top of page

Unabii 86 “Siku ya Upatanisho – YEHOVAH Amehukumu Dunia!”


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa usiku wa Yom Kippur (27-9-20) na mchana (28-9-20)


Maandiko Husika


Kumbukumbu 10:12-13

12 Na sasa, ee Israeli, YEHOVAH MUNGU wako Anataka nini kwako ila kuMcha YEHOVAH MUNGU wako, kwenda katika njia ZAKE, kuMpenda na kuMtumikia YEHOVAH MUNGU wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, 13 na kuyashika maagizo ya YEHOVAH na amri ZAKE ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?

 

Zaburi 29:1-2

1 Mpeni YEHOVAH, enyi mashujaa,

Mpeni YEHOVAH utukufu na nguvu.

2 Mpeni YEHOVAH utukufu unaostahili JINA LAKE;

Mwabuduni YEHOVAH katika uzuri wa utakatifu WAKE.


Ujumbe wa Kinabii

Hukumu! Hukumu! Hukumu imekuja kwa hii sayari iitwayo Dunia. Uvundo wa dhambi umefikia mianzi ya pua ZANGU. MIMI, YEHOVAH, Nawatema nje, ee Dunia! Wako wapi wenye haki? Wako wapi watakatifu? MIMI, YEHOVAH, NInao waliosalia wachache. NInawalinda kwa wivu, kwa maana je, MIMI siYE MUNGU wao (Zaburi 23)? MIMI, YEHOVAH, Nasema “naam” na “amina.”


ALEF na TAV wako hapa – WAWILI na bado UMOJA (Isaya 61:1-4). WAnaakisi MFANO WANGU. WAnaakisi UTUKUFU WANGU. MIMI, YEHOVAH, NImeWAvika taji kama WAFALME wa UTUKUFU (Zaburi 24:7-10). Selah. Inama, ee dunia, na upige magoti mbele ZANGU! Pokea hukumu yako. Kwa maana umekuwa dhalimu mbele ZANGU kama hayawani wa shambani – ukienda baada ya Sheria ya Uwezo. Wapi Haki? Wapi rehema? Wapi ukweli?


Mika 6:8 “Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu na YEHOVAH Anataka nini kwako ila kutenda kwa haki na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na MUNGU wako?


MIMI, YEHOVAH, NImewapa wanadamu maagizo – sheria na amri zilizoshuhudiwa na moyo WANGU mwenyewe (Kumbukumbu 6:4-9). Kutoka kwa wingi wa moyo mdomo unazungumza. Chemichemi za uzima zinatiririka kutoka kwa moyo, moyo WANGU. Uadilifu, wema hivi vitu NImempa mwanadamu. Lakini mwanadamu amefanya nini? Wamevunja moyo WANGU vile wamevunja amri ZANGU (Warumi 3:23). Neno LANGU linasimama imara na kweli kwa wanadamu wote. MIMI si heshimu hadhi ya yeyote. Macho YANGU yanaenda mbele na nyuma toka upande mmoja hadi mwingine wa hii dunia. Ni nini NInachoona?


Sheria ZANGU zimetupwa kando na kupendelea uasi! Uasi ndio uchawi wa sasa. SItaruhusu Sheria ZANGU zibadilishwe na uongo! MUNGU Hadhihakiwi (Wagalatia 6:7-8). Kile mtu apandacho ndicho atakachovuna. NIsikie, ee dunia! Ogopa MUNGU na Mpe UTUKUFU! Mpe UTUKUFU na staha inayostahili JINA LAKE (Zaburi 29:1-2).


Karibuni NItahukumu hii dunia katika njia ambayo kamwe haijawahifanyika. Nyota za Mbinguni zitaanguka kwenye dunia hii ikisababisha uharibifu mkuu (Mathayo 24:29, Isaya 34:4). Uharibifu mkuu. Wapi Safina yako sasa, ee dunia? Nakukejeli sasa. Subira ya kale. NIlikuwa na uvumilivu mkubwa katika nyakati zilizopita. 28-9-2020 Kicho cha YEHOVAH ni safi, nacho chadumu milele (Zaburi 19:9). Hamna kicho CHANGU MIMI na wala hamko wasafi. Dunia nzima, ulimwengu mzima uko katika uovu. Upotovu unazaa upotovu na mtavuna kile mnachopanda, ee ulimwengu.


Hakuna taifa moja Naweza ita takatifu, Naweza ita adilifu. Lakini NItakurudishia uadilifu, ee Israeli. Wakati toba itatirika kutoka kwako kama mto, ndipo kutakapokuwa na uzima (Warumi 11:11-15). Kwa maana itasemwa, “Kutoka huko kunatoka uzima.” NItazatiti Kiti CHANGU cha Enzi katika Israeli, katika Yerusalemu pale ambako Sanduku la Uwepo WANGU linakaa. NItakuwa na watu watakatifu na wakweli mbele ZANGU; bila uongo, bila unafiki (Isaya 10:20-23). Wenye uso mmoja. Wenye akili moja. Hawa ndio watu ambamo NInafurahia. Kondoo wa malisho YANGU. Mfugo wa Mkono WANGU wa Kulia. NInalinda kwa wivu mifugo WANGU, tufaha la jicho LANGU. MIMI NIna mtazamo mmoja, NIna fokasi, NI imara na Mkweli. Neno LANGU halidanganyi.


Ee marabii, marabii! NItawafananisha na nini? Walaji wa mifugo? Wachungaji wa kondoo WANGU? NItawafananisha na nini? Je, mnaNItumikia katika ROHO na katika UKWELI? NItawafananisha na nini? Haya ndiyo maswali NInayo kwenu siku hii. Maana usjiite WANGU ikiwa hauhubiri na kufunza UKWELI. Na UKWELI ni nini? MIMI, YESHUA, ndiYE Njia, UKWELI na Uzima (Yohana 14:6). MIMI ndiYE njia kuelekea kwa Torah, ya kuishi sawa mbele za BABA. Fuateni mfano WANGU. Fuateni Ukweli WANGU na muache kukana JINA LANGU, maana hamna kisingizio mbele ZANGU.


Nawatumia washauri na manabii wenu wenye hekima, lakini mnawafanyia nini? Vile mmewafanyia, ndivyo mmeNIfanyia (Mathayo 25:31-46). Kwa maana mtumishi si mkuu kuliko Bwana wake. MIMI ndiYE BWANA wao. Huu ni Ufalme WANGU. Tubuni au mjipate nje siku ya Hukumu. MIMI, YESHUA, ni huru na wote wanaojipata ndani YANGU wako huru kweli (Yohana 8:31-36). Tubu dhambi zenu na muoshwe katika DAMU YANGU iliyomwagika. Hakuna dhabihu kuu zaidi, hakuna tendo kuu zaidi la utiifu.


MIMI ni Mkarimu; [Na]nyosha mkono WANGU kwa watu wakinzani mchana kutwa (Isaya 65:2-7). Katika nini hamjaNIkinza, ee Israeli? Katika nini hamjakuwa wasiotii? Mababa zenu walitenda dhambi dhidi YANGU nanyi mnaendeleza dhambi zao. Wote wamekatiwa kauli kuwa wenye hatia. Lakini NIlifia wote ili wote waweze kushiriki ufufuo WANGU. Lakini ni chaguo lenu. Ni chaguo lenu ikiwa mtatii au la. NIngependa mchague uzima. MIMI NDIYE UFUFUO na UZIMA (Yohana 11:25-26). NIchagueni na mtaishi. Hakuna chaguo lingine, hakuna njia nyingine.


Uhuru mtapata ndani YANGU. Amani mtaishi ndani YANGU. MIMI ndiYE Njia, Ukweli na Uzima. Hakuna yeyote anayekuja kwa BABA ila kupitia MIMI. Ee Israeli, taifa kinzani na la kurudi nyuma, NInawaita. Je, mnasikia mlio wa shofar? Je, mnasikia kilio cha moyo WANGU? NIrudieni naMI NItawarudia.

Mwisho wa Neno.

©2019 by Torah Keeper.

bottom of page