top of page

Unabii 73“‘Mipango YANGU Kwa Ajili Yenu ni kwa Uzuri na NImewapa Amani,’ Asema YEHOVAH ELOHIM”


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 18 Machi, 2019

Maandiko Husika


Yeremia 29:11

Kwa maana NInajua mipango NIliyo nayo kwa ajili yenu,” Asema YEHOVAH, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.


Yohana 15:5-6

5 “MIMI ni mzabibu, ninyi ni matawi.

Akaaye ndani YANGU, naMI ndani yake, huyo huzaa sana,

maana pasipo MIMI ninyi hamwezi kufanya jambo lolote.

6 Mtu yeyote asipokaa ndani YANGU, hutupwa nje kama tawi na kunyauka.

Matawi kama hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea.

Ujumbe wa Kinabii


NItapura zile bahari saba na zile bahari zingine pia na kifaa CHANGU, na Mkuki WANGU wa Milele wenye Vyembe Vitatu [Traidenti]. Hakuna atakayeachwa akisimama. Wote wataangushwa chini ya Ghadhabu ya MUNGU ALIYE HAI ambaYE pekee JINA LAKE ni TUKUFU KABISA na ADILI.


NInafanya mpya kile kimetupwa na kukataliwa na mwanadamu (Ufunuo 21:5). Kile ni chukizo machoni mwake, MIMI NInarekebisha, [Na]fanya mpya. Hakuna aliye kama MIMI, watoto WANGU. Bila MIMI, nyote mnaanguka, mnapelekwa na bahari na mnapotea katika michanga ya wakati; mnazikwa chini ya mawimbi ya kukumba.


Lakini mipango YANGU kwa ajili yenu ni mizuri na si mibaya (Yeremia 29:11). SIkuwaambia amani YANGU Naiacha nanyi? SIwapi kama dunia inavyopeana lakini na amani inayopita kuelewa ambamo hakuna wivu, hakuna ugomvi, hakuna ushindani (Yohana 14:27, Wafilipe 4:6-7). Utulivu pekee. NIliwaahidi hii amani hata katika katikati mwa dhoruba.


Nyinyi, watoto WANGU, mmekuwa katika dhoruba isiyo na kifani, ndiyo. Mmehisi [zile] athari mawimbi yalivyoanguka dhidi ya nyumba, [zi]limbembeza safina mbele na nyuma hata kama vile Noa alihisi. Kusudi LANGU si kuwaogopesha, watoto WANGU, lakini kuwafanikisha katika njia zote. Kutikisa kila kitu kinachoweza tikisika. Kwa nini, mwaweza uliza? Mara nyingine mti huhitaji usaidizi kuondoa matunda ambayo hayataanguka kwa njia nyingine yoyote. Kwa hivyo Natumia Upepo WANGU kuwatikisa muamke, kuondoa tunda lolote lisilopendeza kabla BWANA Aje. Kwa maana, watoto WANGU, hamtaki Aje kwenu na mpatikane mnakosa kinachotarajiwa kama ule mtini ambao haukutoa matunda (Mathayo 21:9).


La, watoto WANGU, hamtaki patilizo kama hilo. Wengi sana watateseka jaala kama hiyo na wakataliwe milele, wakisimama kama ishara ya kile cha kutofanya kama vile huo huo mtini uliolaaniwa ambao bado unasimama katika Israeli hadi siku hii. Usijiruhusu kuwa nguzo ya ishara kama bibiye Lutu (Mwanzo 19:26). Huu ni ujumbe wa huzuni sana, kwa maana nyakati za huzuni ziko juu Yetu. Na Nasema “Yetu” kwa sababu NDIMI NILIYE YUKO nanyi hadi hata mwisho wa nyakati. Naahidi kutowahi waacha au kuwatelekeza, je, SIku[ahidi] (Waebrania 13:5)? Fanyeni tu sehemu yenu na NItafanya YANGU. MsiNIzuie tu. NItakamilisha kile ambacho NILianza na kufanya kazi safi, kamili.


Kaa ndani YANGU na NItakaa ndani yenu (Yohana 15:5-6). NIfanyieni MIMI kama vile NDIMI NILIYE Amewafanyia nyinyi. Msitie shaka. Msiwe na wasiwasi. Nafanya vitu vyote vipya. NInakumbatia kila mmoja wenu kama vile BABA hukumbatia mtoto ambaye [ametoka] tu kutubu kwa kufanya kosa wakati alijua kufanya wema. NIimbieni tu, watoto WANGU, kwa maana NImechoka na hii enzi ya uovu. Kwa kweli Nachoshwa na Naitamani iwe imeisha.


Mwingi sana, ukatili mwingi mwanadamu amefanya, ameNIfanyia MIMI. Ndiyo, NItaJIchukulia kisasi. NItanoa upanga WANGU wenye ncha mbili unaometameta na kudhihirisha hukumu ZANGU zote ili dunia ione, ili dunia ione Utakatifu WANGU, Ukuu WANGU, Upendo WANGU (Kumbukumbu 32:40-42). Ndiyo, katika hivi vitu vyote, NDIMI NILIYE bado ni MUNGU wa Upendo. NDIMI NILIYE ni upendo (1 Yohana 4:8). Hiyo ndiyo maana hakuna mmoja wenu amefagiliwa mbali. Kwa hivyo NIsifuni kwa ajili ya hili, watoto WANGU. BABA yenu YEHOVAH Anawapenda. MAMA yenu MPENDWA SANA SHKHINYAH GLORIA Anawapenda. MWOKOZI wenu MPENDWA SANA Anawapenda na DADA wenu mpya wa MWANGAZA SOFIA URIYAH Anawapenda.


Sasa nendeni na muongezeke. Nendeni na msitawi. Huu si wakati wa kufanya michezo. Ni wakati tu wa utiifu madhubuti, usiobadili msimamo. Kwa hivyo NIsikieni siku hii, watoto WANGU.


Mwisho wa Neno.

5 views

Recent Posts

See All
bottom of page