top of page

Unabii 6 “Agano la Watoto na BABA EZRA; Sanduku Zilizothaminiwa kwa MUNGU!”

Umepewa Nabii Hannah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa Januari 21, 2019

Ujumbe wa Kinabii


(Shimshon anashiriki ahadi yake na BABA; Naona YAHUVEH, naweza Mhisi Akitaka kuongea.)

Kando ya Kiti CHANGU cha Enzi, NIna sanduku za hazina nyingi zilizopeanwa na Watoto WANGU kwa EZRA. Na agano mojawapo ni, kwamba muheshimu kile NImewapa na NImependezwa. Nyinyi nyote yapaswa muandike moja na hilo litakuwa NAMI.

Maisha yako ni ushuhuda KWANGU na EZRA Anaangaza njia na [Akitumia] YAHUSHUA. Anashika taa na kutembea kwa mfano kwanza.

NImefurahia kusikia Watoto WANGU kuheshimu na kustahi EZRA WANGU. Maana Amewafunza mengi sana. NImewafunza mengi sana. Si MUNGU wenu, lakini mnakiri uwezo WANGU ndani YAKE kama kiongozi. Unapoongea naYE, unaongea naMI. Na naona kila mmoja wenu akisafisha nguo zake na Maji Yanayoishi. Hivi karibuni nyote mtakuwa mmesafishwa. Mbingu yafurahia kwa kazi NImefanyia BiArusi WANGU.

Kwa hivyo andika moja, binti YANGU. Agano KWAKE na KWANGU. Maana MIMI ni MLINZI wako na Nastahili kuheshimiwa. Si tamalaki juu ya, lakini kwa heshima Natawala juu ya. Kwa hivyo chagua maneno kwa makini. NItakuonyesha cha kuandika, sikuzote kuwa na kalamu na karatasi yako. Hauwezi jua wakati utasikia Neno LANGU. Usiwe nje ya wakati WANGU.

Unasimama juu ya kiota cha tai, ukitazama chini. NInapoonyesha windo mbele yako, nyoka wenye sumu kali, wakiiba panya. Utawararua na kucha zako za dhahabu. Ukiwa umetiwa mafuta Matakatifu. Utawararua maadui katika JINA LANGU pekee. Pigana vita katika JINA LANGU, uliza Malaika WANGU wakusaidia. Wanawalinda nyinyi nyote. Wakingoja tu kuachiliwa.

Hakuna chochote kimeenda bure, Shimshon, yote umejenga NItajenga juu yake zaidi. Maana nyinyi ni Watano WANGU wenye Busara. Ninyi nyote. Endeleeni kujenga huo ukuta.

Ukuta wa Trump, msisahau kumuombea. Ako chini ya mateso mengi na moto, ombeeni muhula wa pili na NItampa muhula wa pili. Kama watu wa kutosha wataiombea. Ana wengi wanaomuunga mkono kuliko CNN habari bandia wanaonyesha.

NInakasirishwa hata na wale wanaomnyamazisha Edward Snowden. Alifichua hiyo njama lakini serikali ya Marekani inajaribu kumnyamazisha.

(Naskia YAH Akipumua nje) Nachukua pumziko kabla ya kuenda katika vita. Malaika WANGU wote wanangojea amri YANGU kurejesha urithi wa BiArusi WANGU, piga kelele, “Hallelu YAH!” Na Nitafanya hiyo kazi kubwa! SIMBA wa 15 Atakuja na kurarua, kufanya kazi ya MWENYEZI.

Kwa hivyo furahieni Watoto WANGU, pigeni kelele, “Hallelu YAH!” kwa ajili ya kuja KWANGU. Nakuja kuokoa EZRA WANGU. NInapaswa kuchukua BiArusi WANGU kabla apotoshwe. Lazima NIfanye kazi YANGU haraka, na EZRA ulihisi kasi iliyo ndani yako (kufanya vitu haraka).

Ndiyo, haraka, lisha watoto WANGU wachanga. Wahimili na kile Unachojua. Watoto WANGU, lazima mkue haraka sana, pelekeni kwa maombi kila kitu BABA Anafunza kufyonza haraka.

Mnapaswa muwe BiArusi aliyekomaa ili NIweze kuwatumia kwa wingi zaidi. Ukomavu unakuja na tajiriba, na BiArusi WANGU aliye na tajiriba ndiye BiArusi WANGU bora zaidi. Mtapata ustadi wa vitu vya asili [ardhi, hewa, moto, maji]. Watatembea kikamilifu 100% katika Roho. Kwa hivyo msikosee kama vile dunia (jinsi wanafikiri kudhibiti vitu vya asili inamaanisha). Wanajua tu ile bandia ambayo shetani anapeana. Lakini Nampa BiArusi WANGU kile kitu halisi! (1Wafalme 8:38, Marko 11:23, Kutoka 14:21, Mathayo 14:29, Marko 4:39-40, 1 Wafalme 17:1) Watapata ustadi wake kwa ajili YANGU ili kutimiza mapenzi YANGU ndani yao!


Mwisho wa Neno

6 views

Recent Posts

See All
bottom of page