top of page

Unabii 67 “Acheni MIMI, YESHUA, NIwe Nguvu Zenu!”

Updated: Apr 13


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 22 Machi, 2019


Maandiko Husika


Yohana 14:11-14

11 NIsadiki MIMI kwamba NIko ndani ya BABA na BABA yuko

ndani YANGU, la sivyo, NIaminini kwa sababu ya zile kazi NIzitendazo.

12 Amin, amin Nawaambia, yeyote aNIaminiye MIMI,

kazi NIzifanyazo yeye atazifanya, naam na kubwa kuliko

hizi atazifanya, kwa sababu MIMI NInakwenda kwa BABA.

13 Nanyi mkiomba lolote kwa JINA LANGU, hilo NItalifanya,

ili BABA Apate kutukuzwa katika MWANA.

14 Kama mkiNIomba lolote kwa JINA LANGU NItalifanya.Zaburi 28:7

YEHOVAH ni nguvu zangu na ngao yangu,

moyo wangu umeMtumaini YEYE, nami nimesaidiwa.

Kwa hivyo moyo wangu unarukaruka kwa furaha

nami nitaMsifu kwa wimbo.Ujumbe wa Kinabii


Acheni NIwe nguvu zenu – MIMI, YESHUA – kwa maana Naweza sana kuwabeba, kuwainua juu na mkono WANGU wenye nguvu wa ukombozi, wa wokovu, wa ukweli, wa amani, wa urejesho. Selah. Najua kasoro na udhaifu wenu. NIlikuja kuwa KUHANI MKUU kwa MUNGU WANGU BABA ALIYE HAI. NIna rehema na huruma, maana MIMI pia NIliishi katika mwili na NIkapitia huo udhaifu uliopo na hata hivyo kutojua dhambi (Waebrania 4:15). SIkuwahi tenda dhambi (1 Petro 2:22). MIMI ni mtakatifu. MIMI ni ukweli. NIko nanyi sasa na milele zaidi. Ona NIlivyo MUNGU wa upendo?


Hivi ni vita vya kiroho. Silaha za vita vyenu si za kimwili – sio za kula na kunywa – bali kiroho, za ROHO na DAMU YANGU kupitia JINA LANGU (2 Wakorintho 10:3-5).


Wana na binti WANGU waliodhihirika wameitwa kufanya mengi zaidi kuliko kutupa chini na kupindua milima katika JINA LANGU YESHUA (Yohana 14:11-14). Nyinyi nyote mmepewa ufunguo, ufunguo wa imani, wa Daudi, wa Ezra kubomoa sayari na kupindua ustaarabu nzima kamwe kutosikikwa tena. Wamepunguzwa kuwa jivu, kuwa vumbi – hamtapata makazi yao, naam hata milki zao tena – chukizo sana, ovu sana, zimetiwa najisi sana katika kila kitu (Zaburi 37:10).


Natabiri kifo juu ya haya mataifa ya dhambi na miili geni. Tokeni miongoni mwao watu WANGU, Bi-Arusi WANGU (Isaya 52:11, Ufunuo 18:4). Wakati wa kuvuna, wa mundu na upanga u karibu. Ah jinsi Navyolia na kuomboleza! Kwa wale ambao wameteuliwa kwa njaa, kwa njaa na kukata tamaa wataenda NInapolaza miili yao katika kaburi iliwe na mabuu na funza. MUNGU hadhihakiwi! Vuneni kile mmepanda kizuri au kibaya.


Sasa ndio wakati na msimu wa toba (2 Wakorintho 6:2). Msiukose! Ee dunia, msiukose, maana karibuni kisima kitafunikwa, kswitafunikwa na jiwe nene, zito, sio jiwe sahili la kisima. Kwa ajili ya ugumu wa mioyo yenu NItafanya hili, hili litadhihirika. Wote huvuna kile wanapanda, maana MUNGU si wa kuheshimu hadhi ya watu. Selah.


Sasa fikirieni juu ya haya watoto WANGU. Furahieni katika upendo WANGU na halafu mNIshukuru kwa kutowateua kwa upanga wa uharibifu au vazi la njaa nene na zito sana, [la] kusonga pumzi. Badala yake MIMI, YESHUA, Nawavisha na mavazi ya sifa, urithi wa BABA YANGU. Usiku huu Nawavisha mavazi ya kipekee na sahili ya sifa. Paazieni sauti ELOHIM na mpeane UTUKUFU kwa MUUMBA wa Mbingu na Dunia – ambaYE pumzi YAKE inapaswa kusifiwa kwa maana kupitia hiyo mnapewa NENO la MUNGU kwa msukumo wa ROHO MTAKATIFU! HALLELUYAH mara saba! Ee NIpeni UTUKUFU, kwa maana mtaona MFALME juu na Ameinuliwa – hiki kizazi cha Isaya (Isaya 6).


MBARIKIWA ni MUNGU MUUMBA wangu, MFALME na BWANA wa kila kitu! Inameni mbele ya kiti CHAKE cha enzi katika uchaji. Semeni sifa za juu za MFLAME- YULE ambaYE Alikuwa, yuko na Atakuja! HALLELUYAH!!! (Nilisikia ndimi takatifu za mbinguni)


Kwa hivyo watoto WANGU, NIabuduni siku hii. NIpeni UTUKUFU na uchaji. NItakutana nanyi, kila mmoja wenu, katika njia hamjui. Kuweni tu macho na tayari kwa kuzuriwa kwenu na ukweli na urudishaji nguvuza ujana. Namwaga juu ya kila mmoja wenu na katika kila mmoja wenu maji ya chemichemi kutoka kwa gudulia LANGU la fedha.


[Niliona maono ya YESHUA Akisimama na Alikuwa na gudulia la fedha katika mkono WAKE wa kulia ambalo lilikuwa na maji ya uzima ndani yake na Alikuwa Anaenda kuyamwaga juu ya kila mmoja wetu, kila mmoja kulingana na gawo lake.]


Natan’El: Ninapokea hili gawo la maji ya uzima katika JINA LAKO TAKATIFU YESHUA. Asante!


Naam. Mnanona, watoto WANGU, MIMI NIko kwa ajili yenu katika ukame, katika wakati wa kuzuriwa. Nawaonyesha tu kwa kiwango gani mnahitaji kuNItegemea. Nawapeleka kwenye bonde la kivuli cha mauti lakini SIwaachi huko, maana si fimbo YANGU na mkongojo WANGU vinawafariji? Naam, NDIMI NILIYE yuko nanyi hata hadi mwisho wa nyakati. Hakuna chochote kinachoweza watenganisha na upendo WANGU, ila muiruhusu – sio bonde na vina vyake au mlima na vimo vyake, sio roho ya mauti au kimbunga cha uovu (Warumi 8:35-39). Hakuna chochote kinaweza watenganisha na MIMI au kuwang’oa kutoka kwa Mkono wa BABA YANGU. Bakini tu watiifu. Kuweni tu katika amani na mujue kwamba NDIMI nguvu zenu, tumaini lenu, kila kitu chenu (Zaburi 28:7). NItawategemeza katika akili yenu, roho yenu, mwili wenu, katika kila hali na katika kila njia. Kwa hivyo kaeni karibu na MIMI na mshikilie kwa bidii kwenye upindo wa vazi LANGU.


Ee Bi-Arusi WANGU, wewe ni mrembo KWANGU (Wimbo 4:7). NInaangazia macho urembo wako katika kustahi, NIkijua ROHO WANGU Anakaa ndani yenu. Shamiri, Bi-Arusi WANGU, kwa maana NIko nawe. SItaruhusu madhara yoyote yakujie, maana umetiwa mhuri. Umefunganishwa na mhurikwenye kifua CHANGU, kwenye uzimaWANGU, kwenyeMwili WANGU ndani ya DAMU na JINA LANGU ambalo ni YESHUA MASHIAKH wenu na BWANA ARUSI Ajaye karibuni.


Mwisho wa Neno.

8 views

Recent Posts

See All

Comments


Commenting has been turned off.
bottom of page