambi zenu na mfanywe weupe kama theluji (Isaya 1:16-18). NImekuja kuwatakasa, ee Israeli. NImekuja kuwakomboa kutoka kwa kazi ngumu, shida na mitego yenu. Lakini mtashibishwa [nayo] hadi wakati huo, hadi mtubu njia zenu za kurudi nyuma, ee Efraim.


Fuateni mfano WANGU na mzingatie njia ZANGU. SIkuja kughairi au kufuta Sheria na Manabii (Mathayo 5:17-19). SIkuja kutupilia mbali Njia ya Uadilifu, kwa maana je MIMI siYE Njia, Ukweli na Uzima (Yohana 14:6)? NIsikilizeni, ee Israeli! Sikilizeni na mtii. Sikilizeni na mjue uzima wa milele. Selah.


Mwisho wa Neno

3 views

Recent Posts

See All

댓글


댓글 작성이 차단되었습니다.
bottom of page