Unabii 18 “NDIMI NILIYE Ako Karibu Kuwasha Moto Katika Nyumba ya Israeli!”
Updated: Apr 14
Umepewa Nabii Natan’EL kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 6 Machi, 2019
Maandiko Husika
Yeremia 7:23-26
“Lakini NIliwapa amri hii NIkisema: NItiini MIMI, naMI NItakuwa ELOHIM wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Enendeni katika njia zote NInazowaamuru ili mpate kufanikiwa. Lakini hawakusikiliza wala kujali. Badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Walirudi nyuma badala ya kusonga mbele. Tangu wakati ule baba zenu walipotoka Misri hadi sasa, siku baada ya siku, tena na tena NImewatumia watumishi WANGU manabii. Lakini hawakuNIsikiliza wala hawakujali. Walikuwa na shingo ngumu na kufanya maovu kuliko baba zao.’”
Isaya 29:13-14
YEHOVAH Anasema: “Watu hawa huNIkaribia kwa vinywa vyao na kuNIheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami. Ibada yao KWANGU inatokana na maagizo waliyofundishwa na wanadamu. Kwa hiyo mara nyingine tena NItawashangaza watu hawa, kwa ajabu juu ya ajabu. Hekima ya wenye hekima itapotea, nayo akili ya wenye akili itatoweka.”
Ujumbe wa Kinabii
Ee, Nyumba ya Israeli, NInakutazama kwa wembamba, Asema YEHOVAH BWANA wako. NInakutazama na miale ya moto katika Macho YANGU. NDIMI NILIYE Ako karibu kuwasha moto, karibu kuwasha. Nani anaweza zima hasira ya ALIYE JUU KABISA? Na ni maji yapi yanaweza izima? (Yeremia 7:20)
NDIMI NILIYE Anajaribu mioyo ya wanadamu, Anajaribu kuona ni nani anatosha kusimama mbele ZANGU, kuona nani anastahili kuinuliwa. Nafurahia katika kubariki Watu WANGU. Utiifu ni bora kuliko dhabihu (1 Samueli 15:22). Wapi utiifu wako, ee Nyumba ya Israeli?
Hili linaNIchukiza! Mwanaume kulala na mwanaume (Walawi 20:13, Warumi 1:27). Mwanamke kuachilia usafi wake katika ukahaba. Maovu yapi mengine yapo ambayo haujainua mkono wako kwake?
Hili linaNIchukiza! NItakuhukumu, [Nita]ruhusu uone ghadhabu ya MWANAKONDOO (Ufunuo 6:16-17). Ngoja tu hadi SIMBA wa Yuda Atakaporuka toka kwa maficho (Isaya 31:4). Ngoja tu na uone. Mambo yanaenda kuzidi kuwa magumu – baraka kupungua, kupotea. Maana Najaribu kupata usikivu wako lakini unasisitiza kwenye uasi, kwenye njia iliyotiwa vibamba kwa unono na upana zaidi.
NItazame MIMI na utetemeke, ee Nyumba ya Israeli! NItazame MIMI na unyooshe vipaumbele vyako! Siku hii Naja chini kukagua mioyo ya wanadamu katika mahali pa kimya, mahali pa siri (1 Wakorintho 4:5). Ni bora NIsipate kitu kilicho najisi, kichukizo katika nyumba YANGU, katika hekalu yako. Acha kitu kinacholeta aibu kiwekwe mbali na wewe, kutoka kati yako, ee Nyumba ya Israeli.
Naja chini na moto, na tochi mkononi MWANGU. Nani anaweza himili siku ya kuja kwake, siku ya jairibio lake? Siku ya mtumishi WANGU (Malaki 3:1-5)! Atasimama kujaribu mioyo na nafsi za Levi na wanake. Pamoja na fimbo ya enzi mkononi mwake atasimama, akitangaza na kuamuru Utawala WANGU, Sheria na Utaratibu WANGU. Kwa hivyo tazama na mtahadhari, ee dunia, maana hakutakuwa na huruma ndani yake. Kwa maana mumejaribu uvumilivu WANGU wa zama, wa dahari.
NItasimama ndani yake na chochote anachofanyiwa ni kama kinafanyiwa MIMI, MIMI YEHOVAH! Tahadharini! MsiNIjaribu! Msijaribu Mjumbe WANGU wa Agano. Yuaja na upendo katika JINA LANGU na katika JINA la MWANANGU YESHUA.
Anaongozwa na ROHO, ROHO MTAKATIFU WANGU wa Moto na Upepo. Msitie majaribu funzo lake, kwa maana si yake, kutoka kwake, lakini KWANGU. Anakuja kufunza Njia, Ukweli na Uzima (Yohana 14:6). Mnajua mambo haya, ee Israeli. Lakini, mbona hamsikizi (Zaburi 81:11-12)? Mbona bado mnafanya mioyo yenu migumu, mnakaza shingo zenu? Je, mwajua hukumu yenu itakuwa kali zaidi, nzito zaidi kuliko wale waliokufa jangwani? Maana walikuwa bado hawajaingia Nchi ya Ahadi, lakini nyinyi mmeingia. Mnayo historia yote imefunuliwa kwenu, ikishuhudia dhidi yenu, dhidi ya uhalisia wenu – chukizo.
Kwa hivyo ingieni katika laini, ee Israeli! Ingieni katika utaratibu, maana NItawaua katika sehemu ya mwisho kabisa. NItaweka wazi ufa wako na kufichua mapengo yako, NIkipaaza sauti dhambi zako kutoka kwa paa za nyumba za wakati, za milele (Ezekieli 22). NItazima nuru yako, moto wako geni na kusafisha hekalu. Utaratibu WANGU, Laini YANGU, Moto WANGU vitaishi mara tena katika nchi ya Israeli. Utakuwa tena mrembo sana wa kutazama lakini hata mara mingi zaidi ya nyakati za kale, kwa maana NItakaa ndani yako. [Halafu nikasikia, “Hallelu YAH!”, ambayo ilitoka kwa wingu la mashahidi (Waebrania 12:1)]
NItakutakasa, Mzuri WANGU, Biarusi WANGU, Muhibu WANGU. Utakuwa umevishwa katika nyeupe pe inayometameta – ng’aa, meremeta. Kwa hivyo, NItazame MIMI, ee Biarusi WANGU, na uamke. Amka na usiogope, Kipenzi CHANGU. Naja karibuni, Naja upesi, upesi kuliko kufumba na kufumbua. NItakusafisha ili NIweze KUkukumbatia (Ezekieli 36:25). Biarusi WANGU lazima awe takaso, lazima awe tayari na atakuwa. Biarusi WANGU wa kweli atakuwa tayari, bila doa na safi.
Kwa hivyo ingia kwenye laini na sikia, ee Israeli, kwa maana MIMI NI MMOJA, EKHAD (Kumbukumbu 6:4). Kwa hivyo tetemeka mbele ZANGU na jua kwamba NDIMI NILIYE ni upendo na NDIMI NILIYE pia Amesawazika katika vita. Hautaki vita na MIMI, maana NItashinda na utapoteza. Haudhihaki “NDIMI NILIYE” MKUU na ufikiri unaweza kwepa (Wagalatia 6:7-8). NIdhihaki ikiwa utadhubutu! Ni nafsi yako iliyomo hatarini.
댓글