top of page

Unabii 91 “Ee Israeli, Je, Si ULIAHIDI Kushika Torah?”

Updated: Mar 24


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa usiku wa 31 Oktoba, 2020Maandiko Husika


Kutoka 24:3

Musa alipokwenda na kuwaambia watu maneno

yote na hukumu zote za YEHOVAH,

wakaitikia kwa sauti moja,

“Kila kitu Alichosema YEHOVAH tutakifanya.”


Kutoka 24:7

Kisha [Musa] akakitwaa Kitabu cha Agano

Akakisoma masikioni mwa watu. Nao wakasema,

“Tutafanya kila kitu Alichosema YEHOVAH, nasi tutatii.”


Hesabu 23:19

MUNGU si mtu, hata Aseme uongo,

Wala YEYE si mwanadamu, hata Ajute.

Je, Amesema, kisha Asitende?

Je, Amenena, Asitimize?


Ujumbe wa Kinabii


Mambo hayako yanavyoonekana, mwanaNGU. Utatoa unabii kwa mataifa, makabila na ndimi nyingi. NItafanya paji la uso wako kama jiwe la mango na kutoka kwa mdomo wako kutamwagika Maji YANGU ya Uzima. Hivyo Asema MIMI, YEHOVAH.


Uso wako utakuwa uso WANGU na uso WANGU utakuwa uso wako, kwa maana, je, haukunywa kutoka kwa [kile] kikombe? Sura yako imebadilika.


Fungua malango yako KWANGU, ee Yerusalemu! Fungua wazi kabisa, maana MFALME wa UTUKUFU Ataingia! Tena, Nasema, fungua wazi kabisa na huyu MFALME wa UTUKUFU Ataingia (Zaburi 24:7-10). Fungua wazi kabisa! Inueni juu lango! Msiache. Tayarisheni Bango. Guteni na Mtukuzeni MTAKATIFU, Abarikiwe! Inueni Bango! Tukuzeni JINA LAKE katika mbingu za juu kabisa! Msiache! Refusheni kamba (Isaya 54:2). Panukeni na mshamiri, kwa maana YULE MKUU, EL wa Israeli ni YEYE, Amekuja. Hata kama simba kutoka mafichoni mwake, vivyo Amekuja.


Heshimu Taji la Mfalme. Tukuza JINA LAKE katika mbingu za juu kabisa (Zaburi 68:4). Msiache! Refusheni kamba.


Ee Yerusalemu, uliyeteketezwa na wakati, umeruhusu mahame yako kufifia. Lakini NImekuja. NImekuja katika UTUKUFU WANGU wote kurekebisha upenyu, kurejesha pengo. MIMI, YESHUA, ndiYE YEYE [HAMASHIAKH – (MASIA)] (Mathayo 16:13-17). METATRON ndiyo JINA LANGU na NInafanya kazi na MASHIAKH (MASIA) kutayarisha njia kwa ajili ya BABA (Kutoka 23:20-22). Ee Yerusalemu, tayarisha njia! Tayarisha barabara kuu ya MFALME (Isaya 40:3). Gharimu yote hadi itimie! Tayarisheni mioyo yenu na mifungo na maombi. Teshuvah (Toba)! Teshuvah! Teshuvah!


NIrudieni MIMI, YEHOVAH, na moyo wote. Rudini na msizurure. Najua jinsi ya kuchunga [vilemchungaji] watu WANGU (Isaya 40:10-11). Wewe ni mbuzi au wewe ni kondoo? Watu WANGU husikia sauti YANGU na NInawaongoza kwa chemichemi za maji mazuri ya uzima (Yohana 10:27). NIfuateni, kwa maana ni MIMI tu NIjuaye njia, ni MIMI tu NIjuaye ukweli, kwa maana NDIMI NILIYE ndiye UKWELI. UKWELI unatokana na MIMI, unatokana ndani YANGU. Kwa hivyo msisikize yule mgeni. Msisikize sauti ambayo inaweza kuwaongoza mbali na, kuwapotosha kutoka Huduma ya Torah Keeper [Mshika Torah]. Sikiza na msitie shaka ingawa mnaweza kosa kuelewa.


NItumainieni. NItafuteni na mtaelewa (Mithali 28:5). NInatahini na Nataka kuona kwa jinsi gani, kwa ari gani unataka kujua ukweli, tambua ukweli. Kuna sauti nyingi ambazo zimeingia duniani. Wewe ni wa ipi? Sauti ya ukweli, kwa ajili ya ukweli? Au sauti ya uwongo ikishuhudia katika roho ya shaghalabaghala, ya uhaini? NDIMI NILIYE Anakutazama, ee Israeli – daima NImekuwa na daima NItaendelea [kukutazama] (Zaburi 121:4). Jicho LANGU milele limekazwa juu yenu, kwa maani NIliwapa ahadi, NIlifanya agano ambalo Siwezi vunja (Hesabu 23:19).


Ee Israeli, timiza kiapo, timiza wajibu. Usipuuze Neno LANGU. Usipuuze neno lako, kwa maana uliahidi (Kutoka 24:3,7). NInakuwajibisha kwa neno lako. MIMI NDIYE YEHOVAH, YULE wa MILELE! Torah ni Neno LANGU! Hili ni agizo LANGU! NIfuate katika njia ZANGU zote, kwa maana Najua kile ni bora kabisa – mwisho toka mwanzo (Isaya 46:9-10).Mwisho wa Neno.


14 views

Recent Posts

See All

Comentários


Os comentários foram desativados.
bottom of page