top of page

Unabii 74 "“Siku 3 za Giza!”


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 14 Aprili, 2019

Maandiko Husika


Kutoka 10:21-23

21 Kisha YEHOVAH Akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili giza litande katika nchi ya Misri, giza ambalo watu wanaweza kulipapasa na kulihisi.” 22 Kwa hiyo Musa akaunyoosha mkono wake kuelekea angani, na giza nene likafunika pote katika nchi ya Misri kwa muda wa siku tatu. 23 Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Waisraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo yao waliyokuwa wanaishi.


Yashari [Jasher] 80:36-40

36 Na MUNGU Akatuma giza juu ya Misri, hadi kwamba nchi yote ya Misri na Pathros ikawa giza kwa siku tatu, ili kwamba mtu hangeona mkono wake wakati aliunia kwa mdomo wake.

37 Katika wakati huo watu wengi wa Israeli walikufa ambao walikuwa wameasi dhidi ya YEHOVAH na ambao hawakusikiza Musa na Aroni, na hawakuwaamini kwamba MUNGU Alikuwa Amewatuma.

38 Na ambao walisema, Hatutatoka Misri hata tusije tukaangamia na njaa katika jangwa kame, na ambao hawakusikiza sauti ya Musa.

39 Na YEHOVAH Aliwapiga mapigo katika hizo siku tatu za giza, na Waisraeli waliwazika katika hizo siku, bila Wamisri kujua kuwahusu au kufurahia juu yao.

40 Na hilo giza lilikuwa kuu sana katika Misri kwa siku tatu, na mtu yeyote ambaye alikuwa akisimama wakati hilo giza lilikuja, alibaki akisimama mahali pake, na yule ambaye alikuwa ameketi alibaki ameketi, na yule ambaye alikuwa amelala aliendelea kulala katika hiyo hali, na yule ambaye alikuwa anatembea alibaki ameketi juu ya ardhi hapo hapo mahali; na hiki kitu kiliwatukia Wamisri wote, hadi giza likapita.

Ujumbe wa Kinabii


Ona kuna giza linakuja. Litakuwa muujiza wa kutazama. Hofu kuu itakuwa kila mahali. Kwa hivyo kaeni ndani, watoto WANGU wadogo. Sikizeni BABA yenu EZRA, watoto WANGU, NInapoMpa maagizo ya kile cha kufanya. Msikize na msikose kuMtii. Kuna vita vyaja. Hilo giza litachokonoa hivyo vita. Mauti na hofu kuu ya ghafla itakuwa kila mahali.


Wengi watakufa, mwanaNGU. Naam, wengi watakufa wakati huo wa siku tatu za giza. Kwa hivyo kaeni ndani na mjifiche kwa muda mfupi hadi kiruu CHANGU na ghadhabu YANGU ipite. Ni masalio wachache, kundi teule katika dunia nzima litajua [giza] linakuja na kuwa tayari. Wengine wote watateseka maumivu makali yasiyosemeka katika njia fulani.


Inategemea lile umeNIfanyia, inategemea lile umeNIfanyia hilo litakuwa ulinziwako, kinga yako. Kwa hivyo kaeni ndani, watoto WANGU wadogo, na mjihifadhi ndani YANGU, YESHUA wenu. Funikeni madirisha, funikeni ukingo za kutiwa katika madirisha. SItaki makosa yoyote, uzembe wowote. Hili ni muhimu. NImeweka katika EZRA lile la kufanya kuhifadhi na kulinda kile [ambacho] ni CHANGU. Kwa hivyo sikizeni maagizo YAKE na mtasitawi.


NDIMI NILIYE Amechoshwa na kutokuwa na shukrani kwa hii dunia, shutuma ya chukizo KWANGU MIMI. Fungeni na muombe. Fungeni na muombee ukombozi kutoka kwa huu wakati muovu, wa giza na mbaya. Lazima NIwafikishe mahali salama mwanaNGU, kwa maana SItaki mshikike, mtatanishwe katika giza la siku hizo. Ni mtego juu ya wanadamu kwa ajili ya matendo yao yote ya uovu na chukizo. Huchezi na ALIYE JUU KABISA na ufikiri hautapata kuunguzwa. Machinjo yatakuwa mengi na makuu siku hiyo.


Wafalme wa dunia watajutia ile siku waliwahi zaliwa. NItakabiliana na malaika walioanguka, wale walioanguka ambao wanajiweka kama wafalme juu ya wanadamu. NIliumba wanadamu watawaliwe na MIMI pekee. Lakini walijitafutia wafalme na wanaanguka katika tamaa tofauti tofauti na mbalimbali.


Ah tauni iliyoje juu wanadamu shetani amekuwa. Haikustahili kuwa hivyo lakini chaguo lilifanywa, chaguo lilifanywa. Msiogope, watoto WANGU wadogo, kwa maana BABA Amewaweka katika kiganjo cha mkono WAKE. Katika siku za mbeleni mtaona, ee wanadamu, jinsi gani Navyowapenda.


Hata hivyo, SItakingama hiari yenu na ikiwa mtasisitiza kwenye njia ya uasi, basi itakuwa kwamba mtakutana na mwisho dhalimu. NDIMI NILIYE si MUNGU muovu, AsiYEsamehe. SIzunguki kote NIkitafuta yule Naweza mmeza. Ni chaguo LANGU kwa wanadamu kuishi na kusitawi. Hiyo ndiyo maana NIlipeana MWANANGU wa Pekee – YESHUA HAMASHIAKH.


Ah, lakini Anavyodharauliwa, Anavyodhihakiwa! Si tofauti na Alipotembea duniani. Wengi walichukizwa naYE na kuMkataa, MWANANGU MPENDWA. Ee jinsi Navyosikitika, jinsi Navyolia kwa huzuni! Wanadamu mbona mnadharau na kukataa MPENZI wa nafsi zenu? YULE pekee ambaYE Anaweza waokoa? Na YESHUA HAMASHIAKH ndilo JINA LAKE.


Tubuni dhambi zenu na muoshwe katika DAMU ya MWANAKONDOO. Njooni kwa Mto wa Uzima na muoshwe, mufanywe safi, mbatizwe kwa ajili ya msamaha wa dhambi zenu. Nawapenda sana, ee wanadamu, na NImeandikia barua YANGU ya upendo katika Bibilia, katika nyota.


Mbona msigeuka nyuma? Mbona muangamie, ee Nyumba ya Israeli? Rudini. Rudini. Rudini. NInayo mipango mizuri sana katika hifadhi kwa ajili yenu, kuongoza na kutawala kutoka Yerusalemu mji [ambao] mara moja ulikuwa mtakatifu. NItakuja na kuwasaidia, kusafisha kwa kuondoa waasi, wafarisayo kutoka kwa nchi kwa mkono WANGU mwenyewe, Aapa BWANA YEHOVAH MUNGU wa Majeshi AnaYEishi milele na milele, ambaYE JINA LAKE ni “NDIYO na AMINA.” Kwa kila nukta na punji, Nasema, “ndiyo na amina.”


Someni Torah yenu, ee Israeli. Je, mnahisi kusadikisha kwa RUAKH HAKODESH? Je, mnahisi moto WANGU ukiwaka, ukichoma ndani ya mifupa yenu? Ni joto la hasira YANGU, la shauku YANGU. Chagueni siku hii MUNGU yupi, ELOHIM yupi mtakayetumikia! Chagueni haraka! Msikawie!


Mtulieni kabla ya mwana wa mwangamizo ainuke. Karibuni NItamdhihirisha, NItamfichua – panya isiyofaa kitu na funza wa kuoza! Msimuamini. Msiangalie katika macho yake. Yeye ni mlaghai, mlaghai wa wanadamu, na mwana hasa wa shetani. Ee Israeli, yeye ndiye funza katika tufaha yenu. Nyinyi ndiye tufaha la jicho LANGU.


Msifanye kile NDIMI NILIYE Hawezifanya. Msipuuze Torah YANGU. Msitupe nje Sheria ZANGU ambazo ni za milele kwa amri YANGU. Ee lakini nyinyi ni WANGU, ee Nyumba ya Israeli, kwa amri ya milele, Asema MUNGU MKUU NDIMI NILIYE. Kwa hivyo NIsikieni siku hii na muogope! Kwa maana Najua mwisho kutoka mwanzo. Tafuteni na mpate rehema kutoka KWANGU siku hii – kupitia JINA na DAMU ya YESHUA HAMASHIAKH, MWANANGU wa pekee. Dhabihu YAKE ni ya milele.


NItahurumia yule ambaye NItahurumia, kwa maana MIMI pekee, MIMI YEHOVAH, pekee YANGU ndiYE HAKIMU na MTEKELEZAJI HUKUMU. Najua moyo wako mwanaNGU, na jinsi unavyojali lakini pia Najua mioyo yao na jinsi hawajali.


Hizi siku za giza, siku za maangamizi, siku za mwanzo wa kile kitakuja zitatikisa wengi. Wengi wataamka lakini wengi zaidi hawataamka. Kama vile katika kitabu cha Ufunuo, wengi watafanya mioyo yao iwe migumu na kutikisa ngumi zao hata katika uso wa MIMI, YEHOVAH, katikati mwa pigo.


Lakini mnaona, MIMI si mwanadamu ili kwamba NIdanganye. Neno LANGU linatimia. Hisia sio fimbo ya ufalme ambayo NInatawala nayo, mwanaNGU. NInatawala na ukweli, neema, huruma, na upendo. Si jambo dogo wakati hukumu ya Ghadhabu YANGU inapooanguka juu ya mtu, kwa maana MIMI ni Mstahimilivu. Inamaanisha huyo mtu ameNIsikitisha kabisa.


Ee wanadamu, je, mnafikiri Napenda kumwaga kisasi juu ya waovu? NIngependa muokoke, muwe wenye kutubu. Lakini NInavyoendelea kusema tena na tena, SItakingama hiari yenu. NDIMI NILIYE halazimishi yeyote kuNIpenda. Ni kitendo cha hiari yako, sadaka ya hiari ambayo NInatafuta, Natamani sana, na kutaka sana.


Mko tu kamili ndani YANGU. NIliumba wanadamu hivyo – kupata ukamilisho ndani YANGU tu. Kwa hivyo sikilizeni dhamira YANGU siku hii na msiNIhuzunishe, msionje Ghadhabu ya MWANAKONDOO na YULE AnaYEketi kwenye Kiti cha Enzi. Kwa maana ingekuwa heri kwenu msingewahi kuwepo.

Hili ni kuhusu nafsi. Hili ni kuhusu kudura. Hilo ndilo kile haya maisha yanahusu. Utaokoa nafsi yako, mwanadamu, au utainajisi na kuipoteza katika banda la nguruwe milele? Hakuna kurudi, watoto WANGU. Farijini BABA yenu, watoto WANGU, kwa maana NDIMI NILIYE Amevunjika moyo. Ingawa NIlijua kile kingetendeka, hilo halifanyi iwe rahisi. Moyo WANGU ni moyo wa upendo. YESHUA Alitoka kwa moyo WANGU ambayo inamaanisha YEYE pia ni upendo. Selah.

Na waliouawa na YEHOVAH watakuwa wengi siku hiyo. Kutoka kwa wingi wa mioyo yao giza linafurika kuteketezanafsi zao. Ee wanadamu, NImewahurumia kwa muda mrefu sana sasa, NIkizuia Hamaki YANGU na Hasira, Ghadhabu na Kiruu CHANGU. Lakini Huruma YANGU imetumika yote siku hii NInapotazama toka upande mmoja wa hii dunia hadi mwingine, toka upande mmoja wa huu ulimwengu hadi mwingine kuona ikiwa Ninawi ilichagua kwa hekima na wakati walioongezewa.


Lakini macho YANGU yanaona utumwa badala ya jubilii – wanadamu wanafanya wanadamu watumwa. Macho YANGU yanaona upotovu mbaya zaidi – kuingilia watoto kimwili na kuwanajisi umeenea kote. Je, SIkuonya dhidi ya hili katika Kitabu cha Enoki?


Upotovu ambao ni chukizo sana hata hauwezi kutajwa. Mnafikiri mnaudhishwa na MIMI sasa, wanadamu? Ngojeni tu hadi NIngurume. NIko tayari kunguruma. Sasa hivi Nazungumza na manabii WANGU katika mnong’ono, katika sauti ndogo tulivu, maneno, na hamwezi hata dhibiti hilo.


Ngojeni tu hadi usemi WANGU uwe mgurumo. Hakuna atakayebaki akisimama. MIMI, YEHOVAH, Naja kuteketeza maadui WANGU. Dunia inatetemeka na kutikisika kwa Uwepo WANGU.


Kwa kila mmoja wa [watoto] WANGU wa kweli kote duniani, ingawa hamwajui kwa jina au uso, NItawafanyia kimiujiza, kuwalinda. Wao pia wako katika kiganja cha Mkono WANGU. Kwa hivyo msiogope, watoto WANGU wapendwa. MIMI, YEHOVAH, Nasema msiogope. Mmeingia katika nyakati za kibibilia, nyakati hususan zilitabiriwa kuhusu kutangaza kuja kwa MWANA wa YAH. Sasa mtaona vita visiohadithiwa kama vile NIliambia huyu nabii anayezungumza. Vita vitazuka na mpingakristo atainuka katikati mwa jivu akijidai kuwa “yule mmoja.”


Yeye ndiye “yule mmoja” sawa! Yule mmoja anayestahili Ghadhabu YANGU, mapigo YANGU, uharibifu WANGU. Lakini msikazie fokasi kwa kile anasema, kwa maana atapumbaza akili za wale ambao watampokea na kumuamini. Lakini mradi unaNIpokea na kuNIamini MIMI, NDIMI NILIYE MKUU, EL ELYON, hautadanganyika. Nawapa nguvu na uwezo mpya wa akili ili mweze kufanya kazi NInavyowataka kufanya.


Kwa hivyo msiwe na hofu, songeni tu karibu KWAKE (YESHUA), karibu na MIMI, YEHOVAH, na karibu na MIMI, MAMA yenu SHKHINYAH GLORIA.


NIpeni kitu cha kufanya nacho kazi, watoto WANGU (kuhusu maandalizi ya siku tatu za giza). NItakutana nanyi nusu ya njia nahalafu kubariki kwa zaidi na kwa wingi, kumwaga baraka YANGU ya kuzidisha ambayohamtaweza kudhibiti kwa ajili ya huruma na wema wa BWANA. Kwa hivyo NIbarikini siku hii, watoto WANGU na mtii. Nataka kuwaona mkiNIbariki na mchukulie hizi siku za giza kwa uzito. Utaratibu! Pangeni!


Mwisho wa Neno.

2 views

Recent Posts

See All
bottom of page