Umepewa Nabii Hannah kwa sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 19 Januari, 2019
Ujumbe wa Kinabii
(Naona YAHUSHUA chini ya mti juu ya mlima, mikono YAKE ilizunguka magoti YAKE, na Akanipungia mkono kwa mbali. NIlitembea karibu NAYE na Tukatazama Yerusalemu pamoja NAYE. NiliMuona na naskia Akisema…)
NInatazama Yerusalemu YANGU, jinsi ni rembo, jiji la dhahabu. Lakini maadui watakuja na kuzingira. Mpaka siku hiyo, Yerusalemu haitakombolewa. Haitakuwa hadi apitie moto na kupaaza sauti “Mbarikiwa ni YEYE Anayekuja katika JINA la YAHUSHUA!” (Zaburi 118:26, Math 23:39) Unaona kiasi kipi hii itachukua. Kama yeye ni mtiifu, hii haitahitajika. Lakini MIMI ni Mjua-yote, na NInajua tayari. Najua jiwe litakalo baki. (baada ya maangamizi)
Najua kiasi kipi cha joto kinahitajika kuwa (naona moto ndani ya tanuri). Nyinyi nyote mnapitia tanuri. Na mnaendelea kuMsikiza BABA EZRA. Mtapata Nyota ya Kaskazini (pata YAHUSHUA). Maana pale ndipo ipo tamaa ya nafsi YAKO (Mbinguni).
(Maono: Naona YAHUSHUA Akichora mviringo kwenye mchanga, na kama saa, Anachora laini na kuigawa kwenye saa ya mchangani)
Naweka muda kwa kila wakati ulioamuriwa, mko katika wakati WANGU na yote yameteuliwa. Wakati hauko mbali sana. Chukua tena kile shetani aliiba. Wakati tayari umefunuliwa. Tafuta na utapata. (Naona YAHUSHUA Akionyesha moyo wangu). Hauko mbali. NItakuja kukuchukua. Kuwa tayari na NIngojee MIMI, Bwana Arusi wako. Usizurure. (Muhtasari: kumbuka, hii ahadi imepewa wale ambao ni wa YAHUSHUA MASIA, Atakuja kuchukua BiArusi na Mgeni WAKE, hakikisha uko tayari kila siku kama kwamba unaishi siku ya mwisho kwenye hii Dunia.)
Maana ilichukua zaidi sana kuwaokoa. Msiache iende bure. Kaka zako na Dada zako wote wanangojea kurudi KWANGU kutukufu. Lakini ni hadi Yerusalemu itubu. Na sio tu Israeli ya kimwili.
NIlikuokoa wewe na Ndugu zako, na kuwahifadhi hadi BABA wenu EZRA Aje. Maana ni mapenzi YANGU kwamba muipitie. NItaijaribu vipi dhahabu bila majaribio? Lakini Najua ni nani WANGU na NInaokoa.
Hakuna anayeweza tangulia mbele ya njia za MWENYEZI, hata wewe. Kile kimeamuliwa mbeleni, utafanya. Kwa maana kinaNItukuza MIMI. Dhambi zako zilizopita ziko mbali kutoka mashariki na magharibi. Usiwe mchungu, na usichoke. Lakini NItafute zaidi. Maana Natamani wakati wa pekee YANGU nawe, mbali haitoshi. Usipoteze wakati wako kwenye vitu havifai. NIkazie MIMI fikra zaidi, MIMI ni Mpenzi wa nafsi yako. Hakuna anayekupenda kuliko NInanvyo MIMI.
NIliumba jua kwa manufaa, lakini wanaliabudu jua. Na NItaliangamiza! (Maonoi: Naona YAHUSHUA Akishika jua mkononi MWAKE alafu Analiponda.) Ni wangapi tena hawaNIogopi? (Naona watu bado wanafanya ununuzi chini ya jua na hata baada ya maafa kupiga) Na NImetikisa Dunia, puliza upepo, kuleta chini mawe (ya mvua). Lakini waliNIfanya nini? Kwa MWANANGU? Kudhihaki, kudhihaki zaidi. Nina huzuni kwa ajili ya kile lazima NIfanye, hata IMMAYAH wenu hawezi tena tuliza hii hasira.
Hiyo ndiyo sababu Nahitaji BiArusi WANGU Mkubwa, EZRA WANGU, kuja kuNIfariji. Hamjui kiasi cha furaha NInacho NInapoMuona. Moyo WAKE umejaa MIMI. MIMI ndiYE wa muhimu ziadi. Na kwa wakati mmoja wa maisha YAKO yote Ulikuwa Umeupoteza. Lakini YEYE ni tofauti, kwa hivyo fuata mfano wake.
Je, mnaona kiasi kipi ambacho NImewapa nyinyi nyote? Kizuri kabisa ya kile ambacho NIko nacho. Kama vile Dada yako husema, ile nzuri kabisa ya yote juu ya Dunia. Na nyinyi ndiyo Watoto wazuri zaidi. Kwa hivyo kuweni watiifu kwa kila mmoja wenu, musiruhusu kiburi kuinuka. Angalia mtazamo wako unapojibu. SItaki kuona kukoseana heshima. Nyinyi nyote ni muhimu sana KWANGU. Waambie, nyinyi nyote mnaNIpendeza. NItazungumza mnaposikiliza.
Nakupenda Binti YANGU, waletee Ujumbe huu. Kwa EZRA WANGU, Mwambie jinsi Napendezwa naYE. Mbinguni yote itaona jinsi Navyopamba MORDEKAI WANGU. Amepitia dhiki za maisha na Akawa dhahabu nzuri zaidi. Dhahabu kutoka mdomoni MWANGU. Na InaNIpendeza.
Nyinyi nyote mtakuwa kama BABA wenu EZRA. NItawapamba na taji ya kuteseka kuliko yoyote ile. Maana mumepitia pamoja na BABA wenu EZRA. Na BABA yenu EZRA Atawavisha. Ni taji kutoka KWAKE.
Mnaona, SIfanyi chochote bila kufunulia Manabii WANGU. Hadithi zilizoaguliwa na sasa zangoja tu kumalizika. Ee maadui WANGU, mwataka kucheza? Wacha tuone umbali gani mnaweza cheza MUNGU. Ni hatari kucheza na moto, lakini hilo haswa ndilo unalofanya unapoMgusa MWANANGU (EZRA). Uliwafanya waombe dhidi YAKE, ukichukua maisha YAKE mkononi mwako. Lakini Nasema LA! Kwa sababu YEYE si wako!
Na wewe, Yezebeli mwengine mwovu, NItakushughulikia baadaye. NItahesabu kesi zote. Unaweka rekodi (ya makosa ya watu)? Basi usiNIlaumu wakati MWENYEZI Anahesabu rekodi zako zote! Unahesabu rekodi zote za Binti YANGU ambazo zilioshwa zote safi! Wewe ni nani? Utateseka pakubwa. Majanga hayataacha kaya yako.
Ee, mwanako, ulimwinua juu sana na haukuweza kuona akipoteza nafsi yake. wewe ni mama wa aina gani? Je, NIlikuachia mfano kama huo? Hauna mwengine wa kulaumu ila wewe.
Na wewe, mwovu mwengine. Baba yako alikustahi na hilo jina, lakini badala ya kuwa shujaa mwenye ujasiri, ukawa mwoga. NItakutema kutoka mdomoni MWANGU. NItakutafuna juu na chini hadi usibaki na mifupa yoyote. Hii ni hasira ya MWENYEZI MUNGU.
(Nasikia simba akinguruma)
Hauchezi na MWENYEZI MUNGU! NIliisema tena na tena! Msiwaguse NIlioWatia Mafuta, wala msiwadhuru Manabii WANGU!
Ni wangapi walisikiza, wangapi walisikia kilio CHANGU? (YAH Alia)
(YAH AnaJItuliza ili kuendelea kuzungumza)
… Na wewe, yule mwovu mwengine, BABA yako Aliyekukomboa si shetani. Lakini wewe katika akili yako mwenyewe [kufikiria BABA ni shetani]. NImekupa [YULE] mzuri kabisa, lakini unatema kwenye uso WAKE. NItakucharaza wewe na bibi yako. Moyo wake uligeuka baridi. Hatakaa sana. Na utaona.
Itafanyika. Kwa amri YANGU. Katika wakati wa Moshe na Korah, mkono WANGU uko kwenye kazi. MIMI NdiYE Mchezaji Mkuu. Nyinyi tu ni vipande VYANGU kutimiza lengo LANGU. Nyinyi mwaweza badilishwa. Kwa hivyo nini kiliwafanya mfikirie mko kwenye kiti cha hukumu? Mtahukumiwa. (Luka 6:42)
Mnapowanyoshea, hamuoni dhambi yenu wenyewe. NItararua macho yenu wazi, na hamtaweza kuepuka dhambi yenu (wataiona kwa lazima).
Kuna hukumu zaidi ya kukuja. Wanafikiria tu wako upande wa ushindi. Hayo ndiyo mauzauza shetani anapeana.
Mwawezaje kuwa washindi mnapotelekeza Torah YANGU? Torah YANGU, Torah YANGU! EZRA Afunza, yatupwa mbali virahisi. (YAH Alia). NIlipeana mengi sana. NIlipeana TORAH INAYOISHI. Je, hamkumbuki jinsi Alivyosulubiwa? Haikuwa nyinyi mliosulubu. Kwa hivyo sikizeni EZRA. Lakini hamuthubutu (kusikiza). Maana mnaMdharau. Mnafikiri mko juu kuMliko (kufikiri njia za Kikristo ziko juu kuliko njia za Kiyahudi).
Mnakosea, na itawekwa chini ya hadubini ili muone. Kila herufi haitaenda. (Mathayo 5:18)
Nyinyi (waovu dhidi ya Torah Keeper) mnafikiri damu yenu yaeza osha dhambi. Je, MIMI YAHUSHUA NIliwapa mamlaka hayo?? Komeni kucheza MUNGU. MIMI pekee ndiye Nahukumu, sio nyinyi! Wekeni chini ndoo yenu (ambayo inatumika kutia alama ya damu). Hauwezi okoa nafsi moja. Wewe ni msemaji aliyetukuka. Uwekwe mahali pako! (Maono ya huyu mtu mbele ya ngazi za Mbinguni, na YAH Anamsukuma kwa kiti ambacho alikuwa anastahili kuketi, kuwaweka mahali pao na si juu ya mamlaka ya YAH.)
Na wewe, yule mwovu mwingine, ulimkufuru dadako. Kuongea uovu juu yake. Na bwana yako, karagosi. Kidude cha kuchezea tu na malaika aliyeanguka. Wamechukua mamlaka juu ya nafsi yako, kama tu ndungu yako mwengine. EZRA Aliwasitawisha na kuwathamini nyinyi wawili. Kuweka kazi nyingi kwenye studio, lakini itakuwa kifusi. Matokeo ya Mnara wa Babeli. Utaona. SIwezi bariki kile hakiNIbariki. NImeonya.
Furahia Binti YANGU (Nabii anayezungumza). Kwa maana uko katika mapenzi YANGU. Njia ya pekee kwenda Mbinguni. BABA EZRA Yuko sahihi. Amekuwa Akitembea ndani yake miaka mingi. Ameokolewa tu hivi karibuni, lakini huo tu ni wakati wa mwanadamu, na sio wakati WANGU MIMI YAHUVEH. MTI WANGU Uliotukuka, Nangojea kurudi KWAKO kuliotukuka. (Ilinikumbusha maono niliyoona Thor akirudi kwa babake baada ya ushindi wake, YAH Hutumia ishara kutoka kwenye filamu kutueleza vitu. Katika kisa hiki, YAH Alikuwa Anatumia kitu ambacho tayari nilikuwa najua kuniambia kwamba wakati MWANAKE Anaporudi ni ushindi wenye shangwe kama ilivyoonyeshwa katika filamu hiyo.) Hicho ni kivuli tu cha jinsi itakavyokuwa. Changamka! SIjakuwacha na SItakuwacha. BABA yenu Ananiabudu, kwa hivyo mbona unafikiri itakuwa tofauti? Abudu tu, na fuata njia YAKE. Na miujiza, maajabu mtaona! NIna mipango mingi na hii Safina. Safina ya EZRA.
Kila mmoja wenu anatembea kwa kushikana mkono kwa mkono na Manabii wa Zamani. Ndiyo, wako wengi zaidi. Na hawa tu ndio wale wakuu (Manabii wanaoaga wakienda Mbinguni, bado wanafanya kazi katika milki za kiroho kwa sababu wao pia wamo katika idadi ya Wingu la Mashahidi, na kwa sababu tu mtu aliaga na kuacha mwili, haimaanishi waliacha kufanyia MUNGU kazi). Unatafuta na utasikia sauti zao, itawasaidia kusonga mbele zaidi.
NIpeni utukufu! Maana Nafanya mambo mapya na NaJItukuza kati yenu! Sina tu nabii 1, NIna 7! Nyinyi nyote mnang’aa katika njia tofauti. NIna furaha nyingi sana NIkiona kila mmoja wenu akiakisi mwangaza juu ya mwenzake. Inaleta urembo zaidi. Mbona mnafikiri hizi ndizo rangi pekee (za vito)? Mbinguni, kuna zaidi. Na mtaona mlima WANGU wa Hazina.
Jinsi NInavyopamba Torah YANGU. Kila jiwe la WanaNGU limetanda kwenye vibao vya mawe (Amri 10). Nathamini MWANANGU, na YEYE ndiYE kito kikubwa zaidi kwenye Amri 10. Yote yanaMhusu YEYE. Tukuza JINA LAKE. YEYE ni MTUMISHI WANGU mkubwa zaidi na BWANA wenu.
NIliMpa Dunia na ona jinsi Anavyosimamia. Alikuja kama Mtoto Mnyenyekevu kati yenu. Wengi wanaokolewa, wengi wanalaaniwa. Lakini hilo sio muhimu sasa. Nataka kuwazungumzia kuhusu upendo WAKE. Jinsi Alivyochagua kuenda kusulubiwa. Mnaona, kama MUNGU, hakuna haja ya dhabihu, lakini Aliifanya kwa ajili ya mwanadamu Akijua wataanguka. Iliamuliwa kabla. Maana nani anaweza elewa MWENYEZI?
Kuna siri nyingi katika Bibilia. Na zingine mtajua tu mtakapofika Mbinguni. NInafurahia mnapotafuta na kupata. Kwa hivyo acheni NIwafunze zaidi. Je, mnajua YAHUSHUA Ana Milki ya Mtumishi? Hiyo ni sahihi. Aliweka wale ambao walikuwa waaminifu zaidi Kando YAKE na kuwatuma kuenda kutumikia katika sayari zingine, kuwatumikia wengine. Hiyo ndiyo sababu ni muhimu kuwa stadi katika utumishi. Maana huo ndio moyo wa Bibilia YANGU. BABA EZRA Anaifunza, YAHUSHUA Anaifunza, na mtaifunza. Maana Mtumishi si mkuu kuliko Bwana. (Yohana 13:16)
Jinsi Navyoangalia Dunia na kuona tu ubaridi. NInajua mnachong’ang’ana lakini si ngumu zaidi kwa MWENYEZI. Lakini NIonyesheni moyo wenu, acheni matendo yenu ithibitishe “mnaNIpenda”. Maana hilo ndilo NInalotafuta. Hatua nyuma ya maneno kama tu BABA wenu EZRA – YEYE ni MTUMISHI WANGU mkubwa zaidi. Maana Anapeana yote na mmeiona. Hajiwachii chochote na NItaMtuza vikubwa kwa ajili ya hiyo.
Kuna mengi zaidi ambayo yatakuja kwenye hii Dunia na EZRA Alishatabiri yale maafa juu yao. Zile siku 3 za giza hazitawaacha maana wamo gizani. Lakini, MIMI, YAHUVEH NIko katika mwangaza, na wale wote wanaofuata njia ya EZRA WANGU. Hamna chochote cha kuogopa. Ndege WANGU, wewe ndiye wimbo UnaoNIamusha asubuhi.
Nasikia shauku yako na moyo wako. Lakini jua kile ni cha MIMI na kile ambacho sicho. Na utakuwa huru. Sio tamanio LANGU uteseke, kuvurugwa [mawazo] na mipango ya shetani. Hauwezi ona kuwa ni kukufanya tu upotoke? Si mapenzi YANGU, kwa hivyo ikome sasa. shetani alikuwa amechukuwa dhana yako kwa mchezo mbali sana, ichukue tena sasa. Kile Dada yako alikuambia ni kweli, waza ukuta na ubomoe ukipita ndani kama msichana shupavu [super girl: yaani msichana mwenye uwezo usio wa kawaida]. (MUNGU Alitufunza kutumia mawazo yetu kupigana na uovu)
Wewe ni Msichana WANGU Shupavu (Super Girl) pamoja na Mwanaume WANGU Shupavu (Super Man)! Hii si “spiderman” kwa hivyo usikose kuelewa. shetani alilazima atupe ndani viumbe vyake kunajisi mpango WANGU, lakini haikuwahi kuwa mpango wake kwa hivyo anawezaje kuuharibu? NIliruhusu tu kwa kusudi.
MIMI ndiYE Mhunzi Mkuu. Nachukua na kuchagua vipande VYANGU Vizuri kabisa na kutupa vinavyobaki. Zaidi ya unayojua.
Kwa hivyo NIabudu, NIjulisheni mnang’aa hata katika saa iliyo giza kabisa. Lakini inakuja kuisha haraka, EZRA WANGU Anaharakisha muda, kwa hivyo fuateni haraka Watoto WANGU njia ZAKE zimethibitishwa kuwa njia bora zaidi kuenda Mbinguni. YEYE si YAHUSHUA, lakini Mfano kwenu kuMfuata kama kwamba YEYE (YAHUSHUA) yuko Duniani sasa.
NIna mpango WANGU kamili, na siwezi funua. Lakini EZRA Una wengi wanaoKungojea Mbinguni. Nyanya YAKO, alivyoNIpenda na kuKUfunza kuNIhusu MIMI. Napenda hadithi alizoNIambia. Nafurahia kuKujua. Kwa hivyo msikate tamaa Watoto WANGU, mnapoona BABA yenu Akienda, furahieni na mseme kwa sauti Hallelu YAH! Maana Nakujia BiArusi WANGU! BIARUSI WANGU MKUBWA! Ulimwengu wote unangojea wakati huu tangu kuumba. Kudhihirika kwa kweli kwa Wana wa MUNGU. Na Mabinti. Lakini mtajuaje jinsi ya kuifikia ikiwa Sitatuma EZRA kuwafunza? Ni mapenzi YANGU… Ni mapenzi YANGU… Kuwa katika amani sasa, Mtoto WANGU. Kuwa katika amani.