Unabii 28 Ufunuo wa BINTI wa MUNGU, “URIYAH ni JINA LANGU!”

Updated: Jan 25, 2021

Umepewa Nabii D’vorah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 10 Machi, 2019

Onyo!

Kabla ya kusoma, unaonywa kuwa huyu si mwanamke tu anayezungumza haya maneno. Ikiwa una tashwishi au unashuku hili Neno kuwa la YAH au la, usizungumze dhidi yake bali lipeleke katika maombi. Unaonywa pia YAHUVEH Alisema kuhusu kukufuru ROHO MTAKATIFU ni dhambi ya chukizo kuu ambayo haiwezi samehewa. HUYU ni BINTI wa YAHUVEH. Kwa hivyo unaonywa, ikiwa utazungumza dhidi YAKE, utakuwa unaweka nafsi yako hatarini. Nakuhimiza kutumia hadhari na nafsi ambayo YAH Amekubariki nayo na utafute Hekima kabla ya kuzungumza maneno yanayoweza kukuhatarisha na kukupeleka kwa moto wa Jahanamu milele. YAHUVEH ndiYE HAKIMU, si mimi, lakini lazima niwaonye la sivyo mimi mwenyewe nitawajibishwa. Kwa hivyo, tafadhali, usimpige mawe Mjumbe. Mimi ni msemaji tu na nazungumza ninachosikia kutoka Mbinguni. Ikiwa utazungumza dhidi ya Ujumbe huu, unazungumza dhidi ya MWENYEZI MUNGU WENYEWE!

Pia, URIYAH linatamkwa (OO-REE-YAH).


Maandiko Husika

Zaburi 45:13-17 “Utukufu wote una BINTI MFALME katika chumba CHAKE; vazi LAKE limefumwa kwa nyuzi za dhahabu. Anaongozwa kwa MFALME, Akiwa Amevalia mavazi yaliyotariziwa, Mabikira wenzake wanaMfuata na wanaletwa KWAKO. Wanaingizwa ndani kwa shangwe na furaha, na kuingia katika jumba la MFALME. Wana wenu watachukua nafasi za baba zenu, mtawafanya wakuu katika nchi yote. Nitadumisha kumbukumbu la JINA LAKO katika vizazi vyote, kwa hiyo mataifa wataKUsifu milele na milele.”


Mithali 7:4 “Mwambie HEKIMA, ‘WEWE ni DADA yangu,’ na uite UFAHAMU JAMAA yako.”


Mithali 31:26,29 Huzungumza kwa HEKIMA na Sheria ya wema iko ulimini MWAKE. … “Wanawake wengi hufanya vitu vyenye sifa nzuri, lakini WEWE Umewapita wote.”


Yosefu na Asnati 15:7-8 “Maana TOBA YUmo Mbinguni, BINTI, mrembo zaidi na mzuri, wa ALIYE JUU SANA. Na YEYE MWENYEWE Anasihi MUNGU ALIYE JUU SANA kwa ajili yako nyakati zote na kwa ajili ya wote wanatubu katika JINA la MUNGU ALIYE JUU SANA, kwa sababu YEYE ni BABA wa TOBA. Na YEYE MWENYEWE (TOBA) ni Mlinzi wa Wanawali wote, na Anakupenda sana na Anaomba ALIYE JUU SANA nyakati zote kwa ajili yako na kwa wote wanaotubu Aliandalia mahali pa pumziko Mbinguni. Na Atawafanya upya tena, wote wanaotubu, na kuwatumikia YEYE MWENYEWE milele na milele. Na TOBA ni Mrembo kupindukia, Mwanamwali takato na hucheka siku zote, na YEYE ni raufu na mpole. Na, kwa hivyo, BABA ALIYE JUU SANA AnaMpenda, na Malaika wote wanaMstahi sana. Na MIMI pia, NaMpenda sana, kwa sababu YEYE pia ni DADA YANGU.”

Ujumbe wa Kinabii

(Kabla nisikie ujumbe ufuatao, nilikuwa nimewaza zamani ikiwa ABBA YAHUVEH na IMMAYAH wetu wana BINTI Mbinguni. Ikiwa familia ni mfano wa kile kilicho Mbinguni, si basi Wapendwa UTATU MTAKATIFU WAngekuwa na BINTI pia? Tuna YAHUVEH BABA, na IMMAYAH MAMA wetu Mbinguni, na YAHUSHUA HAMASHIACH ambaYE ni MWANA WAO, lakini je, BINTI? Katika mfano upi binti aliumbwa? Nilipokuwa nimeketi mezani na familia yangu katika YAHUSHUA, nilikuwa na maono ya ‘Mwanamke’ ambaYE Alikuwa MUNGU na hakuwa IMMAYAH! Nilikuwa nimesema maono haya kwa familia na sikuwa naenda kusema kile nilifikiri ilimaanisha kikamilifu kwa sababu ya kutotaka kuleta kikwazo kwa yeyote. Muda mfupi baadaye, nilisikia Neno lifuatalo kutoka Mbinguni kutoka kwa BINTI URIYAH ambaYE Alitaka kuJItambulisha kwa dunia kwa wakati huu.)


Kutoka kwa mdomo wa mashahidi wawili au watatu NENO LANGU linaimarishwa. Manabii WANGU, inamisheni sikio lenu kwa sauti YANGU!


MUZIKI, MIMI ni MUZIKI. MIMI ni MUZIKI. MIMI ni … Nena katika imani, Binti WANGU! Nachukia dhambi! NIsifu! NItafunua zaidi. MIMI ni MUZIKI! MIMI ni ROHO wa UNABII! MIMI ni MUZIKI unaotoka kwa MAMA. NIsifuni Wapendwa WANGU!

NItafunua zaidi kwenu. NInanong’oneza katika kila sikio lenu. Nawazungumzia ufunuo ambao bado haujafunuliwa ambao umefungiwa katika Kitabu cha Danieli. Kwa maana Danieli hakujua kuNIhusu.


ROHO ya UWAZI!

ROHO ya UNABII!

ROHO ya MUZIKI!

ROHO ya HEKIMA!


Hizi zote zinapatikana ndani YANGU! Ee, NIsifuni na NItafunua zaidi!


(Sifa zinaanza; NaMsikia Akisema, “Je, unasikia upepo ukipuliza?”)


Ee muhibu WANGU, NImefunua na NItakufunulia zaidi kuhusu BINTI WANGU. YEYE pia ni ROHO ya UNABII.

Maana NIna BINTI na MWANA!

MIMI, YAHUVEH, na MIMI, IMMAYAH, Twanena sasa!

EZRA, lazima Ufunike Watoto WAKO wanapopokea ufunuo hizi. Kwa maana hizi ni siri ambazo shetani hakuwahi taka zitoke kwa Chumba CHANGU cha Kiti cha Enzi. Lakini ee, EZRA, NImeKUfunulia pia mbeleni Ukiuliza, “ABBA YAHUVEH, IMMAYAH wana BINTI?”

Ndiyo! Ndiyo, MWANANGU! NDIMI NILIYE na ni MIMI NInaYEzungumza naWE.

MIMI NDIMI NILIYE!

YAHUVEH ni BABA YANGU!

YAHUSHUA ni KAKANGU!

IMMAYAH ni MAMANGU!


Kwa maana SISI, UTATU, TUna siri nyingi. Ee, Wapendwa! NImewatazama nyote. NImo kifuani mwa BABA YANGU. NImeishi ndani yake. TUnajuana vizuri zaidi kuliko nyote mnavyojua. Hamkumbuki tu.


NIlipowatuma kwa hii dunia, BABANGU Aliposema, “Nenda!” – mlienda; siri kutoka Mbinguni zimefutwa kutoka kwa kumbukumbu yenu. Lakini zimehifadhiwa katika chembe za mafuta, na NInarejesha DNA yenu. Mnapokunywa hayo maji msikadirie pungufu uweza huu!


MIMI ni MOTO!


Kwa maana MIMI na MAMANGU HEKIMA, MAMA yenu SHALOM, IMMAYAH wenu, SISI ni MMOJA na SISI ni MOTO MTAKATIFU!

MIMI ni MUZIKI. Mnaposifu, NIko hapo. Ikiwa mtajua au msijue. NIko hapo.


NIulize Nikuguse ili usifu BABA YANGU, kuNIsifu MIMI, kusifu YAHUSHUA, kusifu MAMANGU IMMAYAH!


Msiwe na tashwishi Watoto WANGU. MIMI ni DADA yenu! MIMI ni MWENYEZI MUNGU! MsiNIweke katika bweta. Msiweke ELOHIM katika boksi, kwa maana SISI NI ELOHIM!


TUnatawala katika Umoja. SISI, UTATU MTAKATIFU na MIMI!

Msifikiri tu kwa sababu macho yenu hayajaona na masikio yenu hayajasikia kwamba SIko. Mnataka ukamilifu wa upako? Kwa hizi siku 40 zinazofuata, hizi siku 40 za mwisho kabla NIwabadilishe, mlihitaji huu ufunuo!


Nyinyi wanawake (MUNGU Azungumza na mabinti WAKE) – Nitawafunulia zaidi. Pokea Maji Yaliyo Hai moja kwa moja kutoka kwa Kiti cha Enzi cha MAMA YANGU!

NIna Kiti cha Enzi pia, mwajua! NIna Kiti cha Enzi, pia. Na kiko pale karibu na MAMA YANGU. Mwafikiri mfano wa binti unatoka wapi?


Puliza Binti! Puliza ufunuo kwenu. (Anapuliza kote mezani) mara 4 na 1 kwa ajili YANGU.


URIYAH!

URIYAH ni JINA LANGU!


Unashangaa mbona umesikia ‘URIYAH’, kwa maana hili ni kike. URIYAH! Binti, umesikia jina hili wiki iliyopita tena na tena! Na la, la, la, sio kwa sababu ya mwanamme yeyote – na ingawa Nakupenda mwanaNGU – Nilikuwa Namwonyesha mapema ili NIweze kuleta huu ufunuo na NIliweka katika ndimi zilizo katika mdomo wake na NIkaamsha upako wa Unabii, ili nyote mweze kushahidi huu ufunuo! Ili nyote muweze kufunuliwa. Na hati-kunjo ambazo NImewapa – msifikiri kwamba hazina sehemu yoyote ya hili. Hivyo ndivyo jinsi ni muhimu kupokea hizo hati-kunjo ambazo zinatoka moja kwa moja toka Mbinguni, kutoka kwa Chumba cha Kiti cha Enzi.

MIMI, YAHUSHUA, Nazungumza sasa, na ya MIMI, BABA YAHUVEH, na ya MIMI, IMMAYAH. Mbarikiwe Watoto WANGU! Pokea huu ufunuo! (Wote walisema, ‘Naupokea!’)

Ni nyinyi pekee Nimefunulia hili katika dunia nzima. Hii ndiyo maana mnapaswa kufunika dada yenu na nyinyi nyote mnafaa kufunika wenzenu!


Huu si mchezo! SIzungumzi tu kuzungumza. Mnadhubutu vipi kuNIsaili? Yeyote kwenu, msiNIsaili! Msisaili! Maana kwani hili halitoshi, maono, ufunuo, ndoto, haya yote ambayo NImewaonyesha hadi sasa.


Nawapenda! Napenda kila mmoja wenu! Nyinyi ni Kaka WANGU na Dada ZANGU. Lakini MIMI ni MWENYEZI MUNGU wenu. Msisahau hili. Napaswa kustahiwa.


Ufunuo nyingi mno, siri nyingi mno Nitakufunulia binti. Kwa wanaume WANGU wote wanaokaa kwenye hii meza, na zaidi kabisa kwa EZRA WANGU!