top of page

Unabii 48 “Israeli, Siku ya BWANA iko Karibu!”


Umepewa Nabii Shemayah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 21 Mei, 2019Ujumbe wa Kinabii


[Maombi ya Shukrani]


"Dhiki ya Yakobo i mlangoni! Israeli, geukeni! Lilieni nchi yenu! Maana mpinga-kristo yuaja! Lilieni nchi yenu! Shule zimenajisiwa [na] mafundisho ya uongo. Na mnahitaji kurudi KWANGU. Maana wengi ya watu wenu watadanganywa! Na mnahitaji kuNIrudia! Torah, Sheria ya Torah bado yafaa siku hizi! Na ni wangapi mnatii? Watoto wadogo wananajisiwa na uongo, na hili ni chukizo KWANGU. NImemalizana na utovu wa shukrani wa hii dunia, ikijumuisha wewe, Israeli. Wakati unafaa usimamie Utakatifu, unaleta aibu kwa JINA LANGU.


Maadui wana[wa]lemea mlangoni. Jitoe kwenye picha na uNIrudie! Kwa maana unaishi kwa minajili ya tamaa ya mwili !Na haujui kwamba unaenda kuhukumiwa kwa hili? [ABBA YEHOVAH Amechukizwa na karama zisizodhibitiwa katika Israeli] Uvunjaji sheria umeenea. Na Naja karibuni! Lakini mpingakristo yuaenda mbele [YANGU]! Na wangapi mtapokea ukweli? Na imeandikwa muda wote katika Maandiko na Torah yenu. Tafuteni na mtapata. Geukeni kutoka kwa kiburi chenu na mjinyenyekeze. NIrudieni. NIruhusuni NIfungue macho yenu kwa nuru ya Neno LANGU. Kwa malhamu YANGU ya uponyaji ya Gileadi. Lakini ili hilo lifanyike toba ya kweli lazima itendeke.


Maovu makuu lazima yatendeke! Kabla mgundue hamko sahihi! O yahuzunisha kweli? Siku ya huzuni kwa Israeli! Kuona barabara zimefunikwa na damu! Mpingakristo anavyokuja, mtu wa uvunjanji sheria. Na yote mnayopaswa kufanya ni kuita JINA LANGU. Lakini hata hilo limewekwa mbali nanyi. Lakini iko juu yenu, kuchukua hizo hatua, kuNItafuta na moyo wako wote! Maana mnayo Maandiko Matakatifu! Maana mara moja mlikuwa mmetengwa (kwa Utakatifu)! Sasa yote NInaona ndani yenu ni uhalifu! Nini Natanyahu anafanya? Bali kutia moyo. Na wapi uongozi ambao utaonyesha watu WANGU kurudi? [Maono ya Naftali Bennett waziri wa elimu] Anafanya kazi nzuri, lakini wapi uongozi wa kweli? Wale ambao wanasimama na sheria ZANGU na hawatarudi nyuma!


Dhoruba yaja! Na inaenda kuwatupa kupitia kitanzi! Na mnapaswa kujitayarisha! Kwa maana mwisho umekuja! Na kuwasili KWANGU kuko karibu sana; kusafisha hii dunia na najisi iliyomo ndani yake! Kutoka bahari hadi bahari NItarejesha! Ardhi, bahari, vitaponywa! NInapoleta malhamu YANGU ya uponyaji wakati nyayo ZANGU zitagusa Mlima wa Mizeituni. MWOKOZI wa dunia, MWOKOZI wa Israeli! Kuponda maadui WANGU! Wakati wote wanaletwa mbele ZANGU! Na NInasema, ueni wale ambao hawakutaka kuNIabudu! Ueni wale ambao walikuwa maadui WANGU! Maana Ninawawezesha nyinyi, watoto WANGU. Na mamlaka yaliyopewa kutoka Mbinguni! Na mtakuwa NAMI!


Hata sasa, NInatawala toka Mbinguni ikiwa watakiri au wasikiri huo utawala. Lakini wakati utakuja na huo wakati unakuja, watakapoona MWANA wa MUNGU na Utukufu wote wa BABANGU. Na mioyo itaanguka kwa maana wengi wataona wingi gani wa taabu wako ndani! Mioyo yao itasimama. Woga na hofu iliyoje kwenye nyuso zao! Mawe hayawezi waficha! Ingawa wanaita mawe yawaangukie ili kuwaficha kutokana na ghadhabu ya MWANAKONDOO. Lakini hakuna chochote kilichofichika KWANGU. Hata ukijitupa katika vimo vya bahari. Hata ukitafuta nyota Mbinguni. Ungeweza kuenda wapi mbali NAMI? MAANA MIMI NI MWENYEZI MUNGU! Mkono WANGU unafika miisho ya dunia! Umbali wa miisho kabisa! Na hakuna kujificha kutoka KWANGU!


Israeli! Rekebisheni! Kwa maana hakuna muda zaidi kwako! Na NIlingoja vyakutosha. Kile kitu kinachofuata kinaenda kuwasababisha uchungu mwingi sana! Kwa hivyo ni wakati wa kuamka! Na kuita juu ya JINA LANGU! Watu WANGU! Mko wapi? Najua pale mlipo! Lakini ni heri mjitokeze sasa! Kwa maana hakuna muda zaidi! Na ni wangapi kweli mnaNIjua? Hiyo ndio maana lazima muite juu ya JINA LANGU sasa! Watu WANGU Israeli! Muda baada ya muda, lazima NIwaadhibu. Lakini hii ni tofauti, kwa maana hiki ni kitu ulimwengu haujawahi ona mbeleni. Kwa maana maadui wenu wanataka kuwamaliza. Na kuwafagia kutoka kwenye uso wa hii Dunia.


Lakini hakuna anayeweza fanya chochote ambacho SIruhusu! Kwa maana hakuna anayeweza tweza DAMU YANGU! Ijapokuwa wengi wenu mnafanya hivyo! Maana ni katika Israeli DAMU YANGU ilimwagika. Na ilikuwa ni kwa ajili yenu – na Msalaba si tu wa Wakristo. Ni wa nyinyi wote! Kwa hivyo NIkimbilieni MIMI! Kwa sababu Nawakujia kuwakomboa kutoka kwa mkono wa maadui wote! Wale wanaowachukia, wanaowadharau, wanawaita magaidi! Tafadhali NIsikilizeni! Kwa maana Namwaga machozi juu yenu! Tafadhali acheni NIwaokoe! Acheni NIwaponye! Kwa maana MIMI NDIYE MWOKOZI wenu pekee! Hakuna mwengine!


Lakini bado, yule bandia anakuja! Na ni wangapi mko tayari? Oh ni ukweli. O hizi kambi zitakuwa zimejawa na nyinyi! Na msifikiri kwamba Nataka kuona hili! Hiyo ndiyo maana Nawapa Ahadi kwamba NInawakujia! Ili muweze kutazamia anga ya Mashariki. O watoto WANGU! Na mjue kwamba NInawakujia! Kwa maana NInaenda kuwaponya. Kupanguza machozi yote. Halafu hakutakuwa tena na dhambi! Lakini lazima kwanza Tuifanye njia YANGU. Na hiyo inahitaji nini?


Bali mkubali, mlilie DHABIHU pekee ya DHAMBI! Kwa maana hakuna njia nyingine kuenda Mbinguni! Haijalishi chochote kile mtu yeyote anakuambia! Hakuna mwengine aliyekamili! Wote wametenda dhambi na kupungukiwa na UTUKUFU wa MUNGU! Ni jambo la kuogofya kuanguka katika mikono ya MUNGU ALIYE HAI! Utapatikana wapi siku hiyo? DAMU ya YESHUA inakufunika au la? OGOPA! Utaanguka kwenye uso wako! Ukitetemeka! Ukipatikana bila DAMU YANGU! Ukiwa uko katika kikundi cha la – na Nakwambia, “NIondokee, wewe mtenda maovu, kamwe Sikuwahi kujua!” (Mathayo 7:22- 23) na ijapokuwa NIlikuumba, MIMI Sipendelei mtu yeyote. Na kadiri ya itakavyoumiza, bado Nakuambia “NIondokee, ewe mtenda maovu maana kamwe Sikuwahi kujua!” Kwa maana MIMI pekee YANGU Naumba, na MIMI pekee YANGU Napeana uhai! Na uhakikishiwe hili, MIMI pekee YANGU huchukua uhai! Nachagua nani ataishi na nani atakufa. NInavyo vifunguu vya Jahanam maana NIlilipia gharama! Hakuna yeyote wa kuNIambia kile cha kufanya!


Kwa hivyo NIsikieni NIkiwalilia! Geukeni sasa maana Marekani SIO TUMAINI LENU! Wanahitaji usaidizi wao! Kwa maana hiyo bendera ya Marekani kwa hakika yaenda kuchomeka! Wako kwenye mashua moja nawe! Watajawa na zile kambi! Jifunzeni pale pa kuweka tumaini lenu! Haipaswi iwe tu [katika] MUNGU (weka tumaini lako katika MUNGU pekee)? YULE YULE AliYEkutana nanyi kwenye Mlima Sinai? Ambapo huo mlima uliwaka moto! Na nyinyi nyote mlisikia Sauti YANGU! Vile mlisikia kile Natarajia kutoka kwenu! WATU WATAKATIFU! Lakini mmekuwa mengine ila [hilo]! Hata hivyo, Nawapenda! Na upendo wa milele. Msipuuze Neema YANGU kwa maana muda unayoyoma. Mtakapofikia muda, hakuna zaidi. Na umeishiwa! Umeishiwa! Umeishiwa! Kwa hivyo wekeni tumaini lenu ndani YANGU! YEHOVAH! YESHUA HAMASHIAKH ni MWANANGU!


(Naona [maono ya] rais wa China). China kwa hakika itavamia Marekani! Na NIna adhabu ya kipekee ya rais wa China. Jinsi anavyoNIdhihaki! Wewe si mungu yeyote! Si mfalme mkuu yeyote! Kwa kweli, umefilisika! Na utaanguka, Ukomunisti utaanguka! Maana Ufalme utakaosimama pekee ni Ufalme wa MUNGU! Kwa hivyo tazama! NInapokusongesha kwenye ubao WANGU wa sataranji, OH vipande VYANGU vidogo songeni kwa amri YANGU. Jinsi ulivyo mdogo na dhaifu kupigana dhidi YANGU! Mkono WANGU wa kulia! Vita vitakuja! Vita vya kiwango kisichowazika! Viko karibu sana sasa! Viko karibu sana sasa! Mayowe, vurumai, wengi sana hawatajua wafanye nini katika woga! Kule kupiga mayowe! Kwa hivyo utapatikana wapi? Utapatikana wapi? Utaweka tumaini lako katika serikali fulani? Ambao wataishia kukupeleka kwenye kambi au mbaya zaidi?


Au utaweka tumaini lako katika MKONO WA KULIA WA MWENYEZI MUNGU? YESHUA HAMASHIAKH? Juu YAKE utasimama? MWOKOZI wa ulimwengu. MWOKOZI wa pekee wa ulimwengu. Na ingawa kuna bandia, mmoja tu Atasimama, mmoja tu ndiYE Anasimama! Hakuna chochote kama MIMI! YESHUA HAMASHIAKH! Kwa hivyo tubuni siku hii! Kwa hivyo tubuni siku hii! Na mNIpe maisha yenu, weka maisha yako mkononi MWANGU. Na NInakuahidi, hautabaki kamwe kuwa yule yule! Kwa maana Naponya na Naokoa. Najaza furaha yako! Furaha ya maisha haujawahi jua, na tumaini la utukufu! Maisha yasiyoisha! Paradiso iko Edeni! Lakini kuna njia moja tu kuenda huko.


Mwisho wa Neno

0 views

Recent Posts

See All
bottom of page