Umepewa Torah Keeper kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 14 Februari, 2019
Maandiko Husika
Mathayo 5:17-19 “Msidhani kwamba NImekuja kufuta Sheria au Manabii; Sikuja kuondoa bali kutimiza. Kwa maana, amin Nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yoyote kutoka kwenye Sheria, mpaka kila kitu kiwe kimetimia. Kwa hiyo, yeyote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, lakini yeyote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme wa Mbinguni.
Mathayo 19:16-21 “Mtu mmoja akamjia YESHUA na kuMuuliza, “MWALIMU Mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?” YESHUA Akamjibu, “Mbona unaNIuliza habari ya mema? Aliye mwema ni MMOJA tu. Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.” Yule mtu akaMuuliza, “Amri zipi?” YESHUA Akamjibu, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama nafsi yako.” Yule kijana akasema, “Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?” YESHUA Akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze vitu vyote ulivyo navyo, na hizo fedha uwapemaskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, uNIfuate.”
Warumi 10:9 “Kwa sababu kama ukikiri kwa kinywa chako kwamba “YESHUA ni BWANA,” na kuamini moyoni mwako kwamba MUNGU AliMfufua kutoka kwa wafu, utaokoka.”
Muhtasari
Tafadhali jaribu kuelewa huu ujumbe hapa. Kumbuka, dhambi ni kuvunja sheria (1 Yohana 3:4), na dhambi ni kuvunja amri za MUNGU. YESHUA Alikuja chini kutoka Mbinguni kutukomboa kutoka kwa athari za makosa yetu na dhambi/kuvunja sheria YAKE. Sasa, kama vile Paulo asema, na Paulo daima anawaambia waumini wasivunje sheria (Warumi 3:31; 8:4; Mathayo 5:17; Yakobo 2:10-11), kuelewa tu kwamba kutii sheria kwenyewe hakuwezi okoa nafsi ya yeyote (Warumi 3:20; 10:4; Wagalatia 3:10), lakini kwa kushika sheria za MUNGU na PIA kukiri MASIA YESHUA yeyote anaweza okolewa (Mathayo 19:16-22; Warumi 10:9; Matendo 16:31; Yohana 14:21,23; 15:10; 1 Yohana 2:3; 4:15; 5:3). Biarusi anataka kufanyia zaidi MASIA, ambayo inamaanisha, tunataka kutembea maili zaidi kwa ajili ya BWANA. Kile Alituamuru, tunafanya, na yale mengine katika tamaduni za Kiyahudi ambayo yanatukuza BABA MUNGU YEHOVAH, tunafanya pia. Huu ni uhusiano wa upendo na MUNGU. Tunasihi kila mtu anayesoma hizi Unabii kutia hili akilini.
Ujumbe wa Kinabii
Hapa ndipo Amri zilizaliwa. Ni mahali katika chumba cha karibu kabisa moyoni MWANGU. Kwa maana hizo Amri zimo moyoni MWANGU. Fumbo kubwa – kuna fumbo kubwa katika hili. Kuna sababu wale wanaotii Sheria ZANGU wanainuliwa, kwa sababu hii ni MIMI. Ukikataa Sheria ZANGU, unaNIkataa MIMI.
Sheria ZANGU ni aminifu na kweli (Zaburi 19:7-11). Yeyote anayesumbuka kutii Sheria ZANGU 10 NItasema “NIondokeeni enyi watenda uovu, kwa maana Sikuwahi wajua!” (1 Yohana 3:4; 5:2-3, Yakobo 2:10-20, Hosea 4:6)
Kwa hivyo endeleeni Watoto WANGU Wachanga – jitahidini kutii. Jitahidini kuishi Takatifu. Kuweni Watakatifu kwa kuwa MIMI ni Mtakatifu (1 Petro 1:16, Walawi 19:2, 20:26). Sheria ZANGU zimetengenezwa kutokana KWANGU MIMI! Vito vya Moyo WANGU vyote vinaashiria Sheria ZANGU. Kwa maana MIMI ni Mtakatifu! Pasipo MIMI, hakuna sheria.
Ondoka KWANGU MIMI, hakuna Torah. Ee, jitahidi! Jitahidi kuwa Mtakatifu! Usiwe baridi. Usiwache siku ipite bila kujichunguza (1 Wakorintho 9:27; 2 Wakorintho 13:5). Acha Amri ZANGU na Sifa ZANGU ziwe kwenye midomo yako bila kukoma. Kuweni wenye akili komavu watoto! Msiruhusu shetani aibe kile NImewapa. Msiruhusu dhambi iibe kila kitu NImefanya. Njooni KWANGU! Njooni chini ya Maji YANGU Yaliyo Hai. Njooni, njooni, njooni KWANGU MIMI!
Maana kuweni Watakatifu hata vile NIlivyo Mtakatifu (1 Petro 1:16; Walawi 19:2). Nawapenda enyi Watoto WANGU Watakatifu. Huruma. Onyesheni ufunuo mpya wa mfumo mpya wa upendo na huruma na kuweni Watakatifu katika hizi nyakati ovu. Mtahitaji kukua haraka.