top of page

Unabii 83 “Barua ya Upendo kwa Israeli”

Updated: Jun 29, 2022


Umepewa Nabii Shema’YAH kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 27 Januari, 2020


Maandiko Husika

Ufunuo 12:9-12

9 Lile joka kuu [dragoni] likatupwa chini, yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi au shetani, aupotoshaye ulimwengu wote. Akatupwa chini duniani, yeye pamoja na malaika zake. 10 Kisha nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema: “Sasa wokovu na uweza na Ufalme wa ELOHIM wetu umekuja na mamlaka ya MASIA WAKE. Kwa kuwa ametupwa chini mshtaki wa ndugu zetu, anayewashtaki mbele za ELOHIM usiku na mchana. 11 Nao wakamshinda kwa Damu ya MWANA-KONDOO na kwa Neno la ushuhuda wao. Wala wao hawakuyapenda maisha yao hata kufa. 12 Kwa hiyo, furahini ninyi mbingu na wote wakaao humo! Lakini ole wenu nchi na bahari, kwa maana huyo ibilisi ameshuka kwenu, akiwa amejaa ghadhabu, kwa sababu anajua ya kuwa muda wake ni mfupi!”


Ufunuo 6:16-17

16 Wakaiita milima na miamba wakisema, “Tuangukieni, mkatufiche na uso WAKE YEYE Aketiye kwenye kiti cha enzi, na mkatuepushe na ghadhabu ya MWANA-KONDOO! 17 Kwa maana siku ile kuu ya ghadhabu YAKE imewadia. Je, ni nani awezaye kustahimili?”Mithali 11:18-19; 30-31

18 Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu, bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.

19 Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima, bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake.

30 Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima, naye mwenye hekima huvuta roho za watu.

31 Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani, si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?


Mathayo 23:37-39

37 “Ee Yerushalayim, Yerushalayim, uwauaye manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi NImetamani kuwakusanya watoto wako pamoja, kama vile kuku akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka! 38 Tazama nyumba yenu imeachwa ukiwa. 39 Kwa maana Nawaambia, hamtaNIona tena tangu sasa mpaka mtakaposema, ‘Amebarikiwa YEYE Ajaye kwa JINA la YEHOVAH!’ ”

(Maoni Muhimu: YEHOVAH Anazungumza na Israeli yote, Israeli ya kimwili na kiroho. Hiyo inamaanisha, hili neno pia linaelekezwa kwa Wakristo.)

Ujumbe wa Kinabii


Ndiyo, hiyo ni sahihi mwanaNGU mpendwa. Asante kwa kuNIruhusu. Wakati umekuja Ee Dunia!


(Nabii Shema’YAH: Na Ananikumbusha kuwa kitu kingine nilisikia ilikuwa ni tamko hili “nafasi na wakati”.)


Huu ndio wakati! Hili silo neno LANGU kwako ee Dunia: ‘kwamba unaweza fanya dhambi na kukanyangia chini damu ya MWANANGU ambayo imetolewa kwa ajili yenu.’


NIruhusu NIzungumze katika hizi nyakati za mwisho watoto WANGU! [Kwa] Hii dunia, kwa waasi, ili wasikie na wajue kuwa SIfanyi mzaha! Kwa maana kuna hukumu kali kwa dhambi! Ni dhambi na mauti. Kwa maana malipo ni mauti na wote watalipa hiyo gharama njia moja au nyingine (Mithali 11:18-19; 30-31; Warumi 1:28-32; 6:23). Sasa ewe Ee Dunia, MWANANGU Amewalipia gharama. Gharama ya mauti ili mwe huru... wekwe huru, [na] kupata REHEMA kutoka KWANGU, msamaha, na neema. Au mnaweza lipa gharama, au mnaweza lipia gharama ya dhambi yenu!


Najaza midomo yenu kila mmoja wenu na ukweli WANGU, kunena na dunia. MsiNIsikitishe watoto WANGU! Kuweni na akili timamu kama BABA yenu. Na nyote mnafanya kazi nzuri! Kazieni mbele! Kwa maana Nawakazia mbele katika kichaka cha dhamira YANGU! Kama yule mwanakondoo wa kuchinjwa! Kuchinja kwa mwili (Ufunuo 22:8-13; Yashari 23:70). Nawatia nyote mafuta kuitenda kazi. NIpeni kila chenuchote, mizigo yenu yote! Pumzi yenu yote, kwa maana yote ni YANGU! Wekeni yote chini. Jinsi nyote mlivyo wa thamani KWANGU. Almasi, vito, na johari ZANGU (Kutoka 19:5-6)! Milele mtakuwa naMI! Na NItakuwa nanyi. Kazi ipo karibu kumalizika na MWANANGU Atakuja Awanyakue ninyi nyote.


Kazieni mwendo watoto WANGU! Kwa maana ghadhabu kali ya BABA YANGU imekuja kwa hii dunia (Ufunuo 6:16-17). Ee hii dunia haijui na kwa hakika itashangaa, kwa hakika itaudhika. Kwa maana mshipi wa ghadhabu YANGU umekuja juu ya wasiotii ambao hawaNIkiri, ambao hawaNItazami, wala mapenzi YANGU, wala kuja KWANGU (Zaburi 79:6-7; 110:6)! Kwa hivyo kama mwivi usiku, NItanyakua watoto WANGU waaminifu! Na kuacha walio salia katika giza la nje. Kusaga meno yao ndiyo mtakayoona ee watu wa hii dunia. Je, hilo ndilo mnalotaka?! Badala ya mikono YANGU ya upendo (Mathayo 24:42-51)? Ni mapepo mnayotafuta?


Kisasi kikali, ulipizaji kisasi juu ya watu wa shetani (au “kisasi cha shetani juu ya watu” ELOHIM Anasema). “Kwa maana shetani amekuja chini kwenu ee dunia!”, karibuni NItasema (Ufunuo 12:9-12). Je, ni hili mnalotafuta? Au mngependelea mwe huru (kutokana) na utumwa? Utumwa wa uovu ambao MWANANGU Aliwaweka huru kutokana nao, ikiwa tu mtaamini na kuukubali!


Jinsi mnavyoNIdhihaki MIMI! Nyinyi wakanamungu mnaNIdhihaki! Hamjui kile NImewafanyia. Lakini ni juu yenu kutafuta. Na sio kunyoshea kidole na kutoa vijisababu. Hukumu YANGU ya haki! Mko sahihi, hukumu YANGU ya haki itawateketeza NInapoongea (Warumi 2:5-11)! Mwanadamu mfidhuli, duni! Nakulilia na kukuombolezea! Nakuombolezea! NIlikulilia katika bustani ya Gethsemani! NIlikulilia! Ili nafsi yako NIweze kuifikia. Ili nafsi yako NIweze kuifikia na ukweli WANGU, na uhuru WANGU tukufu (Luka 22:39-44). Na upendo WANGU! NIlikukujia katika umbo nyingi, lakini haujasikia. Lakini haujasikia.


Kwa maana unanyosha kidole lakini sio [kuelekea] KWANGU! YULE Anayewasamehe dhambi zenu zote! Kuziondoa zote! Hiyo ndiyo zawadi NIliyowapa. Lakini mnaNIkataa kwa dharau lakini SIkushika hilodhidi yako maana ulikuwa mtoto mdogo, lakini hamkuNIsikiza NIkizungumza. Ni mara ngapi NImekuja kwako Yakobo!? Kwa maana SItarudi tena kwako hadi NIsikie, “Mbarikiwa ni YEYE Ajaye katika JINA la YEHOVAH (MAJINA ya YEHOVAH na YESHUA)!” Hadi NIsikie kutoka kwenu, “NIOKOE YESHUA!” (Mathayo 23:37-39).


NItumainie MIMI MWANANGU YAKOBO! NIlikuzaa! Na NIkakubeba kwenye mabawa ya tai (Kumbumbu 32:9-12). Bado unaNIkataa kwa dharau. Ni mara ngapi lazima NIkulilie, NIkuombolezee? NItafute na utapata (Kumb. 4:29). Lakini sasa, Naficha macho YANGU kutoka kwako. Haijalishi aina ya uovu, haijalishi namna ya uovu ambao utakuja juu yako, dhidi yako (Kumb. 31:16-18). Na watu wako ambao wanapaswa kuwa watu WANGU, kwa maana ni watu wako ikiwa wataenda njia ya mwili. Lakini nyinyi ni watu WANGU ikiwa mtaenda njia ya roho. Kwa maana BABA Anatamani kama wale wanaoabudu katika roho na ukweli (Yohana 4:23). SIfanyi mzaha nanyi Israeli! Huu ndio wakati wa mwisho kama ilivyoandikwa katika Kitabu. Imeandikwa katika Kitabu yote yatakayofanywa, yote yatakayokuja. NImewaonya kutoka kitambo. Musa aliwaonya nyinyi nyote. Moshe aliwaonya nyinyi nyote (Kumb 31:24-27)! Haijalishi mara ngapi mnachana na kurarua kutoka kwa Neno LANGU! Hili Andiko, hilo Andiko; badala ya kupokea ushauriwote wa sheria YANGU ambao waelekeza kwa YESHUA, msaidizi wenu.


Je, si mnataka usaidizi? Je, si mnasema, “Ee ADONAI, SIADIA, TAFADHALI SAIDIA?” Kwa hivyo Naja kuwasaidia kama BABA Aliye na upendo kwenye goti lililoinama kuMuinua MWANANGU, MTOTO WANGU. Nakimbia [kuja] kukusaidia (Zaburi 121:2-4). Naja kuwasaidia, lakini mnakataa usaidizi WANGU kwa dharau. Mara nyingi kote [katika] vipindi, mwokozi baada ya mwokozi Natuma. Mnajua hilo fumbo ni kwa ajili yenu ee Israeli? Natuma mtumishi baada ya mtumishi, nabii baada ya nabii, mwokozi baada ya mwokozi, na [halafu] Nasema, “Ee, NItatuma MWANANGU!” Na mnasema, “Yuko hapa. Mrithi wa vitu vyote. Acha tuMuue na tuchukue urithi! Acha tuMuue! Acha tuue huyu Yesu.” Ee Najua hawa watu hawajui JINA LANGU la Kweli lakini Nawatumia kueneza nuru ya Ukweli WANGU – Neno LANGU, YESHUA, kwenu! Lakini katika hizi nyakati za mwisho, Natumia 14 WANGU–na halafu kwa hakika METATRON WANGU – kuwaletea ukweli. Maji ya Uzima, kuyachota kutoka kwa kisima. Kile mnachohitaji sana kukata kiu chenu katika nchi kavu na iliyokauka. Ee kazi YANGU itakamilika, ee mpingakristo! Na hauwezi ikomesha! Kwa hakika hakuna chochote unachodhibiti (ELOHIM Azungumzia mpingakristo). Nyota zote zimo katika udhibiti WANGU! Mbingu zote zinaNIinamia! NInazishika katika mkono WANGU wa kulia na kuzifunika na [mkono] WANGU wa kushoto, METATRON WANGU. Kutoka hapa kuenda mbele, itakuwa ngumu kwako ewe ee dunia.


Ungana naMI watoto WANGU! Nawaimbia! Naimba juu yenu wimbo wa furaha, wa wokovu (Sefania 3:17, Zaburi 32:7)! Naimba nanyi watoto WANGU. Imbeni juu ya mataifa. Imbeni naMI! Naimba juu ya mataifa! Na mfahamu mapenzi YANGU kwa ajili ya maisha yenu; na urahisi wa injili na Wokovu. Upendo wa Bi-Arusi ambao NImewapa kwa wale ambao wanafukuzia, toa mwili dhabihu. Isalimishe yote kwa maana itakuja, wakati wa kuwatuma nyote nje. Kuimbia mataifa, kunena na mataifa. NImeweka mwili wenu chini ya kidole gumba CHANGU na NItauzuia chini kwa ajili yenu. NItumainie MIMI kipenzi CHANGU. Vitu vyote vitakuwa rahisi unapoachilia dhamira yako KWANGU, unapolaza kila kitu chini kwa ajili YANGU. Kwa maana hiyo ndiyo huu mfanyiko tendani. Hiyo ndiyo maana mnatafuta kukombolewa na MIMI. NIruhusu NIzungumze na moyo wenu na nafsi yenu. Tumaini YOTE ndani YANGU. Wekeni tumaini lenu LOTE ndani YANGU. Wekeni KILA kitu katika mikono YANGU. Nabeba mizigo yenu maana lazima tu muamini kwamba mmesamehewa. NInaposema, “umesamehewa.” MIMI ni JAJI wa HAKI na lazima NIsamehe unapokuja KWANGU.


Kwa hivyo NIruhusu NIzungumze mwanaNGU! NIliweka nguvu ZANGU ndani yako. Hakuna kinachoweza kukutikisa! Napenda unaponena hekima ambayo NInakujaza nayo. Hili linaNIpendeza. Nawe pia muhibu WANGU. Kuwa mwenye jitihada kwa ajili YANGU, na macho yaliyokazia fokasi kwenye MFALME wa wokovu wenu, BWANA wa WOKOVU wenu!


NIko nanyi NYOTE! Kwa maana mtaenda katika maeneo milki ya kiza kabisa mkibeba mwangaza WANGU! Na watajua NImekuja ndani yenu na ujumbe: “TUBU AU MUANGAMIE! Endeni upande mmoja! Kusanyikeni na MASIA! Maana kila kitu kingine kitafagiliwa mbali!” (Mathayo 12:30). Kuna MFALME mmoja kuna MTAWALA mmoja juu ya wote! Wote wanaNItumikia! Mnaweza tumikia hadi kwa UZIMA, au unaweza tumikia hadi kwa MAUTI! NInapowaadhibu nyinyi watu wa hii dunia na MAUTI (Zaburi 110:6, 79:6-7)!


Kwa maana kwa kweli NItawaambia watumishi WANGU, “Leteni wale wote ambao hawakuNItaka MIMI NIwatawale, NIwe na mamlaka juu yao, na mwaue mbele ZANGU!” (Luka 19:27). Kama vile kwa hakika jahanam ipo – itapokea nafsi yako (ELOHIM Azungumza na wasiotii) – Jua hili: MIMI NI JAJI WA HAKI! Napeana zawadi adilifu. Zawadi kwa ajiliya mema, zawadi kwa ajili ya uovu. Unawezafanya mema, ambayo ni tubu na uNItafute MIMI, au unaweza fanya uovu; na iwapo hivyo, enda njia yako (Mithali 11:31; Zaburi 18:24-26; 62:12).


Na jua hili: ni mapenzi YANGU mtubu. Maana NIliwalipia gharama, zawadi YANGU yenye upendo. Jinsi Navyowapenda. Jinsi Navyowapenda (1 Timotheo 2:3-4). Na NIme[i]tangaza kutoka mwisho wa wakati, na sasa hata katika wakati huu, kupitia rafiki YANGU mpendwa (ELOHIM Alitangaza hitaji la kutubu na kuokolewa kutoka mwisho wa wakati). Mashahidi WANGU Wawili. Kwa maana TUnashiriki kila kitu. Na wanapokuja kwako ee Israeli, inamisha magoti yako, ewe mwenye shingo ngumu, usietii. Inamisha magoti yako! Kwa maana SIwatumi hawa (nyota 14 wa YESHUA) bure!


Kwa maana ikiwa hamtapokea, JUA KWA HAKIKA... JUA KWA HAKIKA... MTAPOTEA (ikiwa hamtapokea wajumbe wa ELOHIM, Mashahidi WAKE Wawili)! Milele kabisa! Nyinyi ambao mlipaswa mNIjue... ambao mlipaswa mNIjue milele kabisa, mtapotea katika ndimi za moto za jehanam!


Natoa hili tangazo – hili dai: ikiwa hamtapokea hawa – hawa 14. Upinde WANGU wa mvua wa amani, [&] Moshe WANGU wa Sasa. JUA HILI, mtapotea. KWA HAKIKA. Sikizeni maneno ya Mdomo WANGU! Mtakuwa kwa hakika mmepotea na hakutakuwa na ukombozi kwenu! Kwa maana mtakuwa mmepuuza nafasi ya pekee na ya mwisho kujua mikono YANGU ya upendo, mpapaso WANGU (wa mahaba), mabawa YANGU matakatifu kuwafunika na kuwalinda.


Na hiyo ndiyo maana ee Yerusalemu, Natuma hawa waandishi kwenu na walioelimika katika Torah kunena nanyi. Kwenye kiwango chenu. Kwenye kiwango chenu cha juu! Ee Mfarisayo! Kwenye kiwango chako cha usomi (Mathayo 23:37-39). Kukupatia kile ambacho MIMI huwapa watoto wachanga. Ambacho watoto wachanga hupokea kwa urahisi sana. Maziwa kutoka KWANGU, maziwa ya MIMI. Kwa maana ni ya wanyenyekevu, watoto WANGU wadogo – watoto WANGU wa milele. Unaweza kuwa mmoja [wao] pia ikiwa utakuja KWANGU sasa. SItakufukuza kwa namna yoyote (Yohana 6:37). Lakini lazima uifanye njia YANGU kama vile sikuzote NImekuonya. [NI]mekuambia. [NI]mekuonyesha katika maandiko ambayo unatafuta ndani kwa bidii.


Kwa hivyo NIsikize NIkinena neno LANGU kupitia mwanaNGU ambaye ameingia katika Ufalme kabla yenu (Mathayo 21:28-32). Kwa unyenyekevu wa moyo wake kukiri ukweli: kwamba anahitaji MWOKOZI kama tu nyinyi. NISIKIZE NIKIZUNGUMZA! Shingo ngumu, Israeli yenye shingo ngumu! Kabla NIwaponde na kuwafanya unga! Njoni KWANGU! NIangukieni (Mathayo 21:43-46)! Kwa maana NImeahidi kuwa SItawahi waacha! Lakini mkiNItelekeza sasa, jua hili: NItawatelekeza hadi uangamizaji (2 Nyakati 15:1-4; Malachi 4:6)! Kwa maana ni kama vile ilivyo kwa WOTE wanaotenda dhambi hii, [NItendea] huu ukatili MIMI na MWANANGU AMBAYE Alivuja damu kwa ajili yenu. Ni kweli! Wakristo wanao ukweli. Ndio walipokea ukweli, kwa sababu waliNIpokea MIMI na MWANANGU [YESHUA]. Na hamwezi kwa namna yoyote wahukumu. Kwa maana NInawahukumu nyinyi... na wao! Maana hakuna mapendeleo na BWANA (Warumi 2:1-11). Na wote watatimiza wokovu wao kwa kuogopa na kutetemeka (Wafilipi 2:12). Kwa hivyo NIpendezeni sasa. Inamisheni goti lenu. NIpokeeni. Pokeeni MWANANGU. Pokeeni MWANANGU. Inameni na mNIpokee. Hili litaNIpendeza katika wakati huu. Hakuna MWINGINE. HAKUNA NJIA NYINGINE. Mmesikia NDIMI NILIYE MKUU siku hii. Imenenwa na itaandikiwa nyinyi. Mtafanya nini? Chaguo lipi mtafanya? Ni chaguo lipi mnaweza fanya? Kwa maana hakuna njia nyingine naMI (Yohana 14:6). Na sasa mmeNIsikia NIkizungumza.

Mwisho wa Neno.

2 views

Recent Posts

See All
bottom of page