top of page

Unabii 87 “Msiwe na Wasiwasi Bali mwe Walinzi Usiku!”


Umepewa Nabii Hannah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 29 Septemba, 2020


Maandiko Husika


Zaburi 23:4

Hata kama nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti,

sitaogopa mabaya, kwa maana WEWE upo pamoja nami;

fimbo YAKO na mkongojo WAKO vyanifariji.


Luka 21:36

Kesheni daima na mwombe ili mweze

kuokoka na yale yote yatakayotokea na

kusimama mbele ya MWANA wa Adamu.


Ufunuo 16:15

Tazama, Naja kama mwizi! Amebarikiwa yeye akeshaye

na kuziweka tayari nguo zake ili asiende uchi

na kuonekana aibu yake.

Ujumbe wa Kinabii

Acheni wasiwasi wenu utiririke chini ya mto hata kama vile vifusi hubebwa na kupelekwa baharini na kuzikwa katika vina – katika bahari la sahau. MIMI ni ELOHIM wenu AnaYEshughulikia mahitaji yenu yote. Kulingana na utajiri WANGU katika UTUKUFU, NInatoa na kupeana (Wafilipi 4:19). Hamna lolote la kuhangaikia. Tu NIkazieni fokasi. NIkazieni fokasi na mtazame wasiwasi wenu ukibebwa, ukiondolewa, hata kama matawi yaliyotawanywa kuelekea kona nne za dunia kutowahi kusanywa tena.


MIMI ndiYE YULE MSHINDI; NImepuuzwa na wengi, wachache wameNIjali na bado NDIMI NILIYE daima yuko nanyi. Msitokwe jasho. Msitoe chozi. NItumainieni tu katika njia zenu zote, kwa maana Najua kilicho bora zaidi, je, sivyo? Kwa hivyo NItazameni. Fuateni mfano WANGU. Tangu lini NIshawahi wapotosha? Kuwapitisha katika bonde la mauti, naam. Lakini ili tu mpate ushindi (Zaburi 23:4). Kamwe SIwachi kondoo WANGU nyuma, kamwe SIwaachi waliwe.


Nafukuzia kondoo aliyepotea lakini SItelekezi kundi (Mathayo 18:12-14). JINA LANGU ni “NDIMI NILIYE” na kamwe SIsaliti Uso WANGU. Nia moja NInayo MIMI katika njia ZANGU zote, kwa maana MIMI ni UMOJA. Katika vimo vya juu kabisa NInaishi. Chini ya chini kabisa Naenda na NImeenda kuokoa watu WANGU toka kwa mitego ya jahanam.


JINA LANGU ni YESHUA – BWANA juu ya yote. NIlikuja. NIkaona. NIkashinda. NIlishinda kifo, jahanam na kaburi. Na sasa NInaketi na BABA YANGU. “YEHOVAH” ndiyo JINA LAKE – MFALME wa UTUKUFU. Sikiza Sauti YANGU, kwa maana MIMI NI WOKOVU. Hamtapata katika mwingine utajiri katika UTUKUFU kama huu. Kupitia MIMI unatiririka uzima wenu. Natuma METATRON kuwaonyesha Njia (Kutoka 23:20-23). Kamwe HAsaliti misheni, mwito KWANGU ANIpendeza. YEYE ni NDUGU YANGU AliYEjaribiwa na Mkweli. MRITHI PAMOJA NAMI katika UTUKUFU WANGU wote, kwa maana NInashiriki pamoja na yule NInayeshiriki.


Wewe ni nani, ewe mwanadamu, kusema vingine? Neno LANGU halidanganyi. Yule anayeNIheshimu MIMI, YESHUA, anaheshimiwa na BABA YANGU AketiYE juu ya mafuriko, misimu, nyakati, zama [nyingi] (Yohana 12:26). Jichunge, ee mwanadamu, na usikanyagie chini, usitendee dhambi amri ZANGU. Kwa maana wengi wamekuja mbele yenu na kama wao, mtaanguka; kuuawa katika jahanamu kutowahi inuka tena.


Kaeni katika mwangaza WANGU. Tembeeni katika hatua ZANGU. Mambo yako karibu kuwa rafu. Mambo yako karibu kuwa ya muhimu sana. Kuweni wenye kiasi (1 Petro 5:6-11). Kuweni macho. Ni mara ngapi lazima NIonye mwe walinzi katika usiku, walinzi kwenye ukuta? Nini kilitendekea Babeli? Hawakuweka ulinzi usiku na wakashindwa, wakatwaliwa, wakaangamizwa (Danieli 5). Taifa litainuka dhidi ya taifa na ufalme dhidi ufalme lakini msipatikane pungufu. Kwa maana Nachukua tu Bi-Arusi ambaye ni mwangalifu, aNIangaziaye macho, aNIkaziaye macho (Mathayo 25:1-13). Kwa hivyo wekeni nyumba yenu katika utaratibu, watoto WANGU. Kuweni waangalifu katika huu msimu wa neema. Kolezweni na neema na msisahau rehema ambayo ikikosa hakuna wokovu. Selah.


Mwisho wa Neno.

©2019 by Torah Keeper.

bottom of page