top of page

Unabii 72 “Patikaneni Katika MASHIAKH, Ee Israeli!”


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 16 Novemba, 2019


Maandiko Husika


Isaya 52:1-2

1 Amka, amka, ee Sayuni, jivike nguvu.

Vaa mavazi yako ya fahari, ee Yerusalemu, mji mtakatifu!

Asiyetahiriwa na aliye najisi hataingia kwako tena.

2 Jikungʼute mavumbi yako, inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, ee Yerusalemu!

Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako, ee Binti Sayuni uliye mateka.


Luka 1:31-33

31 Tazama, utachukua mimba, nawe utaMzaa MTOTO MWANAUME na utaMwita JINA LAKE YESHUA. 32 YEYE Atakuwa mkuu, naYE Ataitwa MWANA wa ALIYE JUU SANA. YEHOVAH ELOHIM AtaMpa kiti cha enzi cha Daudi baba YAKE. 33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na Ufalme WAKE hautakuwa na mwisho.”


Ujumbe wa KinabiiUsiogope, mpendwa WANGU. Usiogope. Shikilia vazi LANGU na uje naMI. Ee Bi-Arusi WANGU, Nakutazama na macho yenye uchu, na macho ya moto. Hakuna anayeweza lingana na moto uliomo katika macho YANGU kwa ajili ya Bi-Arusi WANGU.


NInamchukulia kisasi. MIMI, YESHUA, Namtegemeza. Katika susu ya mikono YANGU NInambembeza kwa upole. Kwa hivyo kuwa katika amani, mwanaNGU. Usiwe na wasiwasi. Usiwe na wasiwasi juu ya waovu. NItawashughulikia katika wakati WANGU. Watakuwa mithali miongoni mwa mataifa, sio zaidi [ya hiyo] (Ezekieli 14:8).


Kwa hivyo NIkazieni fokasi siku hii. NInajaribu kope za mwanadamu kuona pale fokasi yao ipo. Je, wataNIkazia fokasi katika dhoruba dhalimu au watajitazamia, [tazamia] mkono wa mwili? Waona, mwanaNGU, lazima NIpure mataifa (Mathayo 3:12). Lazima NIkanyage shinikizo la mvinyopekee YANGU katika raghba na ghadhabu ya ALIYE JUU KABISA (Isaya 63:1-6, Ufunuo 14:19-20). Hakuna njia nyingine.


Mataifa yote lazima yasujudu mbele ZANGU, lazima yafungue mikono yao kuNIpokea, kukubali kwa moyo TORAH ILIYO HAI. NIko hapa kukaa na SIwezi kusongezwa. Ufalme WANGU ni Ufalme wa milele, unajaza upana wa dunia (Danieli 2:44-45, Luka 1:33). MWAMBA wa MILELE. JIWE KUU LA PEMBENI la MILELE.


MsiNIdharau, ee watu WANGU. Yakobo, kuwa msikivu. Israeli, sikiliza. Tilia maanani onyo ZANGU, watu WANGU, kwa maana SItamani muangamie. Karibuni na hivi karibuni sana NItakuja. Chukueni taa zenu za mafuta na mpatikane mkingoja, mkiNIngojea – [wewe, ee Israeli, ndiye] tufaha la jicho LANGU [kipenzi CHANGU].


Msishtakiane na kosa. Samaheaneni na muonyeshe upendo NIliwapatia wanadamu (Yohana 15:13). Msisahau masomo NIliwafunza – huruma, wema, upole, upendo. Tamani rehema badala ya hukumu. Kuweka mfungwa huru badala ya ukandamizaji. Fanya NIlivyofanya. NIlikuja kuweka mateka huru (Luka 4:16-21). Ifanye katika JINA LANGU YESHUA, kwa maana hakuna mwengine ana nguvu za kuokoa, kuponya, kukomboa katika jina lake.


NItawakanyaga, ee Israeli, kwa maana NImekuja kusanya divai ya msimu. Mtatoa nini? Divai inayoonja NInavyopenda? Mta[toa] nini? Msiwe kama nyongo chungu au ile siki iliyokuwa imeloweshwa kwenye sifongo iliyowekwa kwenye midomo YANGU (Mathayo 27:33-34). NItawatapika. Wale tu watakaso, wasiotiwa unajisi ndio Najipatia. Fanyweni wapya.


YEHOVAH Azungumza: Muoshwe katika DAMU ya kuNIpendeza, katika DAMU ya MWANAKONDOO AsiYE na doa, MWANANGU YESHUA. YEYE ndiYE dhabihu yenu ya milele. Zingine hazisimami. YEYE ndiYE Upatanisho wa Mwisho na ukamilisho wa Torah, Akiwa Njia, Ukweli na Uzima. Msikieni, ee Israeli. Msisikie mwengine, kwa maana katika HUYU MCHUNGAJI MWEMA kuna wokovu (Yohana 10:11-18). Msisikie sauti ya mwengine, ya mgeni, ya mfanyikazi wa kukodiwa, ya mbwa mwitu.


Wanasimama katikati yenu – katika mahali pa soko, katika miundo yote ya serikali kote nchini. Msiwasikize ingawa wanaweza kufanana na nyinyi. Kwa kweli wao ni mbwa mwitu katika mavazi ya kondoo, [wameji]weka kula kondoo. Mtii tu na hamtadanganyika, hamtachukuliwa kama nyara. Kwa maana wengi watakufa, wengi wataangamia katika moyo wa uasi (Zekaria 13:8-9). Msifanye mioyo yenu migumu, ee Israeli (Zaburi 95:8-11). Mna umbo la KUMCHA MUNGU lakini uko wapi KUMCHA MUNGU ndani [yenu]?


Kule kukariri maombi, kule kuimba Neno LANGU sio wokovu. Katika tu MWANANGU YESHUA kunapatikana TUMAINI lenu la UTUKUFU (1 Petro 1:17-21). Pateni kuMjua leo. Karibuni na hivi karibuni sana giza litafunika ardhi na Safina itafungwa. Mtafanya nini, ee Israeli, katika hizo nyakati za giza? Ni heri mwe mmechenga utambi wenu na moyo wenu uwe umejaa UTUKUFU WANGU. Ni heri mpatikane ndani YANGU.


Kaeni ndani YANGU, ee Israeli, na mtubu dhambi zenu. Geukeni toka kwa njia zenu za uovu na mNIfuate na moyo wa toba ya kweli (Zaburi 51:17). Msije tu KWANGU kwa ajili ya baraka. Nabariki, ndiyo, lakini Natamani uhusiano na kila mmoja wenu. Tafuteni uso WANGU na msujudu mbele ZANGU. NInayo mipango mizuri sana juu yenu. Msigeuze kando mkono WANGU unaowaongoza. Msigeuze kando Mkono WANGU wa Wokovu ambao unaokoa.


Msifanye shingo zenu ngumu katika uvuguvugu. NItawaamsha, ee Israeli, kwa maana kile kimetabiriwa lazima kitimie (Isaya 52:1-2). Manabii watakatifu hawakuwa waongo. SItaruhusu maneno yao yaanguke ardhini kama bure na matupu, kwa maana ni Maneno YANGU (Isaya 55:10-11). Maneno YANGU ni moto unaoteketeza makapi. Maneno YANGU yanagawanya, yakiweka wazi njia iliyowekwa mbele zenu. Maneno YANGU yanazaa, yakileta mtoto mchanga toka kwenye tumbo.


NIsikie MIMI, ee Israeli! Nakujia Bi-Arusi takaso na asiye na doa! Wewe ni yupi?

Msizuilike katika kuNIsifu MIMI, kwa maana humo mnao ufunguo wa ushindi. Selah.


Mwisho wa Neno.

4 views

Recent Posts

See All
bottom of page