Unabii 37 "Ee Israeli, Marekani na Dunia, Vita vi Karibu!” |Unabii wa Kikundi
Updated: Mar 21
Umepewa Manabii kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 19 Mei, 2019
Muhtasari
BWANA Ametutia mafuta sisi manabii kadhaa kuamsha upako ndani ya wenzetu. Kuna mara nyingi ambapo mmoja anatabiri, halafu BWANA Anaambia mtu afuataye kuendelea kutabiri. Na huu unabii ulikuja tu vivyo hivyo.
Ujumbe wa Kinabii
Njooni juu zaidi. Watoto WANGU njooni juu zaidi. Hata kaeni karibu NAMI, MIMI URIYAH (Bofya kwenye mstari ujue URIYAH ni nani). MIMI ni mkufunzi wenu wa muziki, mwalimu wenu wa muziki. Je, kwani SIjaMpa EZRA fimbo ya kifalme? Na Alikuwa Ameishika na kuitumia. Alikuwa Anawafunza nyinyi nyote jinsi ya kuwa katika uzalishaji WETU. Katika kila ndimi zenu kuna hata noti za muziki, mkiimba, ulizeni kuiimba, mnajua. Mnafikiri ni nani, mbona mnafikiri Wayahudi wanaimba Maandiko? Sio tu kuchanti lakini kuimba nyakati zingine. Imejawa na utukufu. Utukufu mkuu. Kwa hivyo oneni kile wakati ujao unawaonea, Watoto. Kwa maana TUmewaambia wazi, pale imani yenu ipo Pasaka itakuwa.
Kwa kile NInawapa, nguvu za mpigo wa nuklia ndani yenu, ndani ya kila mmoja wenu. Mtahisi huo moto mnapoamini. Kwa hivyo acheni huu moto, huu moto uendeleao bila kukoma, huu mviringo wa moto usiwahi zima. Lakini Mviringo wa Moto [muhtasari: eneo ambalo lina mitetemeko ya ardhi na milipuko ya volkano mingi] Maana yaja upesi. Mtaona. Ikiwa Hukumu itakawia. Ikiwa watu wa kutosha, ikiwa wa kutosha kama Nineve wataomba itacheleweshwa. Ombeeni ulinzi wa Donald J. Trump, msipuuze hili, maana wakati ujao wa Marekani angalau sehemu ya wakati ujao umeidhinishwa katika huyu mtu.
Na ndani ya huyu mwanamme, rais mwadilifu wa mwisho katika historia ya Marekani. Kwa maana umeona Marekani na hata dunia nzima? Hata na sheria ya Taiwan ya karibuni, ndoa ya jinsia moja, ambayo iko nje ya mapenzi YANGU? Wameondoka kwa njia YANGU na amri ZANGU na katiba YANGU. Kwa hivyo wataenda mbali zaidi. Maana kazi ya toba huleta uhai wa milele.
Kwa hivyo kuweni kwa amani, siku hii. Na mjue Maneno YETU yote ni kweli, Maneno YETU yote ni kweli. Ee jinsi Navyopenda wakati manabii WANGU wanazungumza, mmoja baada ya mwingine, baada ya upako ulipoanza kama moto wa chamchela.
Muda ni mfupi, muda ni mfupi, Wanafunzi WANGU. Muda ni mfupi. Muda ni mfupi. Vitu vichache tu zaidi vyakufanya. Muda ni mfupi. Kwa maana kama vile chamchela inachukua kila kitu katika njia, ghafla bin vuu NItakuja maana kisasi ni CHANGU! (Hadi) kwamba huu ulimwengu haukutarajia! NItawakumbo! Pia kwao. New York, NItakukumbo. Kwa maana unaNIdhihaki! Mchana na usiku! Mchana na usiku mnadhihaki NDIMI NILIYE MKUU!
Israeli, Israeli WANGU, sikizeni Neno LANGU! Pale ambapo NInawatumia Nabii WANGU mwengine kuwaonya; kwa miaka mingi Natuma Manabii WANGU kwenu ili [m]tubu! Na mNIfuate kama vile mababu wenu walifanya! NItumikieni kama mababu wenu Abrahamu, Isaka na Yakobo! Kwa maana walikuwa watumishi waaminifu. Njooni KWANGU kama Mfalme wenu Daudi na moyo wa toba. Maana Mfalme WANGU Daudi alijua jinsi ya kujinyenyekeza. Na Nawataka, Israeli WANGU, Yerusalemu WANGU kujinyenyekeza na mNIombe huruma. Kwa maana NImekuwa mvumilivu kwa miaka mingi, maana nyinyi sio kama mababu wenu. Walijua na moja kwa moja walitubu kila wakati walijua wametenda dhambi dhidi YANGU.
Lakini nyinyi sasa, mnafunika masikio yenu na hamtaki kusikia maneno YANGU. Kwa sababu saa hii mnaona ulimwengu mzima, na mnataka kufuata baada ya huu ulimwengu. Yerusalemu YANGU, Torah YANGU, Torah YANGU inang'aa katika Yerusalemu hadi mataifa yote hadi dunia nzima. Na kwa nini, kwa nini Yerusalemu, kwa nini hauangalii Torah YANGU na moyo wako tena? Mbona tu unakariri Torah YANGU na midomo yako na sio moyo wako? Kwa nini Yerusalemu WANGU? Maana Natuma Mana iishiyo toka Mbinguni kukulisha! NInakuongelesha Israeli WANGU, Yerusalemu WANGU, MIMI ELOHIM wako! MIMI- EL SHADDAI! NInawaita Israeli na Yerusalemu, kwa maana mnapaswa kuwa mwangaza kwa mataifa. Mnafaa kung'aa kama nyota angavu Mbinguni! Maana Nawatumia Torah Iishiyo. Fungueni macho yenu! Fungueni moyo wenu! Na mruhusu MASHIACH wenu AliYEahidiwa, AliYEtiwa mafuta – Mruhusu! Ruhusuni ZAWADI Kuu kabisa, kwa maana YEYE sio hivyo vitabu, YEYE sio hizo kurasa. YEYE ni Torah, YEYE ni Torah Iishiyo, Israeli WANGU, Yerusalemu WANGU.
Pokeeni. Pokeeni, pokeeni YESHUA kama MASHIACH wenu! Na komeni, komeni kufikiri kwamba YEYE ni MUNGU wa Wakristo. Kwa maana NImechoka kuona hilo! Kuona kwamba mnafikiria hivyo. Kwa maana mnajua MASHIACH wenu Hatavunja amri ZANGU. Nataka mjue kwamba ni watu wanaohadaiwa n shetani kuvunja Amri ZANGU, kugeuza Neno LANGU kupatana na taswira ya mwanadamu. Nawaambia Yerusalemu, kwamba mnashindwa kuona wazo kuu [ambalo Najaribu kuwaonyesha]! Kwa maana Nawatumia manabii tena na tena na tena kuwaonya mpokee YESHUA kama MASHIACH wenu kabla kuwe kumechelewa tayari. Pokeeni zawadi ya Wokovu. Mpokeeni siku hii. Maana muda ni mfupi. Watu WANGU, muda ni mfupi.
Muda ni mfupi. Marekani mko kwenye ukingo wa vita. Urusi itawavamia. China itawavamia. Hata Japani ndogo. Watatuma makombora dhidi yenu. Msidhani wameng'olewa uwezo wao wote. Kwa maana wanajenga kitu ndani, kindani. Korea ya Kaskazini iko dhidi yenu vikuu, Marekani WANGU. Mmesahau tamaduni (za) mababu. Misingi mmesahau.
Ee Marekani, ni kweli. Mko kwenye ukingo wa vita. Angalieni hatua yenu inayofuata! Kwa maana itakuwa yenu ya mwisho! Mabohari ya makombora yenu yamefichuliwa, pale wanataka kuvamia. Na NItakuwa na kicheko cha mwisho ikiwa hamtageuka. Kwa maana NImeonya na NImeonya. Mwaka baada ya mwaka na hamjasikiliza. Ni lini mtarudi KWANGU? Ili NIwasanye kwa mikono YANGU ya upendo? Lakini hamNItaki kabisa. Tabia ya kupenda kucheza na hatari hadi karibu yake kabisa! Shikilieni kwa nguvu, Marekani. Kwa maana NImehifadhia mwisho mabaya zaidi. Hukumu yenu imekuja.
Marekani, hii ni nafasi yenu ya mwisho. SIjali watasema nini. Rudini! Na muunge rais wenu mkono (Donald J. Trump)! Kwa maana hii kweli ni nafasi yenu ya mwisho. Okoeni watoto, tupeni nje uavya mimba! Na mchukue hatua za toba! Labda NItaepusha wengi, watu wachache watakufa mnapotikisa damu kutoka kwa mikono yenu. Hamjasikiza mababu wenu wenyewe ambao waliwawekea misingi, na [wa]lijua MUUMBA Yupo. Lakini mliwatupa nje pia. Na sasa NImemalizana nanyi. Kwa maana nyinyi ni kama mtoto aliyetendekezwa sana, kama mtoto mchanga anayetikisa ngumi yake kwa uso WANGU. Umetosha mchezo wenu wa kitoto! Kwa maana huu kweli ni mwisho wenu. Na wanawajia kwa vitisho, hata maadui wenu, jinsi wanavyowazingira! Kutoka Venezuela watakuja na hiyo ni sehemu moja tu ya uzinduzi. Makombora yatakuja! Miji yenu itavunjwa! Uharibifu utakuja!
Joel Osteen, hawa ndio aina ya watu ambao wamejaza makanisa yenu ambao mmesikiza (watu wa Marekani wamesikiza watu kama Joel Osteen)! Hakuna Utakatifu katika nchi! Na hakuna Utakatifu katika nchi! Na SIwezi waepusha bila toba ya kweli! Binti wangu mpotovu, ni heri utubu sasa! Kwa maana muda uko karibu kuisha! Na hakuna tena maonyo mengine zaidi! Utengano utakuja! Maana MIMI MWENYEWE NItawagawanya! Hata NInapofanya hivyo, hakuna kukoma. Uharibifu kutoka kwa bahari, na merikebu itatua kwenye pwani yako. Wanajeshi watakutana na ardhi yako, pwani yako, fuo zako. Wataua, teka nyara watu wako, ni Mamluki wakatili. Hawatakoma kwa lolote kumpora, binti WANGU mpotovu. Maana hiyo ndiyo hukumu kama hauishi Vitakatifu. Maana MIMI YEHOVAH pekee YANGU HUITA VITA! Na MIMI YEHOVAH pekee YANGU HUKOMESHA VITA! Na mmeita vita dhidi YANGU! Vita dhidi ya watoto WANGU! Na hili halitawahi simama! HamNIchochi Machoni MWANGU na msitarajie kwamba SItaJIpigania! Na ku[wa]chocha pia! Maana ni hilo ndilo NInalohitaji kuwachocha pia! Kila kitu kinasambaratika! Kwa maana MIMI NI MWENYEZI MUNGU! YEHOVAH! YESHUA! Na Nastahili heshima! Mnapaswa kuinamisha magoti yenu KWANGU. NImewapa kwa upendo muda wa kutubu. Na kuendeleza muda baada ya muda baada ya muda. Tuma mhubiri baada ya mhubiri. Wale waliokuwa wa kweli. Na iwapi toba?
Angalieni kinachoendelea na shule zenu! Na vipi mnafikiria NItaruhusu msimamo huu? Kuenda na wanaogeuza jinsia na halafu kufunza watoto kuhusu ushoga! Hili ni chukizo machoni MWANGU! Unajisi wa umaasumu unapokea hukumu kuu kabisa! Maana ukigusa watoto WANGU wadogo, hii inaleta adhabu kubwa kabisa! Kwa hakika NImekasirika!
Ndiyo, Mwanangu, unapongojea zamu yako, ulihisi na uliona na ulisikia Neno la Israeli. HUYU ni MIMI, ABBA wako YEHOVAH na NInanena na Binti WANGU Mpotovu. NIlituma MWANANGU Israeli, mwale mng’avu uwakao wa Upendo wa Milele. Lakini wanaMgeuzia uso wao, bado NIlijua hawataMpokea wakati huo, badala yake Alilaza maisha YAKE chini, na kumwaga upendo WAKE. Na katika kaburi hilo mwili WAKE ulilala lakini baada ya siku 3, Alifufuka. Na YUYO HUYO YESHUA, YUYO HUYO MASIA Yuaja hivi karibuni. Kuwa tu na imani kuamini, kuwa na imani na uamini! Kwa maana ni kweli, pale Imani yako ipo Pasaka yako itakuwa. Pale moyo wako upo, hapo ndipo hazina yako ipo. Kwa maana hiyo ni hazina [kuwa] NAMI, hapo ndio moyo wako utapatikana. Kwa hivyo usiruhusu vikengeusha fikra.
Kwa hivyo Israeli, Nakupa onyo kuu. NIshanena damu itatiririka hadi kwenye hatamu ya farasi. Ni heri ujisawazishe NAMI, Binti YANGU. Maana kuna vita vinakuja. Imefichika kwa macho yako, lakini sio kwa Manabii WANGU, sio kwa mitume WANGU, sio mwinjilisti WANGU, Wachungaji WANGU, wahubiri WANGU, walimu WANGU, kwa wale ambao wanakazia kwa bidii kusikia sauti YANGU. NImefunua na NItafunua asili ya hivi vita!
Maana ingawa Israeli unalilia Masia, vilio vyako ni vya nia iliyo najisi. Kwa maana hamkuMlilia MWANANGU kurudi, mnalia ni kama Hakuwahi kuja. Na NItawahukumu kwa hili. Hiyo ndiyo maana mpinga-Mashiakh anakuja. Maana mtapokea yule anayekuja na jina lake mwenyewe, kwa sababu mnaMkana YULE AnaYEkuja katika JINA LANGU, JINA LANGU MIMI YEHOVAH. Kwa hivyo someni na mlie, watoto WANGU, watoto WANGU wapotovu. Someni maandiko yenu na mlie. Kwa maana theluthi mbili watamalizwa usiku. (Zekaria 13:8) Ghafla, kufumba na kufumbua. Uharibifu wa ghafla utakuja. Lakini hakuna ulinzi wa Zaburi 91, kwa maana ukikana Neno Lililohai, unakana Neno Lililoandikwa. NItakuwa na huruma kwa yule ambaye NItakuwa na huruma, NItamwaga ghadhabu YANGU kwa yule ambaye NItamwagia ghadhabu YANGU. Kwa yule ambaye upanga wenye ncha mbili umekusudiwa kuangukia, wataangamizwa kabisa. Kwa wale ambao watarithi njaa na uharibifu, watainamisha goti, na kuliwa wakiwa hai.
Siku za huzuni, majaribio ya huzuni. Siku za angamizo na majonzi. Lakini kuna matumaini, lakini ikiwa tu mtaNItumainia, MIMI YESHUA. MnapoNIkana, hamna matumaini. Maana ni vipi Naweza heshimu waasi? Hii ndiyo maana Israeli, o Yuda, majonzi mengi yamekuangukia tangu wakati NIlipaa juu. Kwa sababu mnaNIkana. Mlikubali kushindwa na uongo wa Wafarisayo. Mligeuka njia ya Masadukayo. Mnafuata njia ya Balaamu, nyinyi mko KWANGU kama Kaini.
Lakini NItasafisha kwa kutoa waasi wa nchi. Kupitia majaribio na kazi nyingi na chungu. NItasafisha nchi. Nchi ambayo Damu ya MWANANGU ilimwagwa kwa ushindi. Kwa maana Hakufa katika ushinde, Alikufa katika utiifu KWANGU. Kwa maana Hakusema, hii Amri Alipata kutoka kwa BABAKE kuweka chini uhai WAKE? Alikuja kuhubiri mwaka na msimu wa Jubilii kuachilia huru mateka, kufungua macho ya vipofu, kuwapa moyo laini kwa wale wenye moyo mgumu; kwa wale ambao wangepokea na kuamini kwamba yule MWANA Anaweka huru ni huru kweli. Lakini Israeli, NItakapopuliza pumzi YANGU ya moto, mwaka wa kisasi utaanza, maana MWANANGU Hakuja mara ya kwanza kuachilia hilo, lakini Alikuja kupeana Wokovu. Na ingawa mnaMtukana na kudhihaki Maneno na Mafumbo YAKE, hadithi ZAKE za Ukweli na Ufunuo, bado NIna huruma. Bado NInaamua kuonyesha Neema YANGU. Maana bado haikuwa wakati wa kufungua mhuri kwenye hati-kunjo ya Ufunuo. Katika kitabu cha Ufunuo NInazungumzia.
Lakini – mhuri zimevunjwa. Hati-kunjo zimefunguliwa. Wakati u karibu, wakati u karibu sana, wakati uko hapa. Maana SIkusema, hakuna kukawia zaidi? Kwa hivyo, hili liko na huu upaaji. Wafalme wenu wote watakuwa kama watawala wa kale, watasimama wima. Huku wakisimama kwa heshima, na karibuni watakuona. Lia, Hezekia analia. Yosaya [analia]. Mbona mko haraka kutupilia mbali ushuhuda wao, mifano yao? Nawalilia Israeli, o Yerusalemu, o Yuda. Ni nini mmefanya? Mtalipia gharama kwenye mikono yenu ya vita. [Tegemea] badala yake kwenye mikono YANGU. Kwa maana katika mikono YANGU kuna usalama, kuna ulinzi, kuna kila kitu, mnaweza tumaini. Lakini mnaona, mnafanya moyo wenu kuwa mgumu, wakati mlifanya hili, mlitelekeza tumaini, tumaini lililobarikiwa.
Mnaona, NIlituma RUAKH HAKODESH katika hiyo siku ya Pentekote, na mlidhihaki na mliambia na mlisema wanafunzi WANGU, Mitume WANGU, WANGU Waliotumwa Nje walikuwa wamelewa, walikuwa wamejazwa na divai kupindukia. Lakini ni nyinyi ambao mmelewa, mmelewa na ujinga wenu wenyewe. Na mchanganyiko geni ambao ni chukizo KWANGU. Na umeaibishwa. Kama tu ilivyokuwa katika siku za ndama wa dhahabu. Maana wakati Moshe alirudi, alifahamu sauti ya kusherehekea kwa zinaa. Sauti ya uchi, kwa aibu yenu mlikuwa uchi. Ni wewe ambaye umelewa, sio Mitume WANGU, sio wale wanaongojea mlimani, sio wale walio na moyo kama Yoshua. Maana walisimama kwa uangalifu, kwa ujasiri, na wako hapa sasa.
Mbona, O Israeli, mbona mnaendelea kutupilia mbali Torah? Kwa maana inafaidi nini mtu kuadhimisha Sherehe Takatifu, na bado aMtupe MWANANGU WA PEKEE? Hizo sherehe zinaishiria [KWAKE]! Wazimu mtupu! Bado NInafungua macho yenu. Kunao waliobaki, macho yao yako wazi na NInawatumia kufungua macho ya wengine.
Kwa maana meza zenu zimegeuka mtego kuwatega, kwa dhambi zenu za upuuzi, kiburi chenu, uasi wenu. Haingekuwa hivyo ikiwa tu mngetii. Mmeweka kumbukumbu ya Torah [akilini], mmeweka kumbukumbu ya Amri 10 [akilini] lakini herufi yaua. Lakini karibuni, Sauli watageuka Paulo. Miujiza, ishara na maajabu karibuni yatakuwa kawaida ndani yenu, O Israeli. Lakini Nawaonya, msiruhusu Sodoma na Gomora kuinuka na kuwashutumu. Ni heri mpokee Mashahidi WANGU Wawili, ni heri mpokee au hiyo miji – MWANANGU wa Pekee SHADDAI Alilaani katika ule wakati Alitembea Duniani – Miji iyo hiyo Alilaani itainuka na kuwashutumu. Msiruhusu hili litendeke, Israeli.
Korazini, ni heri muwe na ufahamu na Agano Jipya, Israeli. (Math 11:21) Ni bora muache kufukuza Wayahudi wa Kimesaniki, SIzungumzii wale wa vuguvugu, maana NItawakanyagia chini ya wayo. Wao ni wenye kuchukiza machoni MWANGU, wanavunda. Wanachafua moyo. Wengine watatubu, wengi hawata[tubu]. O nyinyi mlio vuguvugu! Mnajiita Wayahudi wa Kimesaniki lakini nyinyi ni wa Sinagogi la shetani. Nyinyi ni sababu ya wengi kukufuru JINA LANGU katika nchi yote ya Israeli, na kote duniani, mtalipa na NItakuwa na upanga WANGU wenye ncha mbili. Na kama vile NIlisema mbeleni, sio kama NItanoa upanga WANGU unaometameta, maana tayari ushanolewa. Ni muogope, ni mtetemeke.
Maana mnawajibika vikuu kabisa. Maana Watakatifu wa Kale wanakanyaga nchi ya Israeli kila siku wakinong'oneza, wakihudumu, hata wengine wakionekana kimwili kuwaonya. Huo ndio wingi wa jinsi NInawapenda. Kwa hivyo ni heri mgeuke kutoka kwa kiburi chenu, Sitaki kulazimika kuwapiga. Hamtaki kunywa kutoka kwa kikombe CHANGU cha ghadhabu. Lakini Najua ule huzuni lazima uwaangukie, Najua kile Yakobo lazima apitie. Machozi mengi, nyakati chungu, mboga chungu. Ni heri mjitayarishe kwa Farao wa Mafarao. Hiyo ndiyo tuzo yenu kwa kuNIkana MIMI, O Israeli!
O Israeli, MIMI YESHUA Naja hivi karibuni. Msikose wakati wenu wa kuzuriwa. Wakati wenu wa kufarijiwa wa kufarijika. Ni heri mshike Torah. Lakini sio kaida bure za dini za tamaduni bure. Maana ingawa mnafurahia, NDIMI NILIYE Mkuu Anawapa Neno. Bado, mnakosa pointi. Kwa maana, mnaangalia Maandiko kwa ajili ya Wokovu. Lakini mnapata tu nusu ya picha. Ni heri mkemee marabii wenu waovu. Wale ambao wanaficha na kusetiri ukweli kama Wafarisayo wa kale. Hawa nyoka wanaoudhi. Wanajua Masia ni nani. SIsemi kwamba wote wanajua, maana NInao waliobaki ambao watatubu. Lakini wale ambao wanajua, hawa reptilia, hawa wapenyezaji watalipa. Kwa hivyo Naita nchi yote kujionyesha imeidhinishwa kabla ya mtetemeko wa ardhi mkuu ambao utadhihirika kimwili na kiroho kuwaamsha, kutikisa na kuvunja kila kitu ambacho kinaweza vunjwa. Kwa sababu unaona, NInapoonya katika Kumbukumbu 8, mlipokuwa matajiri na wakwasi, mlipoingia katika nchi, NIlionya msiruhusu moyo wenu kunona. Au mngeNIsahau. Kwa hivyo lazima NIwaamshe. Lazima NIruhusu kile lazima NIruhusu. Vitisho vitawaangukia. Mizuka [viumbe geni visivyo vya hii dunia] kutoka juu, mizuka kutoka ndani na kutoka chini.
Mnaweza fanya matambiko yenu ya Kabbalah, lakini hayatawalinda. Kwa JINA na DAMU ya YESHUA pekee. Kwa hiyo tu mtalindwa, muokolewe. Na hata wafia dini WANGU wale ambao maisha yao ya kimwili yanaangamizwa. Msifikiri kwamba bado hawahifadhiwi. Kwa maana ni kupitia njia hii Nawaleta katika Ufalme wa Mbinguni. Ni kupitia hili wanaweza kutimiza wito wao. Kwa hivyo ni heri muombe saa hii kwamba wale wote ambao kweli wamezaliwa kuwa wafia dini, wafia dini Watakatifu, ni heri muombe kwamba imani yao itiwe nguvu sasa. Ili imani yao iwe tayari wakati huo. Ili wasisaliti.
Usaliti mwingi sana utafanyika wakati huo kwa sababu ya roho ya woga. Katika Israeli na kote duniani na Marekani. Tayari NIlishaonya hili katika Maandiko YANGU lakini ni nani anasikiliza? Wanapenda kuwa katika uwepo WANGU lakini inapokuja kutekeleza Neno LANGU, wanaepusha JINA LANGU lenyewe na Maneno YANGU mbali NAMI. Kwa maana NIlikuwa wimbo mzuri wa mapenzi kwao, lakini ni hilo tu, ni mfumo wa kuburudika tu.
Kwa hivyo kuweni waangalifu na hili, watoto WANGU, kuweni waangalifu. Msiache akili zenu kuwa kwa utulivu hadi kwa uangamizaji wa nafsi. Nawataka mwe watulivu, lakini SIwaambii mwe wavivu. Lakini nyakati zote mwe waangalifu, wenye kiasi, macho, kuwa tayari, kutomkadiria shetani pungufu. Kwa maana wadanganyifu watakua wadanganyifu zaidi. Na Watakatifu watakua watambuzi zaidi. Nyakati zote NItegemeeni, nyakati zote NIkiri na NItaelekeza hatua zako. Hamjui, watoto WANGU, ni mara ngapi NImewafanya mruke, mzunguke mitego ya shetani! Yote kwa sababu ya JINA na DAMU ya YESHUA. Hamwezi jiokoa, hamwezi okoa yeyote. Ni MIMI pekee, MIMI YESHUA pekee Nafanya kazi ndani yenu na kuwapitia. NInawahifadhi. Kupitia Rehema na pamoja na Neema YANGU. NInahifadhi. NInaokoa. NInafanya kipofu aone. NInafanya kiwete kupaa juu angani. NInafanya maskini kuwa tajiri. Na NInazungumzia kwanza kabisa wale tajiri wa imani. Kwa maana kutakuja wakati ambapo umaskini utashika nchi yao, katika ukataji tamaa watatupa dhahabu na fedha zao njiani, kwa kufa moyo. Lakini majonzi ya wapagani, majonzi yao ya kiuchumi, si ya watoto WANGU. Alimradi mnaweka mikono yenu safi kutokana na ghadhabu ya hii dunia, kutoka kwa njia ya kutotii.
Kwa hivyo NInataka hili Neno kwenye tovuti bila kukawia. Lakini Israeli lazima ionywe. Si juu yenu kuanzilisha Ukweli, hiyo sio kazi yenu, watoto WANGU. Kazi yenu ni kuitikia tu. Ni tu kubeba ujumbe kwa yule ameteuliwa. Wewe ni mjumbe. MIMI NDIYE MFALME. MIMI ndiYE Seremala, wewe ni nyundo, wewe ni msumeno, MIMI ndiYE Mfinyanzi, wewe ndiye udongo wa mfinyanzi. MIMI ndiYE Mchungaji Mwema, nyinyi ni kondoo. Na NInatunza kondoo WANGU, NInapiga mbwa mwitu mbali [nanyi]. NInawaokoa kutoka kwa mdomo wa simba, kutoka kwa dubu. Na NInaua mara moja. Watenda uovu. Wale ambao wanadhuru wafanya kazi WANGU ikiwa hawatatubu.
Msiwe katika mawimbi ya bahari, mkitupwa mbele na nyuma. Sio kama meli iliyoshikwa katika kimbuga na kutupwa kwa nguvu kwenye jabali. Lakini bakini kwenye njia ya NDIMI NILIYE MKUU. Kaa kwenye njia. Kwa maana kila mmoja wenu anaNIpendeza, sikuzote kuweni katika amani. Usiruhusu maarifa ya kujua wewe ni kazi inayoendelea, kutumika na shetani kukushutumu. Hakuna mmoja wenu aliyekamili, lakini NInawakamilisha.
Kwa hivyo msisikilize sauti ya shetani. Lakini kwa sauti ya MCHUNGAJI MWEMA NDIMI NILIYE MKUU. Na jueni tu kwamba manabii wote, mitume wote wa kale, wanawalinda, wanasimama tayari kuwasaidia, iteni tu JINA LANGU. MIMI YESHUA. Ulizieni tu hekima zaidi, ufahamu zaidi, imani zaidi, msiaibishwe na ushuhuda wenu ndani YANGU.
Comments