top of page

Unabii 67 “Ee Israeli, Tumainieni Katika YESHUA HAMASHIAKH!”


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 6 Novemba, 2019 – kabla tu ya usiku wa kati na sehemu ya pili ilipokewa 9 Novemba, 2019 Jumamosi asubuhi mapema

Maandiko Husika


1 Yohana 3:2-3

2 Wapendwa, sasa tu wana wa MUNGU, lakini bado

haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba YEYE

Atakapodhihirishwa, tutafanana naYE, kwa maana tutaMwona kama Alivyo.

3 Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani YAKE hujitakasa, kama vile YEYE Alivyo Mtakatifu.


Mathayo 24:15-18

15 “Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’

lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu”

(asomaye na afahamu),

16 “basi wale walioko Uyahudi wakimbilie milimani.

17 Yeyote aliye juu ya dari ya nyumba asishuke ili

kuchukua chochote kutoka ndani ya nyumba yake.

18 Aliye shambani asirudi nyumbani kuchukua vazi lake.


Yeremia 17:7

“Lakini amebarikiwa mtu ambaye tumaini lake ni katika YEHOVAH,

ambaye matumaini yake ni katika YEHOVAH.

Ujumbe wa Kinabii


Andika, kwa maana haya Maneno yako upesi na kweli, hai na hayajakufa! NInakuja, ni kweli, kwenye mabawa ya upepo kusafirisha (kutupa) maadui WANGU na kunyakua watoto WANGU hai. Naja na MIMI si mfu – MIMI, YESHUA.


Wale ambao wanaotia shaka kuja KWANGU wamekosea kabisa. Wale wanaotia shaka Kufufuka KWANGU wamekosea kabisa – fukara na hohehahe wa imani. Kuweni wenye nguvu katika hizi nyakati za mwisho. Kuweni na imani katika Tumaini la Kufufuka KWANGU, kwa maana vile NIlivyo ndivyo mtakavyokuwa ikiwa mna imani na msikose, msitie shaka (1 Yohana 3:2-3).


Kutia shaka ni kuchafua maji, kuchochea matope na uchafu [uliopo] chini. Kwa hivyo kuweni watulivu na njooni mtembee juu ya maji naMI MWOKOZI wenu, YESHUA wenu. MIMI NIKO hai na si mfu. Na hivyo ndivyo imani yenu yapaswa kuwa. SIwezifanya kazi na imani iliyokufa lakini Nawezafufua (Yakobo 2:14-26). NIite leo na NItainua hema la maisha yako lililoanguka. Halafu ufurahie na ujue kuwa kazi YANGU ni aminifu na kweli!


Furahieni na msitie shaka, kwa maana mtu yeyote mwenye nia mbili husitasita katika njia zake zote (Yakobo 1:5-8). Ruhusu DAMU YANGU kukutakasa, ee Israeli. Hekalu (ya tatu) itajengwa na lazima itajengwa, ni kweli, ili Maandiko yatimie – mstari juu ya mstari na kanuni juu ya kanuni (Mathayo 24:15-18, 2 Wathesalonike 2:1-4). Lakini mjue hili, dhabihu zenu ni bure, ee Israeli, kwa maana MIMI ndiYE UPATANISHO wenu wa MWISHO wa DAMU na hakuna nyingine.


Tubu, ee Israeli, na na mje katika mikono ya upendo ya MASIA wenu Ben David. MIMI, YESHUA, NIko hapa kuwaokoa ikiwa tu mtaruhusu, ikiwa tu mtainamisha goti lenu na kukiri na mdomo wenu kwamba MIMI NDIYE. Basi mtasitawi na kuchanuka kama waridi jangwani.


Wewe na MIMI Tunafana sana, ee Israeli (Isaya 52:14). Kuteswa sana, kukataliwa zaidi. Lakini achenikuNIkataa MIMI ee Israel, kwa maana MIMI ndiYE Tumaini lenu la UTUKUFU, NURU yenu ing’aayo gizani. Mnasema mnaona, lakini hamuoni Ukweli [uliomo] ndani YANGU (Yohana 14:6). Kwa hivyo unabaki kipofu.


Eden ni angahewa. Eden ni ufalme. Ikiwa tu mtatii, mtapata amani YANGU ndani yake, kwa maana wabarikiwa ni wale wote ambao wanaweka tumaini na ukaaji wao ndani ya MIMI, YEHOVAH (Yeremia 17:7). Je mnaNIsikia, ee Israeli? NIlisema wabarikiwa ni wale wote wawekao tumaini lao ndani YANGU, kwa maana hawatafedheheshwa. Hawatafedheheshwa lakini watakombolewa kutoka kwa malalamishi yao yote.


MIMI NI MWANGA. MIMI NI MFALME. MIMI NI MWENYEZI MUNGU katika mwili. MIMI, YESHUA, NIko hapa leo, ee Israeli! Leo ndiyo siku yako ya wokovu (2 Wakorintho 6:2). Msipoteze dakika nyingine. Msichelewe. Nani yuajua kile kesho yatazama? Ni MIMI, YESHUA tu. Ni MIMI, YEHOVAH tu. Ni MIMI, IMMA tu. Ni MIMI, URIYAH tu. Kwa hivyo tazama na msitie shaka. Nasimama mlangoni na kubisha, mlangoni mwa mioyo yenu, ee Israeli. Kwa hivyo NItazameni MIMI hii leo na mmbadilike. Kuweni wapya. Njooni mnywe MAJI YALIYO HAI siku hii, kwa maana si mikono YANGU iko wazi kuhuisha wahitaji na kushibisha kila nafsi iishiyo (Zaburi 145:16)?


Mnajua Torah. Kwa hivyo ifanyeni. Njooni KWANGU na mfanywe wazima. Njooni KWANGU na mfanywe wapya, kwa maana NIna ujumbe kwenu.


Mwisho wa Neno

1 view

Recent Posts

See All
bottom of page