top of page

Unabii 8 “Njooni Kwenye Mlima Kuabudu BABA Pamoja na MIMI, YESHUA!”

Updated: Apr 14

Umepewa Nabii Hannah kwa sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 23 Januari, 2019

Ujumbe wa Kinabii


Ee Watoto WANGU, NImefurahi mnaNIpa Utukufu! Ndiyo, NIabudu MIMI, bila – kukoma! Furaha nyingi NInayohisi. Kwa hakika NInatukuzwa na kuteseka kwenu, kuumia kwenu.


Hawakuwahi elewa kwa nini watu WANGU hufurahia katika dhiki. Lakini silo hilo kile Neno LANGU linasema? Furahia katika kuteseka KWANGU, ni kwa manufaa yenu. Inajaribu moyo wenu, kuona kile kiko chini kabisa.


Ndiyo, cheza naMI! NIonyeshe hatua yako inayofuata! Nyinyi nyote mnaNIletea furaha nyingi mno. NInazihifadhi [hizo sauti]. Sio wengi wanaoNIimbia kwa kweli tena. Na NInaye Mfalme WANGU Daudi wa Sasa ambaye anaNIletea ibada ya kweli. Watoto, ibada ya kweli yatoka moyoni mwako, sio ikiwa unaimba katika tuni au mahadhi. Kwa hivyo msidanganywe, NIimbieni tu, MWOKOZI wenu. NIimbieni bila kukoma. Inasongeza vitu pia. Uwezo wa ibada ni mkubwa zaidi ya mnayofikiri.


(Ndimi za YESHUA) Inavunja Jahanamu! Inavunja laana zilizo juu yako! Wakati inaunganishwa na Meza ya BWANA, ni yenye uwezo mkubwa zaidi!


Hakuna kinachoweza shindana na Utukufu WANGU uliofunuliwa katika ibada. Abudu JINA LANGU, ‘YESHUA’. JINA juu ya majina yote. YULE mnaYEpenda, ee kabisa.


NInatamani ibada. Inafariji moyo WANGU. Kama NIlivyotoa dhabihu maisha YANGU. Natarajia kukumbukwa kwa hii kazi kubwa ya kihistoria. NIlitoa maisha dhabihu kwa ajili ya Marafiki WANGU. NIliwafia. Misumari ilidunga mikono YANGU, ee kwa uchungu sana. Lakini NIlikumbuka kila moja ya majina yenu, na NIkajiwezesha kufanikiwa.


Sasa NIko hapa kutukuzwa na Natukuzwa! Asante! Asante kwa ibada! Ukweli ni, sio wengi walioNIjali.


Kuja NAMI, Mpendwa WANGU. NItakupenda na zaidi. Imba NAMI, wimbo WANGU wa mapenzi. NItafunza kila mmoja kibinafsi. NImetia fikra moyoni mwa wengine tayari, Nangoja tu idhihirike kupitia njia nyingi za kazi zenu. Upendo WANGU – ambao unashinda kazi zote za shetani – ee, ovu kabisa. Mipango miovu. Itabatilishwa. Kazi zote zisizo ZANGU. NItatangua na kuinua wale ambao ni WANGU. Wako kwenye Mlima Sayuni pamoja NAMI. TUnaabudu BABA pamoja.

Sikizeni sauti YANGU, amri YANGU. Sivunji matumaini. MIMI ndiYE NENO Linaloishi, haliwachi kuongea kamwe. MIMI ni UNABII, na haukomi hadi Mbinguni. Mtakuwa NAMI, hakutakuwa na hitaji.


NENO LANGU LINAISHI, Linatiririka chini kutoka mlima ulioinuka juu sana. Kutoka pahali pa YEHOVAH pa kibinafsi. Anawapa iliyosafi kabisa kunywa.


Ufufuzi, radi – mtakuwa na upendo zaidi kwa kila mmoja wenu. Utafufuliwa. Wengine wamekufa kwa ajili ya ukatili wa dunia, lakini katika JINA LANGU wanafufuliwa. Itateketeza kwa nguvu zaidi. Kwa hivyo msiwe na wasiwasi Watoto WANGU, mnao Upendo WANGU, mnahitaji tu kukamilishwa ndani YANGU.


Wale walio dhidi YANGU, mlikosa kuelewa mengi kuNIhusu. Je, MIMI si MFALME wa Kiyahudi? Mbona mnataka kutelekeza Torah YANGU? NIlikuwa tu na Torah ambayo NInaweza zungumzia kuhusu. Agano la Jipya halikuwa. Ndiyo, MIMI ni vitabu 2 katika moja. Hakuna utengano. Hakuna utengano, lakini mnatenganisha wenyewe.


Dunia nzima ni YANGU! NInafanya njia YANGU kutoka chini kwenda juu. NInafanya kazi katika Miujiza. Si wengi wanaelewa, au wanataka kusoma. NInayo Miujiza YANGU, inayofanywa kwa imani.


(‘Ni nini kiko kwenye moyo WAKO?’ Niliuliza) Moyo WANGU umekazia dunia, ukitafuta nani anayeNItafuta. Wakati unakuja, karibu sana sasa, wa mlango kufungwa (naona mlango wa Safina ukifunga). Wengi watalilia fursa iliyopita. Ingia kwenye Safina haraka! Usikawie! Safina yako iko wapi? Je, Niko ndani yake? NIsikilize, unapaswa kurudi. Tunahitaji kufanya kazi pamoja. Tunahitaji kuwa pamoja, sio kutengana.


UsiNIsahau katika wakati wako mgumu sana. NIabudu MIMI, NIimbie, NIbusu. Nakuficha chini ya mikono YANGU. Nakukumbatia na upendo WANGU, na mabusu.


NIrudie MIMI, Yerusalemu. Hebu tujadiliane. NIrudie, mpendwa WANGU. Sijakutelekeza. UmeNIsahau. Kwa hivyo kawia naMI kidogo zaidi, Tutaimba pamoja. Lakini rudi. NIsikilize. Kaa ndani YANGU. Rudi. ‘Mtakatifu WANGU’ – Ningependa NIkuite hivo sasa, lakini Siwezi. NIrudie ukiwa umesafishwa safi katika akili. Kukataa Torah ni kuNIkataa MIMI! (YESHUA Alia) Lakini MIMI ni Mstahimilivu na Mvumilivu.


Nyinyi ni Vifaranga WANGU wachanga. NInawalinda chini ya Zaburi 91. Ikariri kila siku, kila asubuhi. Msisahau. Mnathaminiwa sana. Fanyeni tu kazi yenu ili NIweze kuwalinda. Kila mmoja wenu ana moyo WANGU. Fanyeni kazi pamoja ili Mwili WANGU uungane. (Ndimi za YESHUA).



Mwisho wa Neno

9 views

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page