top of page

Unabii 63 "NItafuteni MIMI, YEHOVAH, Wakati NIngali Nawezapatikana!"

Updated: Apr 10


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 20 Machi, 2019


Maandiko Husika


Kutoka 15:11

“Ni nani miongoni mwa miungu aliye kama WEWE, Ee YEHOVAH?

Ni nani kama WEWE: Uliyetukuka katika utakatifu,

Utishaye katika utukufu, Ukitenda maajabu?


Isaya 55:6-7

6 Mtafuteni YEHOVAH Akingali Anapatikana;

Mwiteni Akingali karibu.

7 Mtu mwovu na aiache njia yake, na mtu mbaya

na ayaache mawazo yake. Yeye na amrudie YEHOVAH,

naYE Atamrehemu, arudi kwa MUNGU wetu,

kwa kuwa Atamsamehe bure kabisa.


Yeremia 29:13

MtaNItafuta na kuNIpata. MtakapoNItafuta kwa moyo wenu wote


Ujumbe wa KinabiiAndika, Nasema, andika, kwa maana kisasi cha kiruu cha ALIYE JUU KABISA kimekuja katika Uso WANGU! NItatekeleza Maneno ya MFALME MKUU – Mbarikiwa ni YEYE milele – na kutangaza kisasi cha ELOHIM ADONAI wa Majeshi (Isaya 61:2)!


Ni nani aliye kama YEYE, enyi mataifa (Kutoka 15:11)?! Tangazeni ni miungu yenu ipi ambayo ina mkono wenye nguvu kuokoa, mkuu katika mapigano, mkuu katika vita, nguvu katika bonde, katika vina, ukuu na fahari katika vilele. Hakuna aliye kama YEYE ambaye anavurugavuruga vina, akivifanya kutapika falme za majini, akivichokoza katika ukuu na kiruu cha ajabu... maonyesho ya kisasi CHAKE cha KIFALME. Vile mtu huacha simba na windo wake, bila kuingilia, vivyo hivyo pia acha MFALME kwa Shughuli YAKE.


Usijiingize katika vita vya biashara na wala usiwe kinyaa na waa machoni MWAKE, kwa maana karibuni MFALME AtaJIamsha dhidi ya sio tu taifa moja, nusu moja ya dunia, lakini dunia nzima; naam hata mbele ya mbingu hadi kwa mpanuko wa ulimwengu dhidi ya wale wote wanaotangaza umoja lakini kwa hakika wanatafuta uasi dhidi ya ALIYE JUU KABISA katika kutupilia mbali Amri ZAKE (Zaburi 2).


Msiwe wajasiri katika kiburi, mkiwa na sura ya kinafiki ya unyenyekevu. Lakini tubuni na kwa kweli muwe wanyenyekevu. Karibuni MIMI, YEHOVAH, SItapatikana, SItafanya NIjulikane lakini NItajificha katika giza nene (Isaya 55:6-7). Ee jihadharini dunia wakati NInaficha Uso WANGU, kwa maana wakati huo ndipo kiruu itaachiliwa katika pande saba tofauti.


Lakini NInafunika watoto WANGU na upendo (Zaburi 91:4). Hakuna chochote, hakuna chochote, hakuna chochote kinaweza wajiri ila MIMI, YEHOVAH, MUNGU wenu NIkiruhusu. Kwa hivyo furahieni ndani YANGU siku hii. Usiache amani yako. Usiache furaha yako. Usitoe sadaka kile SIjekuambia utoe sadaka. Kuweni wapole na wa hali ya chini, kwa maana mko karibu kuirithi dunia, kurithi [utawala] WANGU wa milele. Bakini tu wanyenyekevu. Tafuteni na kila kitu mko nacho (Yeremia 29:13). Fanyeni kila siku iwe na matokeo ya maana. Karibuni usiku utaingia, kionjo cha jahanam kwa wale ambao imeteuliwa, na hakuna kazi itatimizika (Yohana 9:4).


Mtabidi kutafuta njia mpya za kutimiza vitu. NItawapa uvumbuzi cheshi, maazimio ambayo yatatikisa hii dunia kwa ajili ya UTUKUFU WANGU (Mithali 8:12). Wengine wataamka, wengi hawataamka, lakini wote wataonywa, kwa maana hizi ni nyakati za mwisho... mwisho wa dhambi na mwanzo wa UTAWALA WANGU wa KITUKUFU duniani – Ufalme wa kimilenia – utawala wa utakatifu na bila kipimo. Je mnaNIsikia, watoto WANGU? Bila kipimo. Bila kipimo.


Mwisho wa Neno.

5 views

Recent Posts

See All

Σχόλια


Ο σχολιασμός έχει απενεργοποιηθεί.
bottom of page