Unabii 19“MIMI YAHUVEH Nasema, ‘Ikiwa Mnakataa Sheria ZANGU, MnaNIkataa MIMI!’”
Umepewa Nabii D’vorah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 14 Februari, 2019
Maandiko Husika
Mathayo 5:17-19 “Msidhani kwamba NImekuja kufuta Sheria au Manabii; Sikuja kuondoa bali kutimiza. Kwa maana, amin Nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yoyote kutoka kwenye Sheria, mpaka kila kitu kiwe kimetimia. Kwa hiyo, yeyote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, lakini yeyote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme wa Mbinguni.
Mathayo 19:16-21 “Mtu mmoja akamjia YAHUSHUA na kuMuuliza, “MWALIMU Mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?” YAHUSHUA Akamjibu, “Mbona unaNIuliza habari ya mema? Aliye mwema ni MMOJA tu. Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.” Yule mtu akaMuuliza, “Amri zipi?” YAHUSHUA Akamjibu, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama nafsi yako.” Yule kijana akasema, “Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?” YAHUSHUA Akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze vitu vyote ulivyo navyo, na hizo fedha uwapemaskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, uNIfuate.”
Warumi 10:9 “Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba “YAHUSHUA ni BWANA,” na kuamini moyoni mwako kwamba MUNGU AliMfufua kutoka kwa wafu, utaokoka.”