top of page

Unabii 33 “Tena, MIMI, YAHUVEH, Nasema, Msiwe na Wasiwasi Kuhusu Kemeo! Utiaji Moyo wa MELEKH TSEDEK

Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 24 Machi, 2019

Maandiko Husika


Mithali 3:11-12

“Mwanangu, usiidharau adhabu ya YAHUVEH na usichukie kukaripiwa naYE, kwa sababu YAHUVEH Huwaadibisha wale Awapendao, kama vile baba afanyavyo kwa mwana apendezwaye naye.”

Mwanzo 14:18-20

“Ndipo MELEKH TSEDEK Mfalme wa Salemu Alipoleta mkate na divai. Alikuwa Kuhani wa EL (MUNGU) ALIYE JUU SANA. NaYE Akambariki Abramu, Akisema, ‘Abarikiwe Abramu na EL ALIYE JUU SANA, Muumba wa mbingu na nchi. Abarikiwe EL ALIYE JUU SANA, ambaYE Amewaweka adui zako mkononi mwako.’ Ndipo Abramu akaMpa MELEKH TSEDEK sehemu ya kumi ya kila kitu.”

Waebrania 5:5-6

Pia MASIA Hakujitwalia utukufu YEYE MWENYEWE wa kuwa Kuhani Mkuu, bali AliMtukuza YULE AliYEmwambia, “WEWE ni MWANANGU; leo MIMI NImeKUzaa.” Pia mahali pengine Asema, “WEWE ni Kuhani milele, kwa mfano wa MELEKH TSEDEK.”

Ujumbe wa Kinabii


(Nilikuwa naMtafuta YAH kwa ajili ya kichwa cha Neno nilisikia wakati Alianza kunena nami. Hili hapa Neno hilo na linaitwa “Msiwe na Wasiwasi Kuhusu Kemeo” (ulipokewa 12-03-19; Neno:)

Ndiyo jivishe joho lako la jubilii, la ushindi MwanaNGU. Msiwe na wasiwasi kuhusu hizi kemeo, maana zinahitajika. Zipokeeni na furaha Watoto WANGU, kwa maana mnasonga tu karibu na 100%. Na kila tendo la utiifu, mnaNIpendeza. Msitie shaka upendo WANGU kwa kila mmoja wenu. Kwa kweli ni kwa Kiwango cha Mbinguni – kiwango kizuri – ambacho NInawahukumu.

(Halafu Neno likaja:)


Msiwe na wasiwasi kuhusu kemeo. Tena, MIMI, YAHUVEH, Nasema msiwe na wasiwasi kuhusu kemeo. Jioneni kama watoto wachanga. Fikiria huyo mtoto mchanga anaoshwa kutokana na uowevu wa mamake. Kemeo ni MAJI YAISHIYO yanayowaosha kutokana na unajisi za hii dunia. Kuweni na mtazamo mwema. Msione hizi kemeo kama nyundo inayotumika kuponda na kuangamiza chombo.


NDIMI NILIYE si shutuma. SIshutumu lakini tu Natafuta kuhuisha, kuleta nguvu mpya, na kufanya mpya (Warumi 8:1). Hiyo ndiyo Asili na Silika YANGU. Ikiwa mtu anaNIkana, basi wanaNIacha bila chaguo bali kufanya kile SIngependa kufanya, kwa maana SIta na SIwezi stahimili uasi katika viwango VYANGU, katika utaratibu WANGU.


HUYU ni MELEKH TSEDEK (Melkisedeki) Anazungumza. Utaratibu WANGU unahusu ukamilifu, kutumikia BABA Apendaye na Aishiye na upendo ulio kamilika. YEYE ni Mnyenyekevu. YEYE ni Mkweli. Shikamaneni naYE Watoto WANGU, na msiondoke kutoka kwa ushauri, wasia WAKE wenye hekima, kwa maana Maneno YAKE sio kama maoni matupu ya mwanadamu. Na mnajua kile NInachofikiria kuhusu maoni – hayatakiwi wala hayajauliziwa. NInakaa katika Ukweli na SIjali kuhusu chochote kilicho chini yake, maana mbona NIpoteze wakati WANGU katika nadharia na uzushi?


Pale ambapo pana maneno mengi, dhambi haipo mbali (Mithali 10:19). Kumbuka hili. Kumbuka kuwa mnyenyekevu na mwenye kiasi, ukipima maneno yako kwa uangalifu, sio tu mbele ya MUNGU lakini pia mbele ya wanadamu, kwa maana [hizi] siku ni ovu – siku za usaliti, siku za kiasi, siku za ndoa/harusi zisizo takatifu. Walikuwa wakila na kunywa, wakipeana katika ndoa katika siku za Noa, moja kwa moja hadi hapo gharika lilikuja na kuwaosha wote mbali – jinsi ilivyo huzuni (Mathayo 24:37-39).

Lakini SIjawapa roho ya usingizi na kusinzia, lakini ya upendo, nguvu, na akili timamu/angalifu (2 Timoteo 1:7). Kwa hivyo itumie. Mnafanya vyema Watoto WANGU, mnapofanya kazi za YULE AliYENItuma. Hizi kazi ni kazi za tovuti na za uandaaji kwa ajili ya siku za giza. Hamwezi hata anza kufahamu athari kamili hii itakuwa kwenye dunia, kwenye maisha yenyewe katika hii enzi ya sasa, na bado, lazima iwe, lazima itendeke NInaposongeza vitu kuviregesha kwenye njia sawa.

Naja kuweka vitu katika mpangilio. Hicho ndicho cheo na hali YANGU, wito na kuweko KWANGU. Kwa hivyo, NIsikizeni MIMI, MELEKH TSEDEK wenu, maana NInawapenda. MIMI ni fumbo lakini SIko mbali. NIko karibu nanyi kuliko pumzi yako inayofuata. Nakupa pumzi. Mnaishi, tembea, na kuwa na uzima ndani YANGU kupitia Damu ya MWANAKONDOO – YAHUSHUA MASHIACH wenu ALIYEFUFUKA. (Matendo 17:28)


Mwisho wa Neno

2 views

Recent Posts

See All
bottom of page