top of page

Unabii 83 “MIMI, YESHUA NdIYE NYOTA YENU ANGAVU ING’AAYO!”

Updated: Mar 23


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 29 Aprili, 2020


Maandiko Husika


Yohana 14:6

YESHUA Akamwambia, “MIMI NDIMI Njia, na Ukweli, na Uzima; mtu haji kwa BABA, ila kwa njia ya MIMI.


Zaburi 118:26

Na Abarikiwe YEYE Ajaye kwa JINA la YEHOVAH;

TumeKUbariki toka nyumbani mwa YEHOVAH.


Ujumbe wa Kinabii


NItazame MIMI, mwanaNGU, NYOTA yako ANGAVU ING’AAYO ya UTUKUFU na KUDURA. MIMI ni YESHUA MFALME wako, MWENYE HAKI wa ZAMA. Umetajwa baada YANGU MIMI. MIMI ni KICHWA chako. WEWE ni Bi-Arusi WANGU. Endelea kutembea katika njia ZANGU imara, kwa maana ndani yake hautawahi enda makosa. Mipango YANGU kwa ajili yako ni imara na hakika, bila ufa katika msingi, kwa maana MIMI NDIYE MSINGI wako. JIWE KUU la PEMBENI NDIMIMIMI (Matendo 4:8-12).


Kanyaga* juu YANGU (Yohana 14:6). Tembea naMI, kwa maana SItawahi kuangusha. JINA LANGU ni YESHUA YULE wa MILELE wa ZAMA. MIMI NIko kama BABA YANGU MFALME wa UTUKUFU. NImeumbwa na NImeundwa baada YAKE [Yaani kwa mfano wake]. NImezaliwa naYE na MAMA YANGU SHEKINAH GLORY, YULEMREMBO waZAMA (Yohana 3:16). YEYE (SHEKINAH GLORY) yuko naMI popote pale NIendapo, kwa maana MIMI ni mwaminifu kwa BWANA ALIYE JUU SANA.

NIfuate na Mfuate BABA NDIMI NILIYE MKUU (Yohana 10:30). YEHOVAH ndiyo JINA LANGU. YEYE YUko ndani YANGU na MIMI NIko ndani YAKE. TUnafanya kazi pamoja kuzalisha matunda mengi mazuri ndani yako. TUruhusu kukamilisha kazi iliyoanzwa ndani yako, kwa maana, kuu na ya kustaajabisha ni mipango TUnayo kwa ajili yako, kudura ya nafsi yako iliyoimarishwa kutoka zamani (Yeremia 29:11). Hauna habari ya vitu vizuri TUmehifadhi kwa ajili yako. Kuwa tu mnyenyekevu na uendelee kutembea katika upendo na ndugu zako. TUruhusu kukukamilisha katika huo upendo, kwa maana upendo kamili hutupa nje yote hofu (1 Yohana 4:18).


NIKO hapa kukuokoa. MIMI ni MFALME na SHUJAA wako MSHINDI. NInatawala na kumiliki kutoka milele na NIna mamlakayote juu ya wakati. Katika wakati na katika umilele NIlishinda shetani. yuko chini ya mguu wako, mwanaNGU, kama vile njia na njama zake zote (Luka 10:19-20). Usimuogope, kwa maana NDIMI NILIYE yu nawe. Mkuu zaidi ni YULE AliYE ndani yako kuliko yule aliye duniani (1 Yohana 4:4). Karibuni yule dragoni mkuu atatupwa nje. Karibuni njia zake zitafika kikomo.


MIMI ni MKUU juu ya Wakati na Nafasi. Yote yameshikwa mkononi MWANGU. Hakuna aliye mkuu kuNIliko ila BABA YANGU (Yohana 14:28). Tilia maanani njia ZAKE, kwa maana NIko ndani YAKE na YEYE yu ndani YANGU. SISI ni UMOJA. Shema Yisrael, YAH ELOHEINU, YAH EKHAD. NIsikieni, ee Israeli (Kumbukumbu 6:4). NImekuwa Nawaita kupitia enzi. Mtakuja KWANGU. Kupitia maji na kupitia moto mtakuja. Lakini haitakuwa ya kufurahisha. Neno LANGU halidanganyi, ni kama nyundo, kama moto! NItavunja katika vipande yale mabonge, mioyo ya mawe. Inamisheni dhamira yenu KWANGU, ee Israeli! Kunyweni kutoka kwa Kikombe cha Mateso. Mnakataa kuNIfuata sasa. MtaNIfuata wakati huo. Wakati itakuwa ni kana kwamba kila kitu kimepotezwa na nchi yenu iko karibu kumezwa, NItatokeza mtakapolia kwa sauti, “BARUKH HABA BISHEM YEHOVAH ELOHEINU! BARUKH HABA BISHEM YEHOVAH ELOHEINU!” (Zaburi 118:26, Mathayo 23:37-39).


Halafu NItatokeza na moto machoni MWANGU, MIMI, YESHUA, MFALME na MASIA wenu! NIsikize ee Israeli, na msikawie tena! Msikawie tena katika kutupilia mbali desturi za wanadamu! Wengi wa marabii wenu ni makaburi yaliyojaa mifupa ya wafu (Mathayo 23:27-28). Kwa nje wanaonekana wazuri, wamepambwa, wamevishwa katika vitani vizuri kabisa, mavazi mazuri kabisa. Lakini Nawaambia sura ya kitu yawezadanganya. Kwa maana SIkusema, SIkuonya msitazame umbali mwingine na macho ya mwili, macho ya umalaya, ya uovu?


Mwili wenu unashirikiana na shetani. Lazima mtoke katika milki ya mwili. Msiende kwa hisia, watoto WANGU wapendwa. Kwa maana mtadanganyika mara kwa mara. Yote yaliyopo hapo ni uchungu wa moyo na maumivu, zana na taabu. Paeni juu zaidi naMI, MIMI, YESHUA wenu. NIko hapa. Nawapenda na upendo wa milele. Njoni KWANGU na acheni NIwaoshe safi. Na MAJI na DAMU iliyotiririka kutoka upande WANGU, acheni NIwa takase safi kwa ndani na nje (Yohana 19:33-37). NIko hapa kuwaokoa, watoto WANGU mahabubu. Msikose fursa yenu, kwa maana nani yuajua kile siku yawezaleta.


MIMI ni ALFA na OMEGA, ALEF na TAV (Ufunuo 1:8). Fanyeni kazi za BABA YANGU na mtakuwa mnaNIheshimu, kwa maana Sote lazima tuwe juu ya shughuli za BABA YANGU (Luka 2:49). Muda ni mfupi sana kwa hivyo fanya kile umeitwa kufanya na ifanye upesi. Usiku waja wakati hakuna mtu yeyote anaweza fanya kazi (Yohana 9:4). Naam, nyota ZANGU zitang’aa kwa wangavu, lakini fanyeni kile mmeitwa kufanya na msikawie tena. Selah.


*YESHUA ndiYE Njia ambayo tunafaa tutembee juu yake


Mwisho wa Neno.

6 views

Recent Posts

See All

Comments


Commenting has been turned off.
bottom of page