top of page

Unabii 49 “Someni Bibilia YANGU, Sio Studio ya Marvel!”


Umepewa Nabii Hannah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 21 Mei, 2019


Ujumbe wa Kinabii


Wakati wa kuabudu usiku, niliangalia pote na nikasikia YEHOVAH MUNGU Akizungumza.


“Huu ndio usharika WANGU wa kweli uliojawa na upendo, wenye moyo mmoja na nia moja. NIlisema NItakujia Bi-Arusi Mtakato, na nyinyi ni Bi-Arusi WANGU Mtakato wa Milenia ambaye karibuni atakuwa Bibi wa YESHUA WANGU. Nataka Mataifa yote yajue hili, kwa hivyo tafsirini huu unabii na unabii nyingine yote kuanzia sasa. Kwa maana hilo litavuta nafsi ndani, na watafsiri zaidi wataletwa ndani. Kwa hivyo fanyeni kile Nasema, na fanyeni kile Nafanya, WANGU wa ubani, watoto WANGU wa moyo WANGU. Kile mmeona, ndicho kile kwa kweli kitatendeka hivi karibuni.


Nabadilisha vitu sio kama vile wanadamu hufikiria, na hizi siri bado SIjawaambia, sio sasa, sio wakati huu kwa maana akili zenu hata haziwezi fahamu. Kwa hivyo msiwaze kupindukia kuhusu hili jambo, jueni tu NImeita wengine wenu *wasafiri wakati wa kusudi ZANGU mwenyewe. (*Wasafiri wakati – wale wanaoweza safiri katika wakati uliopita na wakati ujao)


Ulimwengu ZANGU nyota zingine zimekuwa zinaNIasi. Sasa wanakutana na Galaktas. Msifikiri kwamba hao wahusika kutoka vibonzo (komik) vya Marvel ni ubunifu tu wa mwanadamu. Kwa maana sio tu dhana bunilizi. Ni ubunifu uliovumbuliwa jahanam. Na wakati ubunifu unachukua mzizi katika ufalme wa jahanam, ufalme wa bahari unautuma duniani kwa utoaji. Na ufalme wa dunia halafu unaanza kutandia ufalme wa jahanam. Aibu kwenu! Nyinyi nyote! Studio ya Marvel, wewe pia! Kwa maana umekuwa ukitandia shetani kwa muda mrefu. Huu unabii NItauweka juu [kwenye tovuti], maana wewe ni tu ufalme duni wa jahanam.


Ulimwengu ZANGU – pangikeni na mkusanyike na mNIsikilize, watoto WANGU na mashujaa wa milele! Kusanyikeni! MIMI NI YEHOVAH na MIMI PEKEE NIliumba ULIMWENGU, Marvel Universe (au Ulimwengu wa Marvel) si shindano KWANGU. Wao sio mungu bado wanajifanya kama mungu, wameumba ulimwengu nyingi za vibonzo (komik). Lakini yote itachomwa katika moto mkubwa, moto mkubwa, mkubwa. Watoto Duniani, mnasikiliza na kutazama, “Ni mfululizo upi ufuatao?” na hata watumishi WANGU waaminifu kabisa wamenaswa katika upumbavu huu. SIjawaambia mtawaliwe na mfululizo wa hizi ulimwengu, hivi tu ni vikengeusha fikra kutoka kwa shetani. Nawaambia mvitelekeze, kila moja wapo.


Nasema, na kutikisa kichwa CHANGU kwa mamilioni wote wanaotazama hizi filamu na bado wanadai hawana muda wa Bibilia YANGU! Unawezaje sema hivyo? (YAH Anapiga [kwa] mkono WAKE kwa hasira) NIlimwaga yote NInayo kwenye hivi Vitabu! Vitabu vya zamani! NImefanya manabii WANGU wa zamani kuvificha ili visiharibiwe, ili mvisome! Ili mvisome! NImefanya manabii WANGU ambao hamwajui na wanafunzi wao kukimbia na kuvificha, kuvifungia katika magudulia, kuvifungia katika vyombo tofauti, kuficha mahali kwingi na hata vingine bado ambavyo vimefichika lakini vimesahaulika... ili viweze kuokoka moto, uharibifu, marisasi. Mnafikiri lilikuwa jambo rahisi?


NItawaangamiza! Na nyinyi mbaki tu wanyenyekevu ndani YANGU! Katika wakati ufaao NItawainua na SIdanganyi, MIMI NI YEHOVAH wa Milele, Muumba na mtunzi wa Kitabu cha Wokovu, mnakiita Bibilia katika lugha ya Kidunia. Someni Bibilia YANGU, watoto wa Dunia, kabla muda uishe na lazima mkimbie na kujificha na kumeng’enya Neno LANGU gizani. NInajaribu kuwaepusha kutokana na vitisho vya aina hivi, kwa hivyo someni Neno LANGU na muombee Safina YANGU (ambayo utaingia) iko wapi.


Mwisho wa Neno

5 views

Recent Posts

See All
bottom of page