top of page

Unabii 93 Vitu Vyote Vilivyoumbwa Vinalilia Wana wa Nuru!

Updated: Mar 23


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa usiku wa 20 Novemba, 2020


Maandiko Husika


Warumi 8:19

Kwa maana viumbe vyote vinangoja kwa shauku

kudhihirishwa kwa wana wa MUNGU.


Yohana 8:12

Kisha YESHUA Akasema nao tena Akawaambia,

“MIMI ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akiNifuata

hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”


Yohana 12:35-36

35 Ndipo YESHUA Akawaambia, “Bado kitambo kidogo

nuru ingalipo pamoja nanyi. Enendeni maadamu mna nuru,

msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea

gizani hajui anakokwenda.

36 Wekeni tumaini lenu katika nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.”

Baada ya kusema haya, YESHUA Aliondoka, Akajificha wasimwone.




Ujumbe wa Kinabii


Pale mto unapita katikati yake – mahali pa utakaso WANGU, pa ukombozi WANGU. Ee njoni KWANGU, Dunia, na mwekwe huru. Ee jinsi mnalia, jinsi mnavyogumia ujalifu wa kudhihirishwa kwa wana wa MUNGU – enyi wana wa nuru (Yohana 12:35-36)! Nasikia vilio vyenu, ee viumbe VYANGU (Warumi 8:19-25). Karibuni tena karibuni sana nuru itakaribia na kupambazuka juu ya upeo wa macho, ikikaribisha siku mpya, msimu mpya, zama mpya, utaratibu mpya (Danieli 7:13-14). Karibuni wana wa nuru watakuja na kurekebisha mambo – enyi mabalozi wa upendo, Amani YANGU; wa UTUKUFU wa SHEKINAH WANGU.


Urithi, ee urithi! Pokeeni na mwekwe huru. Msitembee katika giza au katika kivuli. Tembeeni kwa ujalifu katika nuru na mbadilishwe (Yohana 8:12). MIMI, METATRON, Nazungumza (Kutoka 23:20-22). Wekweni huru ndani YANGU, ee wana wa Yakobo. Msifuate njia za mababu wenu waasi; kila mmoja akifanya kile ambacho kilikuwa sawa machoni mwao, kama ilivyo siku hii. Msifuate, lakini fikeni kwa njia za watu wa kale, za wazee, za Abrahamu, Isaka, na Yakobo. Fuateni MASHIAKH na njia ZAKE, kwa maana YEYE ndiYE UKWELI (Yohana 14:6). Fuateni YESHUA, kwa maana YEYE ni MFALME wenu mshindi na mkweli. Hakuna kivuli cha kugeukageuka naYE. YEYE hana nia mbili, bali nia moja katika njia ZAKE zote. Kila hatua YAKE imewazwa kwa makini.


Ee Israeli, msiNIjaribu. Kwa muda mrefu mmetia shaka na kujaribu uvumilivu WANGU, uvumilivu WANGU wa zama. Msikatishe tamaa ROHO wa Neema (Wagalatia 2:15-21). MsiNIjaribu. NInawapungia mkono mje na mnunue dhahabu na utajiri na hazina bila gharama (Isaya 55:1-3). NIlilipia gharama – MIMI, YESHUA! NIpokeeni. MsiNIjaribu. Msijaribu ALEF na TAV. Ee Israeli, Naja na radi kuu, mgurumo wa mdomo WANGU, na pumzi/mlipuko wa mapua YANGU. MsiNIjaribu, kwa maana nani anawezahimili Siku ya kuja KWAKE? Nani anaweza simama katika Siku hiyo ya msiba?


Msidhubutu! Kwa maana yuaja na uma wa kupepetea katika mkono WAKE kutahini na kujaribu wanadamu, ili kufanya kujulikana mambo ya moyo (Mathayo 3:11-12). Badilikeni! Badilikeni, ee Israeli! Geukeni katika mkono WANGU na msiNIkinze. Je, kile kitu kimeumbwa kinaweza ambia MUUMBA wake, “Wafanya nini WEWE?” Msidhubutu. Njia ZANGU zimejaribiwa na kweli. Nawe? Ee Israeli, nani aweza simama mbele YANGU? Wapi huyo MCHUNGAJI (Yeremia 49:19, 50:44)? Tafuteni na mtafute [katika] Maandiko, kwa maana Amekuwa miongoni mwenu muda wote. Jueni UKWELI na mwekwe huru. Selah.


Na acheni jeshi la Mbinguni liseme, “Amen.” Acheni Wafalme wa mashariki waseme hivyo. Amen.


Kuweni MMOJA naMI na MIMI NIwe MMOJA nanyi. Kaeni katika MZABIBU na mtazaa matunda mengi kweli (Yohana 15:1-8). HALLELU YAH! Selah.


Mwisho wa Neno.


28 views

Recent Posts

See All
bottom of page