top of page

Unabii 95 Thamini Sana Mapenzi ya BABA wa MBINGUNI


Umepewa Nabii Hannah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 11 Januari, 2021 wakati nikifikiria kuhusu jinsi tunapaswa kuthamini sana mapenzi ya BABA wa MBINGUNI


Maandiko Husika


Luka 12:32-34

32 Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa BABA

yenu Ameona vema kuwapa ule ufalme.

33 Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka.

Jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu,

mahali pasipokaribia mwizi, wala nondo haharibu.

34 Kwa kuwa hazina yenu ilipo, ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu.



Ujumbe wa Kinabii


Ni nini mnathamini sana juu ya mengine yote? Mapenzi yako au mapenzi ya BABA wa MBINGUNI? Kwa maana pale hazina yako ipo, hapo moyo wako utakuwa pia (Mathayo 6:19-21). Mapenzi yako yanavunda, yanavundisha – hayapaswi kufufuliwa. Lakini pumueni ndani YANGU, ee watoto. Pumueni ndani YANGU, MIMI BABA yenu YEHOVAH na mpate utegemezi wenu (Zaburi 20:6-8). Sio vizuri zaidi hivyo, sio rahisi zaidi njia hiyo?


Usione hisia zako kuwa kitu chochote cha kunata, kuinua, kuinuliwa juu ya Sheria ya Torah YANGU. Nimesema hisia sio fimob ya kifalme Ninayotawala nayo; Sijawahi, Sitawahi. Lakini pumueni ndani YANGU, ee watoto. Niruhusini Nijaze mapafu yenu na Pumzi ya Uzima. Vinginevyo mtakuwa vuta ndani uvundo, muozo wa nyama inayooza na hata msijue– mmezoea sana kufanya mambo njia yenu.


Lakini NDIMI NILIYE yu hapa! MIMI, YEHOVAH! MIMI, YESHUA! Tuko hapa! MIMI, METATRON. Tuko hapa. Kutumikia wanadamu Tumekuja (Mathayo 20:28). Lakini msipuuze huruma YETU, kwa maana SISI ni WATAWALA WAKUU. Enzi ya kigalaksia, utawala wa milele Tunashika katika Mikono YETU. Uumbaji wote tumeshikilia Mikononi MWETU. Kuinua, kujenga – SISI ni MWENYEZI MUNGU, EL SHADDAI.


Naja katika umbo, maumbo ambayo hamfikirii. Msihukumu kulingana na ionekanavyo kwa nje, lakini na uamuzi mwema (Yohana 7:24). Je, inambatana na Sheria ya Torah YANGU? Ikiwa hivyo, mbona unahukumu kimakosa? Maoni yako si ukweli, sio Injili – haijawahi kuwa na haitawahi kuwa. Acheni “ndio” yenu iwe “ndio” na “la” yenu iwe “la”. Chochote zaidi ya hili ni upumbavu, ni uchongezi, ni ujinga (Mathayo 5:33-37). Ningewaepusha machungu ya moyoni na taabu, watoto WANGU, ikiwa tu “ndio” yenu ingekuwa “ndio” na “la” yenu ingekuwa “la”. Usiape, lakini timiza ahadi zako. Gandamia “ndio na amina”, א (ALEF) na ת (TAV) (Ufunuo 1:8).


Kwa hivyo, Nisifuni watoto WANGU, kwa maana Nimewaonyesha njia! Ni baba wangapi wanapotosha watoto wao hata [wakiwa] na nia nzuri kabisa za kufanya vitu sawa? Na bado MIMI, BABA yenu YEHOVAH, Nina nia nzuri kabisa, matilaba mema kabisa, na ukweli (Mathayo 7:11). Kwa hivyo Nifuateni na msisikize mwengine. Mtajua wale Ninaotuma, kwa maana matendo yao yatafuata maneno yao. Hawa wanaweza aminiwa. Wale wanaofuata Sheria za Torah YANGU, Njia za Torah YANGU. Hawa wanaweza aminiwa. Wale wanaoweka YESHUA na METATRON kwanza juu ya yote. Kwa wale wengine wote Nasema, “Songeni nyuma YANGU, kwa maana ninyi ni kikwazo. HamNipendezi. Watenda maovu ambao hawalindi Ninachoenzi lakini watafuta kupora, kuiba, kunyang’anya (Mathayo 7:21-23). Haya si matendo ya watakatifu bali ya wale ambao ni wa shetani bwana wao. Tubuni!”


kwa hivyo mnaona, watoto WANGU, jinsi nia ZANGU ni nzuri? Mipango Ninayo kwa ajili yenu ni kwa wema (Yeremia 29:11). Tangu lini mtoto wa miaka mitano akaelewa mipango ya baba yake? Vivyo ilivyo nanyi watoto WANGU. Hamtaelewa sikuzote. Ni bora msikize! Hamtaelewa sikuzote, lakini hilo halipaswi liwazuie kutii, kung’ang’ana kadri mwezavyo. Hata Ninawavalisha viatu vya utayarisho wa Injili ya Amani. Nawapa amani YANGU (Yohana 14:27). Sasa tembeeeni ndani yake. Tembeeni naYE – wote wawili א (ALEF) na ת (TAV). Nisikieni! Tembeeni naYE, kwa maana wakati huo mtakuwa mnatembea naMI, MIMI, BABA yenu YEHOVAH. Selah.


Mwisho wa Neno.


©2019 by Torah Keeper.

bottom of page