top of page

Unabii 77 “Usitafute Wapenzi Wengi, Ee Israeli!”

Updated: 4 days ago


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Sehemu ya kwanza ilipokelewa asubuhi mapema 19-7-2019 na sehemu ya pili 5-1-20 asubuhi mapema baada ya kusoma sehemu ya kwanza.


Maandiko Husika



Zaburi 95:8-9


8 Msiifanye mioyo yenu migumu, kama mlivyofanya kule Meriba,

kama mlivyofanya siku ile kule Masa jangwani,

9 Ambapo baba zenu waliNIjaribu na kuNIpima,

ingawa walikuwa wameyaona matendo YANGU.



Kumbukumbu 30:19-20


19 Leo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako,

kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana.

Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi,

20 na ili upate kuMpenda YEHOVAH MUNGU wako, uisikilize sauti YAKE na kuambatana naYE.

Kwa kuwa YEHOVAH ndiYE uzima wako, na Atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi Aliyoapa kuwapa baba zako Abrahamu, Isaka na Yakobo.


Ujumbe wa Kinabii


(19-7-2019) NIruhusu MIMI, YESHUA, kukuzingira na upendo WANGU. NIruhusu NItulize akili yako, kukuosha katika DAMU YANGU iliyomwagika pale Kalivari. Nakujia Bi-Arusi WANGU bila doa na mkweli. (5-1-2020) Nakujia Bi-Arusi WANGU na moto wa uchu katika macho YANGU.


Songeni kando! Simameni kando! Napuliza maadui chini, kwa maana MFALME Anapokuja hakuna kikwazo chochote kinaweza simama njiani MWAKE. MIMI NI MFALME! MIMI NI JAJI na si kwa neno la mwanadamu yeyote NInatangaza (Yohana 5:20-30). NaJIshughulisha na shughuli za BABA YANGU. NaJIshughulisha na Utaratibu wa MFALME.


[YEHOVAH Azungumza] Shughuli YANGU ni YANGU mwenyewe. NInamudu mambo YANGU mwenyewe na kutawala na huruma na ukweli. Nani ndiye wa kumwambia “NDIMI NILIYE” MKUU kile Anaweza fanya au Hawezi?


Ee Israeli, nini kisingizio chenu? Mkono wenu umeingia wapi? Nini mmejiingiza ndani? Kufanyafanya mambo ya mizungu? Ee israeli, NImewaita kwa kuishi safi, kwa mtazamo mmoja, kukaizia fokasi kwenye upendo WANGU kupitia MWANANGU YESHUA. Uasi sio njia (Zaburi 95:8-11). SIvutiwi na uchawi wenu.


[YESHUA Azungumza] NIrudieni MIMI sasa! Rudieni “NDIMI NILIYE” MKUU! Rudieni fadhili za upendo na mtelekeze ugumu wa mioyo yenu. Nawezaondoa lile jiwe. Naweza waweka huru na kuwapa uzima, kwa maana MIMI NDIYE Ufufuo na Uzima (Yohana 11:25-26). MIMI NDIYE UWEZA wa MUNGU uliodhihirishwa. MIMI NDIYE MFINYANZI, nyinyi ndio udongo wa mfinyanzi. NIsikize!


NIsikieni, ee Israeli! NIsikize na muinamishe goti. Inamisheni sikio lenu kwa mlio wa sauti YANGU na muwekwe huru. Kaeni katika utakatifu, katika mwangaza. Tokeni kwa giza. Wekweni huru kutoka kwa minyororo ya uovu wenu. Someni Torah na mkumbuke mara moja tena njia za uadilifu zilizowekwa mbele yenu. NIngependa mchague uzima (Kumbukumbu 30:19-20). Chagueni uzima ndani YANGU.


Ee Israeli, tamanio la moyo WANGU ni mpate kuishi, kuona UTUKUFU WANGU. Je, hamjui kuwa mipango YANGU kwa ajili yenu ni kwa uzuri na sio kwa uovu (Yeremia 29:11)? Je, mlisahau Neno LANGU ambalo NIlinena na Yeremia?


Toeni gogo kutoka kwa jicho lenu (Mathayo 7:1-5). NIgeukieni na moyo mzima. NIgeukieni katika usahili. Ee Israeli, NIliweka mbele zenu mpango WANGU wa Wokovu, Wokovu WANGU wa Zama. Fungueni macho yenu. Nafungua macho yenu kwa Wokovu WANGU. Nawapa dawa ya macho.


Jiosheni na Maji YANGU ya Uzima (Isaya 1:6-17). Fanyweni wazima na Neno LANGU. Je, mnaNIamini ee Israeli? Mnasoma Torah, lakini wapi imani yenu? Wapi imani yenu (Warumi 10:5-13)? Nawakaripia kwa sababu mnawajibishwa zaidi kuliko yale mataifa mengine. Kwa nani uaguzi wa MUNGU ulitumainiwa, ila kwako, ee Israeli.


Mnatafuta, mnapekua Maandiko tena na tena na tena kwa ajili ya Wokovu lakini mnakana JINA LANGU TAKATIFU. Ee Israeli, iteni juu ya JINA LANGU na msiabike. Wokovu hauji na mwingine ila MIMI, YESHUA. NIkose MIMI na mkose BABA, kwa maana hakuna awezaye kuja kwa BABA ila kupitia MIMI, YESHUA (Yohana 14:6).


Mwisho wa Neno.

10 views

Recent Posts

See All

Commenti


I commenti sono stati disattivati.
bottom of page