Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 26 Januari, 2020
Maandiko Husika
Ufunuo 22:12
Tazama, Naja upesi! Thawabu YANGU i pamoja naMI,
kumpa kila mtu sawasawa na alivyotenda.
Wagalatia 6:7-9
7 Msidanganyike, MUNGU hadhihakiwi. Kwa kuwa
kile apandacho mtu ndicho atakachovuna.
8 Apandaye kwa mwili, katika mwili wake atavuna
uharibifu,lakini yeye apandaye katika ROHO, katika ROHO atavuna uzima wa milele.
9 Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa
tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.
Ujumbe wa Kinabii
Ee watoto WANGU, jinsi mnavyoNIpendeza! Mking’aa kwa ung’avu kama nyota ya wakati wa usiku na hata vikuu zaidi (Danieli 12:3). Kwa maana mnaona ya kimwili katika anga ya wakati wa usiku lakini Naona ya kiroho. Na mnang’aa toka upande mmoja hadi mwingine kote katika zama zote. Hamuijui bado lakini wakati NItawaambia mje hapa juu, kukaa kando YANGU, mtaona NInavyoona na mtajua MPENZI wenu MMOJA wa KWELI Amewalinda hii miaka yote – MWANANGU YESHUA, Mkono WANGU wa Kulia, Mkono WANGU wa Kulia ambao si wa mwili, si [wa] najisi, si [wa] dhambi. Kwa maana Neno LANGU ni aminifu na kweli. Ilivyokuwa mwanzoni, ndivyo ilivyo sasa na milele itakuwa. YULE AliYEkuwa, yuko, na Atakuwa (Ufunuo 1:8). Sujuduni na mpe YEYE UTUKUFU (Wafilipe 2:9-11).
Naam, NInenee, mwanaNGU. NIngurumie [kwa ajiliya MUNGU]. Ghadhabika kwa ajili YANGU. Sauti ya kipekee na kweli kama mlivyo kila mmoja wenu. Kila mmoja wenu ushuhuda wa kipekee, radi ya kipekee, sauti ya kipekee, maji ya kipekee. Lakini yote yameunganishwa pamoja ndani YANGU MIMI, YEHOVAH. Kwa UTUKUFU WANGU.
Msiruhusu vikengeusha fikira toka sasa kwenda mbele. Lakini kazeni mwendo kuelekea alama ya juu ya mwito wa Bi-Arusi Mkuu wa UTUKUFU. Kwa maana hakuna lolote linaloweza kuwashinda, watoto WANGU, ila mliruhusu. Kwa maana NIko nanyi (Waebrania 13:5). Tu msigeuze mwangazo wa macho yenu kutoka KWANGU. Sikuzote kazieni macho Maji ya Uzima ambamo riziki yenu inatiririka kutoka. Na NItawalinda katika hii zama kama vile NImewalinda katika zama zote na katika zama zote zijazo. MIMI ni tuzo lenu ang’avu ling’aalo (Mwanzo 15:1)!
Kuweni sahili. Kuweni sahili ndani YANGU. Msiruhusu vikengeusha fikira. Zima mwili na mtaona jinsi mambo yatakvyotiririka kwa wororo na ulaini. Fuateni mfano wa BABA yenu EZRA, kwa maana YEYE hufanya vitu sawa katika macho YANGU. Anabaki sahili. Anabaki chini na Haruhusu mwili WAKE, kiburi CHAKE kuinuka. Sikuzote Anakaa ndani YANGU, kifua cha UTUKUFU. Kwa hivyo jifunzeni hili somo vizuri, watoto WANGU, kabla ya wakati wa vita, wakati wa ole kuja. Kwa maana je SIkusema kuwa mnafaa kuomba kwamba kukimbia kwenu kusiwe katika Sabato wala katika majira ya baridi? Mkamato chungu, baridi, katili wa majira ya baridi (Mathayo 24:20-22).
Yaani, jifunzeni vizuri sasa wakati nyakati ni rahisi. Wakati shetani hapumui chini kwenye shingo zenu [anawafukuza]. Ni kweli anawatesa sasa. Na ni kweli lazima mwe macho. Wakati wa ole bado haujaanza. Mataifa yataghadhibika. Mataifa yatatetemeka. Mataifa hayatakuwa imara kila mahali kwa ajili ya kutoNItumainia MIMI wakati NIkiwalazimisha kunywa Kikombe cha Mkono WANGU wa Kulia wa ghadhabu, kiruu, na hasira (Yeremia 25:15-17, Zaburi 75:8). Tuzo kwa ajili ya ufidhuli wao, kwa ajili ya uasi wao, kwa ajili ya uhaini wao dhidi YANGU.
Hata wewe, ee Israeli, unathubutuje! Mkitoa vijisababu vya kutoNIaminia MIMI na MWANANGU YESHUA MASIA wa Israeli. Unathubutuje! Aibu kwako! Kwa maana NImeaminisha ndani yako kile SIjaaminisha mataifa mengine. Kwa maana Torah ilianza na wewe. Na umefanya nini? Naam, unanakili kwa uaminifu lakini unakosa kuelewa. Unanakili kila nukta na chembe lakini unakosa upendo WANGU. Unakosa MWANANGU. Toa pazia machoni mwako na uone katika njia mpya siku hii. Msifanye mioyo yenu migumu kama katika siku ya uchokozi, kama katika ile siku ya ukufuru mkubwa (Zaburi 95:7-11).
Nawakujia, Nawakujia watoto WANGU, kwa hivyo jitayarisheni (Mathayo 24:44). Kuweni tayari. BWANA ARUSI Yuaja Akiwa Amevalia nyeupe. Na mtakuwa tayari mradi mtii, mradi mNItumainie. Kwa hivyo msiyatoe macho yenu kutoka KWANGU. Tazameni juu, ukombozi wenu unasongea karibu, uko hata katika anga ya mashariki (Luka 21:28). Kwa hivyo msipoteze tumaini. Msiruhusu aibu ifunike uso wenu. Lakini ghadhabikeni kwa ajili YANGU [kuonyesha ghadhabu ya MUNGU dhidi ya dhambi]. Neneni hukumu ZANGU kweli. NInaziteremsha katika roho zenu.
Sasa NIzungumzieni. Ambieni shetani asimame kando. Ambieni hii dunia MWANANGU Yuaja (Ufunuo 22:12). Ambieni wale wana masikio kusikia na macho kuona, [walio] na hatua sawa kuja upande WANGU, kuja upande wa Moshe (Kutoka 32:25-28). Kwa maana upanga utachomolewa. Wale walio kusudiwa upanga, kwa upanga wataenda. Kwa tauni, kwa tauni wataenda (Yeremia 15:1-3). Huu ni wakati wa ole kuu, wa dhiki kuu ya mataifa, kutikisa kwa misingi. Kile ambacho kinaweza tikisika kitatikiswa.
Lakini wapi tunda lenu, watoto WANGU? Je liko naMI? Liko ndani YANGU? Je mnakaa katika TAWI? Haya ndiyo maswali NInayo kwenu siku hii. Kwa hivyo hadharini. Angalieni hatua zenu. Huu sio wakati wa kufanya michezo, maana nyakati kuu za vita zinakuja karibu juu yenu. Tazameni China. Inavuna kisasi CHANGU. Inavuna kile wamepanda kwa kuNIdhihaki hadi kwa uso WANGU (Wagalatia 6:7-9).
Hakuna hata neno LANGU litaanguka ardhini bila kuzaa matunda lakini litatimiza yote NInalituma kuenda kufanya (Isaya 55:10-11). Kwa hivyo lainikeni watoto WANGU na mtazame maadui wakianguka mmoja baada ya mmoja kama dhumna. Kwa maana wakati adui, wakati kiongozi wa kundi la adui anapogongwa wote wanakimbia huku na huku. Lakini sio nyinyi watoto WANGU. Sio nyinyi kundi LANGU dogo la kondoo, kundi LANGU dogo la thamani (Luka 12:32). Kaeni tu chini ya mabawa YANGU.
Msiasi. Msiwe na wasiwasi. Msihuzunike. Lakini kaeni ndani YANGU na yote yatakuwa sawa. Kwa hivyo kaeni ndani YANGU siku hii watoto WANGU. Kwa hivyo nendeni kwa amani. Amani YANGU ambayo inapita amani ya zama. Amani YANGU inazidi nyakati zote, kwa maana MIMI “NDIMI NILIYE” MKUU SIjafungwa na wakati, na vizuizi vya mwanadamu. MIMI NDIMI NILIYE na huyo ndiye NItakayekuwa (Kutoka 3:14). MnaNIelewa?
Comments