Umepewa Nabii Hannah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umepokewa 4 Desemba, 2020
Maandiko Husika
Zaburi 133:1
Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!
Waefeso 4:1-6
1 Basi, mimi niliye mfungwa wa BWANA, nawasihi mwenende kama inavyostahili wito wenu mlioitiwa.
2 Kwa unyenyekevu wote na upole, mkiwa wavumilivu, mkichukuliana kwa upendo.
3 Jitahidini kudumisha umoja wa ROHO katika kifungo cha amani.
4 Kuna mwili mmoja na ROHO mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja.
5 Tena kuna BWANA mmoja, imani moja, ubatizo mmoja,
6 MUNGU mmoja ambaye ni BABA wa wote, Aliye juu ya yote, katika yote na ndani yenu nyote.
Zakaria 1:3
Kwa hiyo waambie watu: “Hivi ndivyo YEHOVAH wa majeshi Asemavyo: ‘NIrudieni MIMI,’ Asema YEHOVAH wa majeshi, ‘naMI NItawarudia ninyi,’ Asema YEHOVAH wa majeshi.”
Ujumbe wa Kinabii
Sikia kilio cha moyo wa BABA. Kilio cha NAFSI YANGU. NIko hapa, watoto WANGU. Kilio cha moyo WANGU ni umoja kati ya ndugu, umoja kati ya wana wafalme (Zaburi 133). Jishughulisheni naMI, “NDIMI NILIYE” MKUU. Tumikieni kilio cha moyo WANGU. BABA wenu Awapendaye Anawalilia. Furaha YANGU ni kuona watoto WANGU wakitembea katika ukweli (3 Yohana 1:4). NImetuma UKWELI na JINA LAKE ni YESHUA, JINA LAKE ni METATRON. Wale WAWILI WAmekuwa MMOJA, kwa maana WAnatembea pamoja katika umoja kamili – ALEF na TAV, miisho yote ya uzi, ya kamba, ya kifungo kinachofunga (Ufunuo 1:8). Miisho yote ya upinde wa jua [spektramu].
NIone, NIsikie NIkinguruma eh Yerusalemu, Yerushalayim. NIsikie na NIone katika maisha yenu ya kila siku, kwa maana kwani SIwapi mkate wenu wa kila siku, kiwango cha kila siku, kikombe cha kila siku kulingana na utajiri WANGU katika UTUKUFU (Zaburi 145:15-16)? Hivyo Nasema MIMI, YEHOVAH. NInatabiria siku za baadaye na kuigandisha kwa umilele. Wakati wote, misimu yote ya uendelezaji inapatikana ndani YANGU. MIMI ni Muongezeka hatua kwa hatua na bado [NI] kamili. MIMI, YEHOVAH, ni BABA wenu KAMILI ANAYEWAPENDA. Na ni nani aliye kamili ila MUNGU pekee (Marko 10:18)? MIMI, YEHOVAH.
NIjueni, watoto WANGU, na mujue kudura yenu. Kwa maana nyote mnapaswa kujipata ndani YANGU. Misimu ya neema yenu imekuja NInapoita mwaka WANGU wa Shemitah (Walawi 25:1-7, 20-22; Kumbukumbu 15:1-6). Njoo! Inuka, ewe mwenye umbo zuri! Kuja naMI, maana NImekutayarishia makao nyikani (Ufunuo 12). Njoo ule naMI chakula kikuu kwenye vikorokoro vizuri kabisa, vizuri kabisa vya china. MIMI, YEHOVAH, Nasema hivyo.
NInatayarisha watu, NIkiwaita kwa jina – msimu wa makazi – kama katika siku za Ezekieli (Ezekieli 37:1-14). Mifupa iliyokauka ishi! Njooni, wakuu wa Yakobo! Njooni na muishi! Jioneni ndani YANGU, MIMI, YEHOVAH, kwa maana MIMI NI UHAI. Chagueni UHAI, NIchagueni MIMI na mtaishi (Yohana 1:1-5). Saa ya giza inasonga karibu. Usijipate nje. MIMI NI MWANGAZA WAKO! Kaeni naMI huu msimu wa Hanukkah.
MIMI ni HEKALU yenu ambayo haijanajisiwa. Pateni riziki yenu ndani YANGU. Kuleni mkate wa wonyesho. Shirikini ALEPH na TAV – WALINDI wa NAFSI YANGU wakishuhudia kilio cha moyo WANGU kwa mataifa. WAO ni kilio cha moyo WANGU, mapigo ya moyo WANGU (Zekaria 1:2-6). Kwa maana si DAMU na MAJI vinapatikana katika moyo*, moyo WANGU? DAMU inalia na hivyo pia MAJI [yanalia], watoto WANGU, kizazi CHANGU, wapendwa na wathaminiwa WANGU. DAMU inalia na hivyo pia MAJI. Mshawahi fikiria kuyahusu, sauti ya maji mengi (Ezekieli 43:2, Ufunuo 1:9-20)?
DAMU inalia uhai na MAJI yanarudisha mwangwi uo huo. Sauti mbili na bado moja(Isaya 40:3-10). Hawahitilafiani. WAKO katika upatanifu kamili wakiimba wimbo wa wawili na bado wanasikika kama mmoja pekee. Hivi ndivyo mnapaswa kuwa watoto WANGU, kwa maana haiko katika Kitabu cha Matendo ambapo waliinua sauti yao kwa moyo mmoja na kuomba hivyo (Matendo 4:24)? Ruhusuni ROHO WANGU kutiririka na siku hizi na makubwa zaidi mtaona, mtapitia mradi mnatii kilio cha moyo WANGU, sauti ya moyo WANGU. Selah.
*Wakati wa hili Neno, niliona maono ya mkato wa moyo na kwamba ndani, kuna vyumba vinne. Hili linawakilisha FAMILIA TAKATIFU - YEHOVAH, YESHUA, IMMA GLORIYA, na METATRON.