top of page

Unabii 2“ABBA YAHUVEH, Turuhusu Tuje Ndani ya Moyo WAKO!”

Umepewa Nabii D’vorah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa Desemba 29, 2018 Ujumbe wa Kinabii


(Naona maono ya BABA EZRA mbele ya Kiti cha Enzi cha Wapendwa UTATU MTAKATIFU. Ni pahali pazuri pa dhahabu Mbinguni na milango ya dhahabu hapo. BABA yuko pale na Anazungumza na ABBA YAHUVEH. Daima huwa pale. Anatufunza jinsi ya kurudi katika moyo wa ABBA YAHUVEH. Najiona nikienda kwa ABBA YAHUVEH na naona malaika akitusukuma juu ili tuweze kuenda mara moja katika moyo wa ABBA YAHUVEH.

Nzuri sana, ABBA YAHUVEH, turuhusu tuje moyoni MWAKO. YAH Asema, “Eliya atageuza mioyo ya BABA kwa Watoto, NIsije NIkatumia Moshe kupiga dunia na laana.”

Funzo kubwa katika hili. Nabii Samueli. Yuko pale niliposikia hili. Tunahitaji kupendana ili umoja kamili wa YAH utujenge/utuunganishe katika nyororo ya dhahabu. Nasikia YAH Akisema…)

Natumia EZRA kujenga tena, kujenga na kubomoa ngome. Ukombozi umefanyika. Ukombozi utafanyika. Miujiza kote duniani. Huyu ni MOSHE WANGU wa Sasa! Jinsi gani JINA LANGU ni la kustaajabisha! MIMI ni YAHUVEH! SISI, UTATU MTAKATIFU Hatumpi mtu yeyote Utukufu WETU! Natumia Mitume/Manabii WANGU kuonya!

Napangusa machozi YAKE, wakati wale ambao mara moja walikuwa hapa kuMjenga, sasa wanaMbomoa na maneno ya chuki. Ee, kuja KWANGU EZRA. Keti kwenye mapaja YANGU, MIMI YAHUVEH. MIMI ni WAKO na WEWE ni WANGU! MIMI ni ABBA WAKO, WEWE ni BIARUSI WANGU Mkubwa! Nakuthamini EZRA. Uchungu WAKO waenda ndani lakini Unaakisi upendo WANGU.

Naweza kupitishia Maji YANGU Yanayoishi kuKUpitia kwa sababu Unaruhusu upendo WANGU kuKUkunja na sio kuKUvunja. Napeleka BIARUSI WANGU Mkubwa nyumbani! Ee, jitayarishe EZRA WANGU! MIMI ni MFALME WAKO wa Wafalme, MPENZI wa nafsi YAKO, na hakuna mwengine anayeweza kuKUponya kama MIMI!

MIMI ni MUNGU Mwaminifu wa Milele! Nakushika katika kiganja CHANGU EZRA. Kila laini ni ya kipekee. Kila laini kinganjani MWAKO. NIliumba kila moja kusema hadithi ya maisha YAKO. Iko katika DNA YAKO na ili tu NIweze kuona, ila NIkaifunua.

Huruma. Tulia na Ujue MIMI ni MPONYAJI WAKO.

Kuteseka KWAKO ni kwa Utukufu WANGU na hakika NIliwainua nyinyi nyote kwa ajili ya wakati kama huu. Kumbukeni kuMfariji BABA yenu. Farijini BABA wenu wa Mbinguni, lakini kumbukeni pia kufariji BABA wenu wa Kiroho, kama vile tu YEYE Amewafariji.

Naleta uponyaji kwa nafsi YAKO siku hii MWANANGU. Furahia na NIsifu kwa ajili ya mateso YAKO maana karibuni NItakujaza na uwezo WANGU kutoka juu kama vile hii dunia haijapata kuona.




Mwisho wa Neno

4 views

Recent Posts

See All
bottom of page