top of page

Unabii 79 “Virusi vya Korona ni Shule ya Msingi Ikilinganishwa na Kinachofuata!”

Updated: Jun 14


Umepewa Nabii TORAH KEEPER kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 10 Aprili, 2020

Nilikuwa nasikia YAH Akisema, “Giza, giza, giza.”


Ujumbe wa Kinabii


Ee Marekani, Niliwaonya kama katika siku za Moshe mnapokula pigo la 8, na vile Nzige wanavyokula mazao yenu na kama vile Virusi vya Korona vinaenea kama kipukusa (Kutoka 7:25-8:15). Ee, Nzige wanaleta pigo la nane katika njia kubwa, kuu na ya uharibifu! Mnafikiri mmeona uharibifu tayari!? Ngojeeni tu pigo la nzige! Bado hamjaona lolote ee, China!


Bado hamjaona lolote ee Marekani! Ee Indonesia mnafuata! Ingia katika patakatifu kabisa, watu WANGU (Waebrania 9:1-28).


Inuka, mwanangu. MIMI ndiye Mtoaji wa kilele wa johari! Nawashika watoto mikononi MWANGU, pajani MWANGU (mbinguni) na Nawafunza siku baada ya siku. Nachukua muda WANGU na watoto. Kwa maana moyo WANGU ni huruma. Moyo WANGU ni rehema (Zaburi 116:5). MIMI ni kiakisi cha BABA kilichodhihirika katika umbo hili.


[Maono: Na naona maono ya nyumba na naona maono ya mawimbi yakija mlangoni mwa nyumba halafu naona wimbi la tsunami likija kuipora hiyo nyumba.]


Ikiwa haujajengwa kwenye mwamba imara na Namaanisha mpendwa WANGU YESHUA, utaanguka kama shimo la kinamasi; katika mchanga unaozama mtaenda. (Mathayo 7:24-27) Mateso yataangukia kila nafsi zenu katika moto wa jahannamu. Maana tazama MIMI ni YEHOVAH! BABA Aliyedhihirishwa na YESHUA kama MMOJA! Kwa maana mko katika nyakati za mwisho na nyakati zinabadilika, na nyakati zinapangika upya. SISI ni MUNGU yule yule jana, leo na milele; ndio, na wokovu unapatikana pekee kupitia JINA LANGU, MIMI YESHUA (Warumi 9:9-10) na kupitia damu YANGU, ndio. MIMI na BABA YANGU ni MMOJA.


Na hivi ndivyo Najaribu moyo wenu katika hili. Mnaona, yote ni jaribio watoto WANGU wapendwa kote dunia hii. Nanena nanyi, ee Dunia!


Na Indonesia! Ikiwa utakataa... ikiwa utanikataa MIMI, MIMI YESHUA na YEHOVAH, mtakula pigo la 8, na Niamini, kipukusa unachoona sasa SI CHOCHOTE ikilinganishwa na kile kinachokuja! Nitaachilia mama wa nzige. (Tazama kitabu cha Ayubu kuhusu Pigo la Nzige.) Atapanda kutoka kwenye shimo la kuzimu. Na atakapotokea, kutatokea pigo la 8 kutoka kwa mdomo wake. Nyinyi mataifa yote jitayarisheni! Kwa maana hofu itaondosha na kuua mioyo ya wengi. Mnafikiri virusi vya Korona vilikuwa vibaya!? Hili ni shule ya chekechea, shule ya watoto wachanga! MIMI ni YEHOVAH na SIFANYI mzaha nawe ee Dunia pumbavu! Nyinyi wanadamu, Dunia dhaifu, hamjui kuwa MIMI, YEHOVAH, Nawezafyekua kwa kidole CHANGU? Nakutoa kwenye ekseli.


Nawatoa kutoka kwa kumbukumbu ya zama. Mmenijaribu kwa muda mrefu sana ee dunia! Wapi toba?! (2 Mambo ya Nyakati 7:14) Wafalme wameenda wapi kwa toba kama siku za Yona?! Uko wapi, ee Dunia!? Nimekasirika! Na moshi unapanda kutoka kwa chumba cha Kiti CHANGU cha Enzi; kutoka kwenye mianzi ya pua LANGU! Kuleni pigo la 8! Nimemalizana nanyi ee Dunia, Nimemalizana, Nimemalizana! Lakini, ee watoto WANGU Sijawasahau! Farijini moyo wa MIMI YEHOVAH!

Msinisahau. Hata mnapoteseka, msinisahau! Nikumbukeni mnapokula, mnapofunga, mnapokunywa. Msinisahau, ee Dunia! Mmenisahau! Je mwanamke anaweza sahau mtoto wake na asihurumie mwana wa tumbo la uzazi wake?! Na kwa hakika wamenisahau lakini Sijawasahau, ee Dunia! (Isaya 49:15)


MWANANGU Alimwaga damu YAKE kwa ajili yenu! Nimewasafisha katika Maji ya Uzima! Niliwazaa kutoka kwenye maji [hayo]! (Mathayo 10:40-42) Nasikitikia watoto WANGU! Ee Sijawasahau, ee dunia! Sijawasahau! Nawapenda! Bado Nawapenda! Bado Nawapenda! MIMI ni YEHOVAH! NA KATIKA hasira YANGU inayochemka moto kuliko jua, ee Dunia! Laja juu yenu na linapanda juu yenu, pigo la 8 lililohifadhiwa moja kwa moja toka kwa chumba CHANGU cha kiti cha enzi, lililochochewa katika bakuli la hukumu, MELEKH-TSEDEK! YUKO hapa! MELEKH-TSEDEK Anawaonyesha vile itakavyokuwa kuchochea – mnapochochea hasira YANGU (Zaburi 110:4)!


Ee New York, jitayarishe, tsunami yaja ufukweni mwenu! Na wale wote ambao hawajaathiriwa na virusi vya Korona hawatapona! Ni masalio wachache sana hawataangamizwa na watapona. Sifanyi mzaha nanyi, ee Dunia! Volkano zitalipuka! Volkano itafoka! Ee Hawaii, Indonesia, jitayarisheni, jitayarisheni, majipu, kipukusa, majipu, majipu.

Mwisho wa Neno.

©2019 by Torah Keeper.

bottom of page