Unabii 31 “Je, Mnasikia Sauti ya Hatua ZANGU Watoto WANGU?”
Updated: Mar 21
Umepewa Nabii Shimshon kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 12 Aprili, 2019
Ujumbe wa Kinabii
Je, mnasikia sauti ya hatua ZANGU Watoto WANGU? NInapotembea kwenye sakafu ya akili zenu. Katika ususu wa mioyo yenu. NIlipokuwa Natembea katika Bustani ya Edeni, walisikia sauti ya hatua ZANGU. Nawaambia, tembeeni NAMI! Nasema, mko wapi? WanaNGU, Mabinti WANGU, m’wapi?
Msiwe kama Adamu, alivyojificha na Eva alijificha Nilipowaita, maana walijificha kwa sababu walikuwa wameabika. Kwa sababu walitenda dhambi, walivunja Amri YANGU. Na walitaka tu kujificha. Na NIlimwambia, “Je, ulikula tunda la mti ambao NIlikanya?”
Kwa hivyo sikieni sauti ya hatua ZANGU siku hii. NInatembea katika bustani ya mioyo yenu. Bustani ya akili zenu. Pale ambapo pamepandwa mti wa ujuzi wa mema na maovu. Na Nawapa Amri iyo hiyo. NIliwapa Amri iyo hiyo! Hamtakula kwa huo mti, tunda la huo mti. Na NInaangalia na NImeangalia kila mmoja wenu. Katika njia moja au nyingine, nyinyi nyote mlikula kwa huo mti.
Halafu yaja hadithi ya Wokovu. MIMI, YESHUA, NIlishuka kutoka Mbinguni hadi duniani. Katika Utukufu WANGU wote. Kwa mwili wa mtoto mchanga mdogo. Na NIlikuwa miongoni mwa wanadamu. NIlikuwa Mwana wa seremala. Macho ya dunia yalikuwa yamekaziwa wakuu, wenye nguvu, mashuhuri, wenye ulumbi, matajiri, wenye uwezo na hawakujua kuwa MUNGU Alikuwa katikati yao; katika umbo la mwana wa seremala. Halafu Utukufu WANGU ukafunuliwa.
NIlitunduwaza dunia. Oh, waliNIchukia, waliNIchukia, waliNIchukia. Na umaarufu ulienea lakini je, mlijua Sikujali umaarufu? NItaenda kutunza wale BABANGU AliNIamini kuwalazia chini maisha YANGU. Kulaza maisha YANGU chini ili wengi waweze kuokolewa.
Na NIlilaza chini maisha YANGU kwenye huo msalaba na NIlimwaga damu YANGU – kwa maana MUNGU jinsi Aliupenda ulimwengu hadi AKATOA MWANAWE wa Pekee, MWANAWE Mzaliwa.
Na NIlikufa na NIkafufuka tena. Kwa ajili ya wote wanaoNIamini na kwa hakika wanaweka matendo nyuma ya imani yao, wanapotubu na kugeuka kutoka kwa dhambi. Halafu NIkapanda Mti WANGU wa uhai na NIkasema “kula", pale ambapo NIliwakanya mti wa ujuzi. Nawaambia nyinyi nyote, “kula"! Kuleni Tunda LANGU na muishi! Acheni NIng'oe kwa mizizi mti wa ujuzi wa mema na maovu. NIruhusuni NIlaze shoka kwenye mizizi.
Na mnapotubu, na mnapokiri mapambano na wenzenu, dhambi – hiyo ni kama kukata mzizi wa mti. Na ule ambao unaanguka unakuwa mti mpya, maana huo Mti wa Uhai unatoa matunda kama vile uhushuhuda wenu. Maana Natumia ushuhuda wenu wa MIMI. Natumia ushuhuda wenu wa pale m'mekuwa kumwaga uhai WANGU juu ya wale wanaowasikia.
Njooni KWANGU, WATOTO WANGU, njooni KWANGU, njooni KWANGU, na acheni NIwashike kwenye kifua CHANGU. Acheni NIwapapase [kwa mahaba], acheni NIwakumbushe nyinyi ni nani na MIMI ni NANI! NIruhusuni NIng'oe kwa mizizi yote yanayowaletea woga. Kila wahaka, kila aibu, NIruhusuni. NIlikuwa Mwana wa seremala. Najua jinsi ya kubomoa na jinsi ya kujenga. Mnafikiri kwa nini BABANGU wa Mbinguni Alichagua seremala kama baba WANGU wa duniani. MIMI, YESHUA, NIlijua kile NIngefanya. Kwamba NIngebomoa na kujenga.
Je, mlijua hili? Baba YANGU wa duniani, alikuwa mkulima wa bustani? AliNIfunza vitu vingi sana. Mnafikiri vipi NIlijifunza mengi sana na NIlizungumza katika mafumbo? Ya yale ambayo NIlijua. Yosefu, baba YANGU, baba WANGU wa duniani, alibeba tabia nyingi sana za BABA wa Mbinguni. Alichaguliwa MIMI. BABANGU wa Mbinguni Alijua pale pa kuNIweka, kama vile tu Najua pale pa kuwaweka Watoto WANGU. Na NImewapa BABA Asiye kama mwingine!
Na Yosefu anakuja KWAKE, sio tu kuMsaidia – BABA wenu EZRA -lakini pia kujifunza kutoka KWAKE. Kuwa Baba hakukomi hapa duniani, unaendelea milele. Jifunzeni kutoka KWAKE, jifunzeni kutoka KWAKE. Maana Anawapenda sana. Alikuwa tu kama baba YANGU wa duniani. YEYE ni kama tu BABANGU wa Mbinguni.
Yosefu AliNIfunza MIMI, YESHUA nidhamu. Mnafikiri ilikuwa rahisi kulea MWANA wa MUNGU? Yosefu aliNIfunza jinsi ya kufanya kazi kwa bidii. Jinsi ya kuwa mwana biashara. Jinsi ya kufanya kazi kwa bidii na mikono YANGU. Yosefu aliNIfunza Torah. Nyinyi Watoto WANGU mko chini ya funzo lilo hilo ambalo MIMI, YESHUA, NIlikuwa juu yake wakati NIlikuwa duniani. Na ndiyo, Nafunza EZRA kile pia MIMI NIlifunzwa. Kwa hivyo, jifunzeni haraka, jifunzeni haraka. Namwaga neema YANGU, rehema YANGU juu yenu, lakini jifunzeni haraka hakuna muda mwingi uliobaki! NIlisema kuweni wazi.
Kutafuta viini vya moyo wenu. Ikiwa hamjui pale kipo, NIulize MIMI, YESHUA, kwa vile wengine wenu hamjakuwa mnafanya hili, maana hamkupenda kile mliona. Mnafikiri Napenda kile Naona?
Nataka kusafisha! Hilo ndilo MIMI hufanya! Nasafisha machafuko, NIruhusu, NIruhusu, NIruhusu, NIruhusu kuosha miguu yenu! NIruhusuni kuosha miguu yenu! Ikiwa huNIrusu kuosha miguu yako, hilo linaonyesha huNIruhusu kuosha na kusafisha moyo wako! Je, unapokea kemeo ZANGU? Je, unapokea marekebisho YANGU? Nayasema haya kwa kila mmoja wenu! Kwenu nyinyi nyote! Kila Unabii ni Maneno YANGU, Maneno YANGU! Na jinsi unajua, choma hadi kwenye nafsi? Je, mwili unajikunyata? Je, unaanguka kwa uso wako? Je, unanyenyekezwa? Je, mwili unainuka?
Haya ni Maneno YANGU! Maneno YANGU ni Uhai! Kali kuliko upanga wenye makali mawili, yakigawanya nafsi na roho, yakichambua fikra, hata zile kusudi za roho. Shaka -Naiona! Woga – Nauona! Tamaa – Naiona! Uasi – Nauona! Chuki – Naiona! Husuda – Nauona! Wahaka – Nauona! Mkijaribu kuficha, Napiga teke milango wazi! Mkijaribu kuzika, Naichimbua!
Nyumba YANGU! Ni nyumba YANGU! NInafunga [yule] mtu mwenye nguvu! Na kupora [hiyo] nyumba. NInatoa yote ambayo hayaNIpendezi. Nawaambia nini lingine Naona – upendo unaokua. Naona huruma YANGU. Naona Amani YANGU. NInatamani mbaki hapo, mkae hapo, muingie katika pumziko LANGU. Naona shukrani YANGU. Lakini Nawaambia hili, kwa nini Nawafunulia kile kiko moyoni?
Nawaambia, ni kama Bustani ya Edeni, mti wa ujuzi ya uovu na uzuri na Mti wa Uhai. NIruhusuni NImalize [hiyo] kazi nzuri. NIruhusuni NIfanye [hiyo] kazi. Kwa maana, Sikusema, nyakati zote Nafanya kazi? BABANGU nyakati zote Anafanya kazi. NIruhusuni, NIruhusuni, NIruhusuni, NIruhusuni! Nina hasa toa upanga wenye ncha mbili pole pole, NInaupitisha moyoni mwako. Inakaa enye vurugu, lakini ufalme wa giza utateseka vurugu, chochote kilicho gizani, lakini Nayafanya kutokana na upendo. Naweka mkono mmoja kwenye bega lako, huo mkono mwingine unashikilia upanga wenye ncha mbili. Na NInausukuma katika moyo wako. Na unatoka nje huo upande mwingine. Hii ndiyo maana unahukumiwa [moyoni mwako]. Hii ndio maana unadungwa hadi kwenye nafsi. Nina kwa uhalisi dunga nafsi yako kutokana na upendo. NIlifanyia lilo hilo mama YANGU duniani, kwa mama YANGU Miriam! NIlichukua upanga wenye ncha mbili na NIkadunga nafsi yake. NIlikuwa na maneno ya kemeo kwake pia. NIlijua NIlikuwa nani! Na MIMI ni Nani!
Na [Miriam] alisema, “Najua huyu MWANA wangu, ni MWANA wa MUNGU! Sikutarajia hili! MWANA wangu mwenyewe kuniangalia kwa uso na kuzungumza maneno yanayopunguza mwili wangu kuwa jivu, ambayo yatadunga nafsi yangu.” Hiyo ndiyo maana Mama YANGU yuko Mbinguni. Ilimbidi aNIsikie, ilimbidi asikilize, ilimbidi atii, ilimbidi aNIpokee! NIlimwonya, kama vile WEWE EZRA Ulionya mama YAKO. Na anashangaa, “ni MWANA aina gani ambaYE niko naye? Huyu si MWANA wa kawaida! Ni nini kilichotoka ndani yangu?” Rehema YANGU iko juu yake, neema YANGU. Natamani kumuepusha [katika] Siku 3 za Giza. Malaika WANGU wanafanya ovataimu naye. Kwa nini? Kwa sababu YAKO EZRA. Kwa sababu ya maombi YAKO. EZRA, Unachosema Nafanya, kwa sababu chochote Nachosema, Unafanya.
Ukiuliza hilo, basi Siku 3 za Giza zitashuka. Nakupenda EZRA. Nakupenda. Nakupenda EZRA. Nakupenda. Kwa sababu tu Ulionya, NItafanya. Unaona EZRA WANGU. EZRA Mtamu. MIMI, YESHUA, Nasema, WEWE ni Mtamu! Hata watu milioni waombe, “BWANA, Usiruhusu hili lije!” Kwa sababu WEWE EZRA Ulilizungumza, litatendeka. Mwaona fadhila? Mnaona fadhila mnayo naMI? Mmoja wenu akizungumza, ni kama mlipuko ulitukia, kwa hivyo Naruhusu sauti na Mbinguni yote yageuza sikio lao na kusema, wote walizungumza, “Acha tusikize, acha tujifunze.”
Maana Nawaambia Watoto WANGU, pamoja na kila neno linalosemwa, unapofungua mdomo wako kuzungumza, kuna safu za ufunuo ambazo zinaenda katika nafsi yako. Hilo hamjui. Kuna ufunuo ambao uanenda juu Mbinguni, kama Wingu la Mashahidi wanaangalia na kusema, “Abwe!”Ni zaidi ya neno tu, ni uhai. Ni uhai wa milele. Kwa hivyo NInaangalia mioyoni mwenu, na NInasema, “Fungua mlango.” Chochote mmezika, chimbua. Msiache MIMI, YESHUA, NIlazimike kufanya hii kazi – ifanye iwe rahisi KWANGU. Ifanyeni iwe rahisi KWANGU, watoto WANGU. Na hii inafanyika katika uwazi, hii inafanyika katika toba. Zaidi ya mnavyokuwa wazi, zaidi ya mko radhi kukiri dhambi zenu, zaidi ya hamuruhusu mwili kuinuka, zaidi ya mnavyoharakisha muda ambao Naweza tumia mdomo wenu, ambao naweza safisha moyo.
Macho YANGU yanaenda mbele na nyuma. Juu na chini. Mnafikiri MIMI sionekani tu? [Mnasema] “YESHUA, nisaidie siku hii yote!” bila kutambua kabisa… Mnafikiri mbona Naendelea kusema, “Niko karibu kuliko pumzi yako ifuatayo?” Hata ingawa Sionekani kwa macho yako ya mwili, kila kitu ni wazi KWANGU! Mara nyingine mko kama watoto wadogo wanaocheza ‘kibe [mchezo wa kujificha na kutafuta]. Unafunika tu macho yako ukifikiri kwamba kwa hakika unajificha. Halafu Naja NIkitafuta. Nakuona pale pale katika wazi na macho yako yamefunikwa. Ukidanganya kuwa kwa hakika umejificha kama tu mtoto mdogo. Na unashangaa NInapokupata. Unashangaa na kusema, “YESHUA kwa kweli Waona vitu vyote?!” Na bado Natikisa kichwa CHANGU na kusema, “Haikuwa ngumu kuona kutoka kwa huu mtazamo.”
Jificheni huku Watoto WANGU, jificheni ndani YANGU, chini ya kinga ya mbawa ZANGU, chini ya uvuli wa MWENYEZI na mtapata pumziko la nafsi zenu. NItawaokoa na mtego wa mwindaji, na tauni ya kutia kinyaa na hamtaogopa vitisho vya usiku, wala tauni iharibuyo adhuhuri, Na hamtakuwa kama wale walio katika ufalme wa giza katika siku watakayoanguka na wafu kote kando yenu, ila mtaona tu kwa macho yenu malipo ya wasiotenda haki (Zaburi 91:4-8).
Kazeni tu upendo wenu juu YANGU na NItaokoa.
NItawachukua juu kwa sababu mmelijua JINA LANGU. NIIteni na NItawaitikia na NItakuwa nanyi katika taabu. NItawakoa na kuwatukuza. Na NItawashibisha na maisha marefu na kuwafunulia wokovu WANGU (Yeshua) (Zaburi 91:14-16). Lakini inaanza na jinsi mnavyoamini! Je, mnaNIamini (Waebrania 11:6)? Hata nabii anayezungumza?!
Ingieni katika pumziko LANGU. Ingieni ndani. Shukrani na Sifa! Je, hamuiingii katika nyua ZANGU hivi (Zaburi 100:4)? Katika nyua ZANGU kuna pumziko, kwa maana hapo ni mahali pa kupumzika. Kwa maana mnasimama mbele za NDIMI NILIYE MKUU, MIMI YEHOVAH, na shukrani. Nataka msifu zaidi! Nataka mpeane shukrani zaidi! Na oneni jinsi Navyokamilisha [ile] kazi nzuri NImeanza ndani yenu.