top of page

Unabii 3 “Shika Amri ZANGU, Sheria ZANGU!”

Umepewa Nabii D’vorah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa Desemba 31, 2018

Ujumbe wa Kinabii


Shika Amri ZANGU, Sheria ZANGU!

Kwa hivyo waona Binti YANGU mpendwa? Fizikia ya kwanta ndio jawabu, lakini siyo ya muhimu zaidi, kile kinachofaa zaidi. Ni kujazwa na upendo WANGU. NItazame MIMI! Hakuna mwengine anayeweza fanya kile Naweza fanya. NIabudu MIMI! Ee Binti YANGU, MIMI ni MUUMBA wako! Wewe ni Mchaguliwa Mteule WANGU, BiArusi WANGU mrembo. Himizaneni na endeleeni kutia moyo BABA yenu. Jifunze kutoka KWANGU. Jifunzeni kuhusu ukweli WANGU.

NItawavuta karibu zaidi kuliko mbeleni. Ee, Binti YANGU mpendwa, BiArusi WANGU, NImependezwa nawe sana leo. MIMI ni ABBA YAHUVEH wako! Umetengezwa katika mfano wa BIBI YANGU, IMMAYAH ni Utukufu wako! Kumbuka hilo. YEYE ni Jiwe LANGU Lililo Hai, Mrembo WANGU.

Utakatifu wa Ndoa ni wa thamani sana KWANGU. Nyinyi 2 (Yahusu wachumba ambao YAH Anazungmza nao) hamtambui maghala NIko nayo yanayongojea Ndoa yenu. Kuwa na uhakikisho wa hili Wadogo WANGU, kila wakati mnaNIsifu, Namwaga tu zaidi ya upendo WANGU juu yenu!

Msisahau hili. Kuweni maasumu, kuweni safi. Tumainia katika vile vitu havionekani, na katika hili MIMI ni BABA MUNGU wenu, ABBA YAHUVEH wenu. Naahidi NItajifanya NIjulikane kwenu na NItajidhihirisha ndani yenu maana nyinyi ni adilifu machoni MWANGU! Sio kwa sababu ya kile fizikia ya kwanta yafanya, lakini kwa sababu ya neema na huruma YANGU.

Kumbuka, endeleeni kuNIuliza NIfunue zaidi ya upendo na uvumilivu WANGU, ili matunda ya IMMAYAH wenu yataendelea kumea na kusonga mbele, na NItawashikilia, na MWANANGU YAHUSHUA Atapumua juu yenu na kufanya makao YAKE kukaa daima ndani yenu.

Ee, EZRA WANGU Mpendwa! Shikilia kwa nguvu MWANANGU. Usikate tamaa ya matumaini.

JINA la MWANANGU linakufuriwa! Ee NIahidi, EZRA, WEWE ni MWANANGU, NIfanye NIkuonee fahari na endelea. Imarikeni, jitianeni moyo. Msiruhusu nafsi zenu kufadhaika au kuruhusu ugomvi kati yenu (nyinyi nyote). Pumzikeni tu ndani YANGU na mtaona baraka. Nzuri zaidi, na si chochote chini yake. MIMI, YAHUVEH, NImezungumza.



Mwisho wa Neno

2 views0 comments
bottom of page